Updates

Watafiti kutoka Ureno wagundua Nyota inayofanana sana na Jua

Watafiti kutoka Ureno wagundua Nyota inayofanana sana na Jua

Kimataifa, Teknolojia, Updates
Watafiti wa masuala ya Anga, wamegundua nyota inayofanana na Jua. Wataalamu hao kutoka taasisi ya elimu ya unajimu na fizikia ya nchini Ureno wamegundua nyota "jamii ya Jua". timu ya kimataifa kutoka taasisi hiyo ilikuwa ikifanya utafiti juu ya umri, chemikali zilizomo, na mienendo ya nyota elfu 17 katika galaksi ya Kilimia . Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na watafiti hao kwa kutumia hadubini za rezolusheni za viwango vya juu waligundua nyota inayokadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.5 ambayo wameilezea kama ndugu pacha wa Jua ambayo imepewa jina la HD186302 . Nyota hio inasemekana ipo umbali wa miaka ya nuru (light years)  184 kutoka duniani. Matokeo ya utafiti huo muhimu yamechapishwa  katika jarida la "Astronomy and Astrophysics".
Kongamano la “Rehma kwa Walimwengu” latoa sisitizo kwa Waislamu kuhuisha Uislamu wa Asili

Kongamano la “Rehma kwa Walimwengu” latoa sisitizo kwa Waislamu kuhuisha Uislamu wa Asili

Jamii, Kimataifa, Updates
Taarifa ya mwishoni mwa kongamano la siku mbili lililofanyika mjini Islamabad, Pakistan kwa anuani ya "Rehma kwa Walimwengu" limetoa sisitizo juu ya ulazima wa Waislamu duniani kushikamana na Uislamu wa asili kwa mujibu wa mafundisho ya Bwana Mtume Muhammad SAW. Taarifa hiyo iliyotolewa hapo jana imeeleza kuwa, ili kuweza kufuata njia ya Uislamu wa asili, inapasa Waislamu wajiepushe na mifarakano na badala yake kushikamana na sira ya Ahlul Bayt wa Mtume SAW. Taarifa hiyo aidha imesisitiza kuwa Bwana Mtume Muhammad SAW alikuwa Mtume adhimu aliyekuwa akitilia mkazo sana kuheshimu dini za watu wengine na kuwataka Waislamu wajiepushe na ubaguzi wa aina yoyote ile, lakini kuna watu majahili wanaotumia kila njia ili kuharibu sura ya dini tukufu ya Uislamu. Kongamano la Rehma kwa Walimwe...
Pongezi kwa munasaba wa Maulid ya Mtume Mtukufu SAW wa Uislamu na kuanza Wiki ya Umoja

Pongezi kwa munasaba wa Maulid ya Mtume Mtukufu SAW wa Uislamu na kuanza Wiki ya Umoja

Jamii, Kimataifa, Updates
Leo Jumanne, 12 Rabiul Awwal mwaka 1440 Hijria Qamaria, sawa na Novemba 20 2018, kwa mujibu wa baadhi ya riwaya ni siku ya kukumbuka na kuadhimisha kuzaliwa (Maulid) Bwana Mtume Muhammad al Mustafa SAW, Mtume Mtukufu wa Uislamu. Siku hii pia ni mwanzo wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Kwa mujibu wa riwaya za Ahul Sunna wal Jamaa, Mtume Muhammad SAW alizaliwa tarehe 12 Rabiul Awwal na kwa mujibu wa riwaya za Shia tarehe 17 Rabiul Awwal mwaka huohuo ndiyo siku aliyozaliwa Mtukufu huyo. Kwa msingi huo, Imam Khomeini, MA, Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambaye alikuwa miongoni mwa wanazuoni wenye kunadi umoja wa ulimwengu wa Kiislamu, alitangaza kipindi cha wiki moja cha baina ya siku hizo mbili, yaani kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Wa
Mvutano wa kimamlaka waibuka Gabon

Mvutano wa kimamlaka waibuka Gabon

Updates
Rais wa Gabon Ali Bongo amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki tatu. Na sasa nguvu za makamu wake zimeongezwa kuhakikisha kile serikali ya Gabon imekiita kuendeleza shughuli za dola uamuzi ambao upinzani umeupinga. Rais wa Gabon amekuwa akitibiwa katika hospitali ya King Faisal mjini Riyadh nchini Saudi Arabia tangu Oktoba 24. Kuna uvumi kuwa alipatwa na kiharusi lakini hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa kuthibitisha. Hadi sasa hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa ya Rais Bongo kurejea nchini Gabon msemaji wake Ike Ngouoni alikairiwa na duru za habari akisema Rais Bongo amekuwa akisumbuliwa na kizunguzungu kikali lakini sasa afya yake inaimarika. Siku ya jumatano mahakama ya katiba nchini Gabon chini ya Rais wake Marie-Madeleine Mborantsuo ilitangaza marekebisho madogo ya katiba
Learn & Donate Internship Program

Learn & Donate Internship Program

Ajira, Teknolojia, Updates
Shaibu Foundation is the non-profit firm based in Tanzania with main object of providing the highest quality of religious, educational, and social services to the community in accordance with the teachings of the Holy Quran and traditions of Prophet Muhammad (peace be upon him). Through our project known as "LEARN & DONATE" We are proud to announce "Learn & Donate Internship Program" Learn & Donate Internship Program is designed to provide exceptional students interested in a career in ICT, Business and Media with a unique opportunity to learn firsthand about the diverse business operations. Those selected will gain invaluable work experience through challenging project assignments, information sessions hosted by Shaibu Foundation senior management, and various additi
error: Content is protected !!