Teknolojia

Hospitali ya Kivunge kutoa dawa kwa njia ya kielektroniki

Hospitali ya Kivunge kutoa dawa kwa njia ya kielektroniki

Afya, Nyumbani, Teknolojia
Hospitali ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja inatarajiwa kuanza kutumia mfumo mpya wa utoaji wa Dawa kwa njia ya Kielektroniki ili kuboresha utoaji wa huduma Hospitalini hapo. Hatua hiyo inakuja kufuatia Wizara ya Afya Zanzibar kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Komputa zitakazorahisisha mfumo huo. Akikabidhi vifaa hivyo huko Kivunge Mfamasia Mkuu wa Zanzibar, Habib Ali Sharif amesema mfumo huo Kielektroniki utasaidia kudhibiti Dawa na kujua upungufu uliopo katika Hospitali hiyo. Aidha amefahamisha kuwa Mfumo huo pia utarahisisha kutathimini jinsi ya dawa zinavyotumika katika Vituo mbali mbali. Mfamasia huyo alibainisha kuwa zoezi la Mfumo wa Kielektroniki mbali na kutumika katika Hospitali ya Kivunge linatarajiwa pia kufanyika katika hospitali ya kendwa. Alieleza ...
Nchini China yatengenezwa jenereta linaloweza kuvaliwa na kufuliwa

Nchini China yatengenezwa jenereta linaloweza kuvaliwa na kufuliwa

Biashara & Uchumi, Teknolojia
Wanasayansi nchini China wametengeneza kifaa ambacho kinaweza kuchaji simu na vitu vingine (nanogenerator), ambacho kitaweza kuvaliwa na kufuliwa. Kwa mujibu ya habari kutoka shirika la habari la Chına Xinhua, Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Cıngcou eneo la Henan mji wa Cıngcou wametengeneza kıfaa ambacho kitatumika kuchaji simu na vifaa vingine vinavyoendana, kifaa  kina uwezo wa kubadilisha nishati inayopatikana kwenye mwili wa binadamu akiwa kwenye mwendo kuwa nishati ya umeme ( nanogenerator). Tatızo la sımu ambazo selı zake huisha nguvu mara kwa mara sasa limepata suluhisho imefahamisha habari hio. Kifaa hichi ambacho hakiingii maji kinaweza kuvaliwa na kufuliwa bila kumuuzi mtumiaji. Utafiti huu ulichapishwa kwenye jarida la Kemia A.  
Mtanzania alietengeneza kipimo cha magonjwa ya moyo

Mtanzania alietengeneza kipimo cha magonjwa ya moyo

Afya, Jamii, Mikoani, Teknolojia
Mwanafunzi wa kitanzania Janeth Tillya kutoka Chuo cha St Joseph cha DSM ameweza kutengeneza kifaa ambacho mtu anaweza kujipima matatizo ya moyo kisha kumtumia Daktari wake matokeo yake hata bila ya kwenda Hospitali kwa wakati ambao anajisikia vibaya. Janeth Tillya amesema tatizo la foleni mahospitalini hukera zaidi watu hasa pale Mtu anapokuwa mgonjwa na kukuta watu wengi kwenye foleni ya kuingia kwa Daktari na muda wa kupima na wakati mwingine unaweza kuta hata vipimo kwa muda huo havifanyi kazi labda kwa tatizo la kutokuwepo kwa umeme (kukatika) au hata mpimaji kutokuwepo maabara au kuwa na kazi nyingi. Kifaa hicho ambacho kinatumia betri ndogo ya kawaida ambayo inapatikana katika maduka ya kawaida majumbani pia kifaa hicho kinatumia Bluetooth kutuma taarifa katika simu wa
Kutekwa kwa Mo Dewji, Serikali yatangaza kufunga CCTV Camera katika Majiji yote Nchini

Kutekwa kwa Mo Dewji, Serikali yatangaza kufunga CCTV Camera katika Majiji yote Nchini

Jamii, Mikoani, Teknolojia
Kufuatia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Serikali inatarajia kusambaza kamera maalum za CCTV katika miji mikubwa na mikoa iliyoko karibu na mipaka ya nchi kwa lengo la kuimarisha ulinzi, na kukomesha matukio ya kihalifu ikiwemo matukio ya utekaji. “Tunampango wakufunga CCTV Camera hasa katika miji mikuu ili kupunguza matukio mbalimbali ikiwemo suala la utekaji, hata ukiangusha sindano lazima ionekane, na ninawaonya wanasiasa uchwara wasitumie tukio hili kujipatia umaarufu”, amesema Masauni. Masauni ameongeza kuwa , “Matukio ya utekaji ni sifa mbaya sana ila sitaki kulielezea sana maana jana (juzi) Waziri wa Mambo ya Ndani amezungumza mengi ikiwemo mafanikio ya jeshi la polisi, ila hili la mfanyabiashara Mohamed Dewji
Wazazi walalamikia tatizo kubwa la simu za mkononi

Wazazi walalamikia tatizo kubwa la simu za mkononi

Afya, Jamii, Teknolojia
Hivi karibuni imekuwa kawaida sana kumkuta mtoto anatumia simu ya mkononi ya mzazi wake na mara nyingine wanatumia bila hata kupata ridhaa ya mzazi mwenyewe. Baadhi ya watoto huonyesha utaalamu wa hali ya juu katika kufungua kurasa mbalimbali za simu hizo. Na inadaiwa kuwa kuna watoto ambao huwa wanajifunza mambo mengi kupitia simu za mkononi. Hata hivyo si wazazi wote ambao hukubali simu zao zitumiwe na watoto, baadhi huwa wakali na kuweka kila aina ya nywila ingawa wengine huwa hawaoni shida kuwapatia watoto wao simu punde tu wanaporejea kutoka kwenye majukumu yao ya kila siku. Baadhi ya wazazi huwa wanaona kuwa simu ndio njia pekee inayoweza kuwafanya watoto wao watulie na wao wapate muda wa kupumzika ama hata kufanya shughuli zao za nyumbani. Je,kuna faida yeyote endapo ...
error: Content is protected !!