Teknolojia

Rouhani: Taifa la Iran halitanyenyekea madola ya kibeberu

Rouhani: Taifa la Iran halitanyenyekea madola ya kibeberu

Jamii, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ustawi na maendeleo ya taifa la Iran ni matokeo ya muungano wa kaumu zote na jamii za waliowachache nchini na kuongeza kuwa: "Taifa la Iran halitayanyenyekea madola ya kibeberu." Rais Hassan Rouhani aliyasema hayo Jumanne wakati wa kuzindua miradi ya maji katika mkoa wa Azerbaijan Magharibi katika eneo la magharibi mwa Iran na kuongeza kuwa: "Nguvu za taifa la Iran ni kubwa kiasi kwamba punde baada ya maadui kulitisha taifa hili wamelazimika kutangaza kuwa hawataki vita." Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: "Taifa la Iran ambalo limeungana na lina imani thabiti daima limekuwa likisimama kidete mbele ya maadui na nukta hii inashuhudiwa siku zote miongoni mwa wananchi." Rais Rouhani ameendele...
UN: Kuna uwezekano mkubwa wakati huu wa kutumika silaha za nyuklia

UN: Kuna uwezekano mkubwa wakati huu wa kutumika silaha za nyuklia

Jamii, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Mkurugenzi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Utafiti wa Upokonyaji Silaha UNIDIR amesema hatari na uwezekano wa kutumika silaha za nyuklia duniani hii leo uko juu kuliko wakati mwingine wowote ule. Renata Dwan amesema hayo katika mahojiano na shirika la habari la Reuters na kubainisha kuwa, "Nadhani ni sahihi kufahamika kuwa dunia hii leo iko katika hatari kubwa ya kushuhudia vita vya nyuklia; na uwezekano wa kutumika silaha za maangamizi za nyuklia uko juu zaidi wakati huu kuliko wakati wowote ule, tokeo Vita Vikuu vya Pili vya Dunia." Dwan ambaye anaongoza taasisi hiyo iliyoundwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1980 kwa ajili ya kutathmini hatari inayoikabili dunia kutokana na mashindano ya kijeshi amesema kadhia kuhusu uwezekano wa kutokea vita vya nyu...
Kenyatta azindua mpango wa uchumi wa kidigitali wa Kenya

Kenyatta azindua mpango wa uchumi wa kidigitali wa Kenya

Biashara & Uchumi, Jamii, Teknolojia
Rais Uhuru Kenyatta Rais Uhuru Kenyatta amezindua pendekezo la mpango wa uchumi wa kidigitali wa Kenya, Jumanne wakati mkutano wa pili wa kuibadilisha Afrika unaofanyika Kigali, Rwanda ukiendelea. Nguzo tano za angalizo la mpango huu wa kidigitali ni : Kubadilisha huduma zinazotolewa na serikali zifanyike kidigitali au kwa kutumia teknolojia , pia kuzijengea uwezo biashara, wajasiri amali, wabunifu na tabaka za ujuzi mbalimbali kupitia teknolojia. Gazeti la The East African limeripoti Jumamosi kuwa Rais Kenyatta, ameeleza mpango huu utasaidia kuwa ni muongozo muhimu kwa kuchochea mabadiliko ya kiuchumi Kenya kwa kutumia teknolojia. “Kusudio ni kutengeneza muundo ili utuongoze wakati tukiendeleza juhudi za kutumia teknolojia hizi kwa mujibu wa mazingira yetu. Natumai
Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kwa ajili ya kuilinda mifumo ya kompyuta dhidi ya ” wapinzani wa kigeni”

Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kwa ajili ya kuilinda mifumo ya kompyuta dhidi ya ” wapinzani wa kigeni”

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kwa ajili ya kuilinda mifumo ya kompyuta dhidi ya '' wapinzani wa kigeni'' Rais huyo wa Marekani amesaini sheria ya utaratibu wa utendaji ambayo inazuwia mara moja makampuni ya Marekani kutumia mawasiliano ya kigeni yanayoaminiwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo. Bwana Trump hataji kampuni yoyote katika agizo hilo. Muasisi wa Huawei Ren Zhengfei aliwahi kusema kuwa Marekani haiwezi kumaliza biashara zake Hata hivyo, wachambuzi wanasema uamuzi huo unailenga kampuni kubwa ya mawasiliano ya Kichina Huawei. Nchi kadhaa- Marekani ikiwemo-zimekwisha elezea wasi wasi wake kwamba huduma za kampuni hiyo zinaweza kutumiwa na Uchina kwa upelelezi. Huawei imesema kuwa kazi yake haisababishi tisho lolote. K...
Air Bus wafanya maonyesho uwanja wa ndege wa Zanzibar

Air Bus wafanya maonyesho uwanja wa ndege wa Zanzibar

Biashara & Uchumi, Nyumbani, Teknolojia
KAMPUNI ya Air Bus iliyotengeneza ndege ya Air Tanzania imefanya maonyesho katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, kupitia ndege ya Air Tanzania na kuhudhuriwa na kampuni mbalimbali za ndege. Akizungumza baada ya kufanyika maonyesho hayo, Meneja wa uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar, Bukheti Juma Suleiman, alisema, maonyesho hayo yana lengo la kuonyesha uwezo wa ndege zao wanazozitengeneza. Alisema ni jambo la faraja kuona kampuni hiyo kuchagua uwanja huo kufanya maonyesho yao kwani inadhihirisha kuwa uwanja huu ni bora na inaweza kuwa fursa ya kukuza utalii. Naye Rubani kiongozi wa ndege ya Air Tanzania, Kassim Suhad, alisema, ndege hiyo ina uwezo mzuri wa kuchukua abiria na tokea kuanza safari zake haijawahi k...
error: Content is protected !!