Fursa: Ufadhili katika masomo vyuo vikuu “Scholarship” nchini Uturuki

Uongozi wa waturuki wanaoishi nje ya nchi na jamii zinazohusiana (YTB) umetangaza kuanza kupokea maombi ya wanafunzi wa kimataifa katika elimu ya vyuo vikuu wanaotaka kufanya mafunzo yao Uturuki. Maombi ya udhamini  kwa mwaka 2019 yameanza kupokelewa.

Udhamini unaotolewa na Uturuki kupitia YTB unawawezesha wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali kudhaminiwa katika masomo ya fani mbalimbali katika vyuo vikuu maarufu nchini Uturuki, Ni aina ya Ufadhili ambayo inajulikana kwa kuwa na  ushindani mkubwa.

Maombi ya ufadhili wa Uturuki kwa mwaka 2019, yameanza kupokelewa Januari 15 mwisho wa kupokea maombi ni Februari 20. Kufanya maombi ni bure. Maombi kwa njia ya posta au kwa njia ya mkono hayatakubaliwa.

Wanafunzi wote wanaotaka ufadhili kwa daraja ya shahada ya 1,2 na ya 3 ” Bachelor, Masters na PHD” wanaweza kutuma maombi yao kupitia anwani ya mtandao ifuatayo “www.turkiyeburslari.gov.tr

error: Content is protected !!