Eid ul-Fitr 2019: Nchi kadhaa zikiwemo Rwanda, Uganda zasherehekea Eid leo

Muumini

Waislamu nchini Rwanda na Uganda hii leo (Jumanne Juni 4, 2019) wanasherehekea sikukuu ya Eid ul-Fitr na kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Jijini Kigali, waumini wa dini hiyo wakiongozwa na Mufti wao Sheikh Salim Hitimana wanatarajiwa kusali sala ya Eid katika viwanja vya Nyamirambo.

Mufti huyo alitoa tangazo la Eid nchini humo Jumatatu jioni, sawa na Uganda ambapo Baraza Kuu la Waislamu pia lilitoa tangazo kama hilo.

Katika salamu zake za Eid, Mufti Hitimana amewanasihi waislamu kuendelea kutenda mema kama walivyokuwa wakifanya katika kipindi chote cha Ramadhan.

“Nautakia Umma wa Kiislamu Eid Mubaraka, nawanasihi waendelee na matendo ya upendo, kujikagua nafsi zao na kumcha Allah na kufanya kazi kwa bidii kama walivyofanya katika kipindi chote cha mfungo,” amesema.

Nchi nyengine barani Afrika ambazo leo ni sikukuu ya Eid ni Somalia, Ethiopia, Sierra Leone, Jamuhuri ya Congo.

Nchi yenye ushawishi mkubwa kwenye masuala ya mwezi muandamo, Saudi Arabia imetangaza Eid leo, hii inamaana kuwa kuna baadhi ya waislamu ambao japo mamlaka za nchi zao hazijatangaza Eid watasherehekea leo kulingana na tangazo la Saudia.

maakuli

Nchi nyengine zinazosherehekea Eid leo ni pamoja na Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain.

Kwa kawaida mwezi wa ramadhan hukamilika kwa siku 29 ama 30, kulingana na kuandama kwa mwezi.

Eid ul-Fitr Jumatano

Msikiti

Tofauti ya kuanza kufunga na kusherehekea Eid miongoni mwa waislamu zaidi ya bilioni 1.8 duniani kote ni mjadala ambao uanaendelea kufukuta na bado hakuna suluhu iliyopatikana.

Na pia yawezekana suluhu juu ya tofauti hizo isipatikane, na kila upande kuendelea na msimamo wake.

Tayari mataifa kadhaa ikiwemo Kenya yameshatangaza kuwa leo ndio siku ya mwisho, yaani mwezi 30 Ramadhan na kesho Jumatano, Juni 4 2019 ndio itakuwa sikukuu ya Eid ul-Fitr.

Mataifa mengine kama Japan, Malaysia, Australia, Misri, Uingereza na Morocco pia yametangaza kuwa Eid itasaliwa Jumatano.

Eid ul-Fitr Alhamisi ?

Waislamu Tanzania leo watatazama mawinguni jioni kuangalia endapo mwezi utaandama.
Waislamu Tanzania leo watatazama mawinguni jioni kuangalia endapo mwezi utaandama.

Kuna mataifa ambayo leo ni mwezi 29 Ramadhan, kama Tanzania na Oman.

Hii ina maana kuwa, waumini katika mataifa hayo leo wataangaza mawinguni baada ya jua kuzama kuutafuta mwezi.

Ukionekana, kesho Jumatano itakuwa Eid kwao.

Endapo hawatauona, basi watamalizia kufunga siku 30 na Eid kwao itakuwa Alhamisi.

Eid ul-Fitr ni nini?

Maakuli huwa ni sehemu muhimu ya maadhimisho ya sherehe za Eid.
Maakuli huwa ni sehemu muhimu ya maadhimisho ya sherehe za Eid.

Eid ul-Fitr maana yake ni “sikukuu ya kumaliza mfungo” na kutumiwa kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Siku hii huwa ni siku rasmi ya mapumziko katika mataifa mengi yenye waumini wengi wa Kiislamu. Hata hivyo idadi ya siku za mapumziko huwa tofauti katika nchi mbalimbali.

Waislamu huanza sherehe hizi kwa kukusanyika kwa maombi ya kila mwaka ambayo hufanyika muda mfupi baada ya macheo.

Ni kawaida kuwaona Waislamu wakikusanyika katika misikiti na viwanja vya wazi kwa maoni ya pamoja.

Kabla ya ibada hiyo, huwa wanatoa sadaka kwa maskini (huitwa Zakat ul-Fitr) ambayo ni moja ya nguzo kuu katika dini ya Kiislamu.

Ni kawaida kwa miji mikuu mataifa ya Kiislamu kupambwa sana na sherehe kubwa kuandaliwa, watoto kununuliwa nguo mpya na kupewa zawadi mbalimbali.

CHANZO: BBC

error: Content is protected !!