Updates

Mawakala wa mitandao ya simu wanaofanya kazi kinyume na sheria wawindwa na TCRA

Mawakala wa mitandao ya simu wanaofanya kazi kinyume na sheria wawindwa na TCRA

Biashara & Uchumi, Nyumbani, Updates
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA  Zanzibar Bi. Esuvatie Masinga akichukuwa maelezo kwa mmoja wa Mawakala wa Usajili wa Simu na Tigo Pesa katika eneo la Darajani Zanzibar wakati wa zoezi la kubaini Mawakala walikuwa hawajasajiliwa na Makampuni ya Simu na kutokuwa na vibali vya makampuni hayo. MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania TCRA ofisi ya Zanzibar kwa kushirikiana na jeshi la polisi imeendesha zoezi la kuwakagua na kuwakamata mawakala wa mitandao ya simu za mkononi wanaoendesha shughuli hizo kinyume cha sheria za TCRA.  Zoezi hizo ambalo limefanyika eneo la darajani hapa Unguja huku Jumla ya mawakala zaidi ya 50 wamekamatwa kuendelea shughuli zao kinyume cha sheria.  Akizungumzia zoezi hilo kwa ujumla Mkuu wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Esuvatie Masinga a
Kisiwa kilichofanyika miaka 6 iliyopita baada ya tetemeko ardhi chatoweka ghafla

Kisiwa kilichofanyika miaka 6 iliyopita baada ya tetemeko ardhi chatoweka ghafla

Jamii, Kimataifa, Updates
Kisiwa kilichofanyika miaka 6 iliyopita katika pwani ya mji wa Gvadar nchini Pakistani kimepotea. Mwaka 2013 baada ya tetemeko  la ardhi la ukubwa wa 7.7 katika pwani ya mji wa Gvadar unaopatikana kusini mwa Pakistan kilifanyika kisiwa chenye urefu wa mita 40, upana mita 90 na kimo cha mita 20. Kisiwa hicho ambacho kilifanyika kutokana na mlipuko wa volcano kilipewa jina la "Zalzala Koh"  likiwa na maana ya “ kisima cha tetemeko” . Taasisi ya uchunguzi wa Bahari nchini Pakistan (NIO) kwa kushirikiana na shirika la utafiti wa anga la Marekani NASA wamethibitisha kupotea kwa kisiwa hicho kwa kutumia picha za satellite.
TI: Jitihada za Magufuli za kupambana na ufisadi Tanzania zinazaa matunda

TI: Jitihada za Magufuli za kupambana na ufisadi Tanzania zinazaa matunda

Biashara & Uchumi, Jamii, Mikoani, Nyumbani, Updates
Rais John Magufuli Utendakazi na jitihada za kupambana na ufisadi za Rais John Magufuli wa Tanzania zimeifanya nchi hiyo ya Afrika Mashariki ishike nafasi ya kwanza barani Afrika katika vita dhidi ya ufisadi. Ripoti mpya ya utafiti uliofanywa na mashirika ya Transparency International (TI) na Afro- Barometer imesema kuwa, Tanzania imeibuka ya kwanza barani Afrika katika kategoria mbili za kupambana na ufisadi na rushwa. Asilimia 50 ya Watanzania walioshirikishwa kwenye utafiti huo wa Transparency International wanaamini kuwa, licha ya kuweko vizingiti vingi katika vita dhidi ya ufisadi, lakini aghalabu ya wananchi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki wako tayari kuchua hatua za kupambana na ufisadi wa kifedha. Watu 47,000 wameshirikishwa kwenye utafiti huo uli

Jamii yatahadharishwa na Mamlaka ya dawa za kulevya kuhusu vitafunwa vya mtaani

Updates
Jamii imetakiwa kuwa makini na vitafunwa vinavyouzwa mitaani, ikiwamo keki na kashata kwakuwa kumeibuka mtindo mpya wa kuchanganya bangi na dawa nyingine za kulevya. Akizungumza katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba, ofisa kutoka Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya (Adu), Sajenti Chad Ngatunga, alisema kadiri siku zinavyokwenda, watumiaji wa mihadarati wamekuwa wakitumia mbinu mpya ili kutenda uhalifu. Alisema watumiaji wa mihadarati hiyo wanafahamu maeneo wanayouziwa bidhaa hizo zilizochanganywa na dawa. “Wapo wengine wanakwenda duka la madawa wananunua dawa kisha wanahangaika na kimiminika aina ya Energy na kujikuta wakilewa kupitiliza,” alisema Ngatunga. Alisema mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2015 kuhusu
Aliyekuwa awe mwafrika wa kwanza kwenda anga za mbali afariki dunia

Aliyekuwa awe mwafrika wa kwanza kwenda anga za mbali afariki dunia

Jamii, Kimataifa, Teknolojia, Updates
Mwafrika wa kwanza kupata bahati ya kwenda anga za mbali, afariki dunia kwa ajali ya pikipiki kabla ya kutimiza ndoto yake. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na familia yake kwa shirika la habari la BBC, Mandla Maseko, askari wa jeshi la anga la Afrika kusini, mmoja wa watu 23 waliopata nafasi kutoka katika chuo cha anga cha Marekani baada ya kuwashinda watu milioni 1 kutoka mataifa 75. Amefariki katika ajali ya pikipiki iliotokea mwishoni wa wiki.
error: Content is protected !!