Teknolojia

China imeitaka Marekani kuchukua hatua kurekebisha makosa

China imeitaka Marekani kuchukua hatua kurekebisha makosa

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Matamshi hayo yanafuatia kukamatwa kwa Meng Wanzhou ofisa mtendaji mkuu wa masuala ya fedha katika kampuni ya Huawei Technologies ya China China imemuita balozi wa Marekani mjini Beijing siku ya Jumapili kuwasilisha ‘upinzani mkali’ juu ya kukamatwa kwa ofisa wa juu wa teknolojia wa China nchini Canada na Washington kutaka apelekwe Marekani ili kujibu mashtaka ya tuhuma za ubadhirifu. Nembo ya Huawei Technologies China ilisema kukamatwa kwa Meng Wanzhou, ofisa mtendaji mkuu wa masuala ya fedha katika kampuni ya Huawei Technologies ni “jambo baya sana” na kuitaka Marekani ifute ombi lake la kutaka apelekwe nchini Marekani kwa kuhusishwa na shutuma kwamba alivunja sheria za Marekani ambazo zinapiga marufuku biashara na Iran. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China, L
Wahasiriwa wanatishiwa kuwa akaunti zao zimedukuliwa.

Wahasiriwa wanatishiwa kuwa akaunti zao zimedukuliwa.

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Teknolojia
Maelfu ya watu kote duniani wamekuwa wakipokea ujumbe kutoka kwa watu walaghai mitandaoni. Ujumbe huo ni tofauti na ujumbe mwingine kwasababu wahasiriwa wanatishiwa kwamba akaunti zao zimedukuliwa. Kitengo cha BBC Trending kimebaini jinsi watu wanavyo hadaiwa na walaghai wanaodai kuwa na ushahidi wa kuthibitisha wamekuwa wakitembelea mitandao yenye utata ambayo huonesha picha za utupu. CHANZO: BBC
Ongezeko la wateja laipelekea PBZ kuzindua mfumo mpya wa huduma Zanzibar

Ongezeko la wateja laipelekea PBZ kuzindua mfumo mpya wa huduma Zanzibar

Biashara & Uchumi, Nyumbani, Teknolojia
Benki ya watu wa Zanzibar PBZ imekusudia kuanzisha mfumo mpya wa kibenki unaotambulika kwa jina la BENKS utaotarajiwa kuanza rasmi tarehe 3 mwezi huu  ili kuondoa changamoto ya kukatika mara kwa mara kwa huduma zake pamoja na kuondoa uzito wa utoaji wa fedha kwenye mfumo. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Juma Ameir Hafidhi amesema PBZ imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kusambaza matawi yake katika maeneo mbalimbali na itaendelea kusambaza huduma ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wanaohitaji huduma za kibenki. Juma amesema kukamilika kwa mfumo huo kunauwezekano mkubwa wa kuondoa usumbufu kwa wateja  wanaotumia  huduma za kibenki kupitia PBZ  na kuwarahisishia huduma kwa urahisi  ukilinganisha na mfumo wa zamani ambao ulikuwa
Chombo ‘Insight’ cha Marekani chatua salama Mars

Chombo ‘Insight’ cha Marekani chatua salama Mars

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Teknolojia
Safari ya anga za juu ya chombo cha kipekee, kilichopewa jina Insight ilikamilika Jumatatu, pale chombo hicho kisicho na rubani na kinachotumia teknolojia ya kisasa kabisa, kilipotua kwenye sayari ya Mars.  Safari hiyo imekuwa ikiangaziwa kwa karibu mno tangu chombo hicho kuondoka ardhini. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa wahandisi na wafanyakazi wa Shirika la Marekani la kuratibu safari za anga za juu, NASA, pale ilipotangazwa kwamba Insight ilitua salama salimini kwenye Mars, maarufu kama sayari nyekundu. Baada ya kusafiri kwa maili milioni mia tatu na kwa muda wa takriban miezi saba, hatimaye chombo hicho kilipunguza mwendo wake na kutua taratibu, huku wafanyakazi na wahandisi wa NASA wakifuatikia kwa karibu kutoka maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kituo cha kimatai
Korea Kaskazini yajiandaa kufanya majaribio ya silaha ya kistratijia

Korea Kaskazini yajiandaa kufanya majaribio ya silaha ya kistratijia

Kimataifa, Teknolojia
Duru za habari zimeripoti kwamba serikali ya Korea Kaskazini inajiandaa kufanya majaribio ya silaha mpya ya kistratijia. Chombo kimoja cha habari nchini humo kilitangaza jana kwamba Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini ametembelea eneo la kufanyia majaribio ya silaha mpya za nchi yake. Hata hivyo televisheni ya serikali ya Korea Kaskazini haikufafanua zaidi kuhusiana na uundaji wa silaha hiyo mpya ya kistratijia. Hii ni katika hali ambayo kabla ya hapo Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ilionya kwamba iwapo Marekani haitofuta vikwazo ilivyoiwekea serikali ya Pyongyang, basi itaimarisha vinu vyake vya nyuklia. Itakumbukuwa kuwa Kim Jong-un wa Korea Kaskazini na Rais Donald Trump wa Marekani walikutana tarehe 12 Juni mwaka huu nchini Singapore ambapo walisisitiza udharura wa kuimaris...
error: Content is protected !!