Updates

Wenye chuki na Uislamu Denmark waivunjia heshima Qur’ani tukufu kwa kuuchoma moto msahafu

Wenye chuki na Uislamu Denmark waivunjia heshima Qur’ani tukufu kwa kuuchoma moto msahafu

Jamii, Kimataifa, Siasa, Updates
Katika harakati nyingine ya uenezaji chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), kiongozi wa chama kimoja cha mrengo wa kulia chenye misimamo ya kufurutu mpaka nchini Denmark ameuchoma moto msahafu mbele ya jengo la bunge la nchi hiyo. Wakati Waislamu kadhaa wakiwa wamekusanyika kusali Sala ya Ijumaa hapo jana mbele ya bunge la Denmark, kama ishara ya kulaani jinai ya hivi karibuni nchini New Zealand pamoja na kuonyesha mshikamano na manusura wa tukio hilo la kigaidi, Rasmus Paludan kiongozi wa chama chenye misimamo ya kufurutu mpaka cha mrengo wa kulia nchini Denmark kiitwacho Stram Kurs, alifanya kitendo cha kichochezi na kifidhuli cha kuuchoma moto msahafu. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, wafuasi kadhaa wa chama hicho waliokusanyika umbali wa mita 10...
Chai: chanzo kikubwa cha mapato nchini Uturuki

Chai: chanzo kikubwa cha mapato nchini Uturuki

Biashara & Uchumi, Updates
Uturuki imeuza chai yenye thamani ya dola milioni  1,674,434 nje kati ya Januari-Februari. Kulingana na ripoti ya DKİB, Uturuki imeuza tani 666 za chai nje ya nchi katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu. Katika kipindi hicho cha mwaka jana, milioni 1 208,000 231 ya mapato yalipatikana kutoka tani 416 za mauzo ya chai. Hivyo, mauzo ya chai katika kipindi hicho yaliongezeka kwa asilimia 60 na asilimia 39 kwa thamani ikilinganishwa na kipindi hicho cha mwaka uliopita. Uturuki imeonekana kuiuzia chai kwa sana nchi ya Ujerumani (109,363,000) ikifuatiwa na Ubelgiji dola 239,710,000 na Ufaransa kwa dola 225, 543,000. Uturuki huuzia chai nchi mbalimbali ulimwenguni na kiasi cha mauzo hayo ya nje kinaonekana kuongezeka.
UTAFITI: Uhalifu unaotekelezwa na waislamu  wazungumziwa kwa asilimia 357 katika vyombo vya habari kuliko uhalifu  unaotekelezwa na wasiokuwa waislamu

UTAFITI: Uhalifu unaotekelezwa na waislamu wazungumziwa kwa asilimia 357 katika vyombo vya habari kuliko uhalifu unaotekelezwa na wasiokuwa waislamu

Jamii, Kimataifa, Updates
Uhalifu unaotekelezwa na waislamu  wazungumziwa kwa asilimia 357 katika vyombo vya habari kuliko uhalifu  unaotekelezwa na wasiokuwa waislamu. Vyombo vya habari vya Magharibi  vimekwepa kutumia  neno « shambulizi la kigaidi » kuzungumzia shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya waislamu Christchurch na kuuawa kwa  watu 50 bila shaka ni  kwa sababu lengo ni kuonesha kuwa waislamu pekee ndio magaidi na kupandikiza chuki dhidi ya waislamu. Asilimia 357 ya mashambulizi yaliendeshwa na waislamu  imezungumziwa katika vyombo vya habari Magharibi  ikilinganishwa na  matendo mengine ya uhalifu yaliotekelezwa na  wasiokuwa waislamu. Vyombo vya habari vya Magharibi havikutumia neno « shambulizi la kigaidi » ka
65 wafa kwa Kimbunga Ida Zimbabwe

65 wafa kwa Kimbunga Ida Zimbabwe

Jamii, Kimataifa, Updates
Watu 65 wamekufa Mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga Ida hata hivyo kati ya watu waliopoteza maisha katika shule mbili ambapo tufani hiyo iliwakumbwa usiku wa manane wakiwa wamelala. Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu wa miundo mbinu katika jimbo la Manicaland karibu na mpaka za Zimbabwe na Msumbiji. Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani walioko,hali inahofiwa kwamba huenda inaweza ongeza idadi ya waliopoteza maisha. Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake mashariki ya kati ili kurejea nchini mwake kutokana na janga hili. Hata hivyo kasi ya kimbunga hicho inapungua,japo kuwa tayari kimesababisha madhara makubwa huku takribani watu 200 wakiwa hawajulikani walipo. Famia nyingi...
Msumbiji katika hatari kimbunga kingine kikali kikitua

Msumbiji katika hatari kimbunga kingine kikali kikitua

Jamii, Kimataifa, Updates
Kimbunga Idai kinatarajiwa kuikumba Msumbiji Watu wanaoishi katika mji mkuu wa Msumbiji Maputo wameonywa kutokea kwa hali mbaya zaidi kutokana na kimbunga kikali. Tufani iliyopewa jina la Idai, ambayo inabeba upepo wenye kasi ya kilomita 225 kwa saa itasababisha kimbunga kikali karibu na bandari ya Beira, mji wenye watu wapatao laki tano. Mvua kubwa iliyonyesha nchini humo tayari imesababisha vifo vya watu 100 nchini Msumbiji na Malawi. Beira ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Msumbiji ambapo bandari yake iko katika mdomo wa mto Pungwe ambao umekwenda mpaka Zimbabwe. Kitengo cha hali ya hewa cha Ufaransa ambacho kinashughulikia maeneo yanayodhibitiwa na Ufaransa katika eneo la Bahari ya Hindi kimeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya kutokana na maji kuj...
error: Content is protected !!