Dondoo za Afya

Watafiti kadhaa wamedai kuamka mapema hufanya mwili kuchangamka na kufanya mambo kwa ufanisi zaidi. Anayeamka mapema anakazia fikra kukamilisha kazi zake mapema hivyo kutimiza mengi hadi mwisho wa siku.

Watafiti wa Chuo Kikuu Rochester wamegundua mtu anaposinzia husaidia ubongo kuondoa protini hatari zinazotokana na shughuli za siku nzima tangu kuamka. Usipopata usingizi wa kutosha protini hatari hubaki kwenye ubongo wako na kuathiri utendaji wa ubongo mfano kufikiri.

Watafiti wamedai ni rahisi kukubaliwa na mwanamke/mwanaume anayevutiwa na harufu yako wakati ukimtongoza. Watafiti wamedai harufu ina sehemu kubwa katika mahusiano ya watu.

Kunusa ni moja ya milango muhimu sana kwa binadamu, hutusaidia kufahamu mazingira mazuri, chakula kizuri n.k. Kunusa pia kunahusianishwa na kumbukumbu ya mtu, hisia na jinsi mtu anahusiana na watu. Harufu nzuri humvuta mtu wakati harufu mbaya humfukuza mtu.

Hasira huchochea sehemu ya ubongo inahusiana na kusema kweli ndio maana wengi hufichua siri nzito wakiwa na hasira.

Kusukutua meno kutasaidia kuuweka moyo wako kwenye afya njema. Wenye matatizo ya fizi & meno wana hatari 25-50% ya kupata magonjwa ya moyo.

Kukaa sehemu ile ile kwa muda mrefu kila siku huongeza hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu na kupanda viwango vya lehemu (kolesteroli).

Tafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa mazoezi mbalimbali mfano kukimbia yanaweza kukufanya mwenye furaha na ujisikie vizuri.

Utafiti umebaini kufanya ngono kunaweza msaidia mtu kupunguza wasiwasi (anxiety), msongo wa mawazo (depression) & mkazo (stress) mara 10 zaidi ya dawa za matatizo hayo eg valium.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia, Canada wamedai kunusa nguo ya mpenzi wako aliye mbali nawe huweza saidia kupunguza mkazo (stress) kwa maana wanawake wana mfumo mzuri wa kunusa kuliko wanaume.

CHANZO: TIBA FASTA

error: Content is protected !!