Siasa

Burundi yasitisha kwa muda NGOs kutoa huduma

Burundi yasitisha kwa muda NGOs kutoa huduma

Kimataifa, Siasa
Serikali ya Burundi imesitisha kwa muda baadhi ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali ya ndani ya nchi na yale ya kimataifa, kwa madai ya kuwa hayaheshimu sheria za nchi. Tamko la serikali Katika taarifa aliyo itowa Alhamisi Katibu Mkuu wa Baraza la Usalama la kitaifa, Jenerali Silas Ntingurigwa, mashirika hayo yamesitishwa kutoa huduma kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia tarehe mosi Oktoba. Lakini hakutoa idadi au utambulisho wa mashirika yanayo kabiliwa na hatua hiyo. Nchini Burundi, kuna mashirika yasio kuwa ya kiserikali yapatao 130. Sababu yakusimamishwa mashirika hayo Katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa, msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza amesema hatua ya kuyasimamisha baadhi ya mashirika yasio kuwa ya kiserikali ya kimataifa imechukuliwa kwa s...
Uteuzi wa Kavanaugh : Kura kamili baada ya upelelezi wa FBI

Uteuzi wa Kavanaugh : Kura kamili baada ya upelelezi wa FBI

Kimataifa, Siasa
Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti imepiga kura kwa kuzingatia msimamo wa vyama Ijumaa ili kupeleka mbele uteuzi wa mteule wa Mahakama ya Juu Brett Kavanaugh kwenda kwenye Baraza kamili la Seneti, ingawaje inaomba wiki moja kulipa nafasi shirika la Upelelezi wa Makosa ya Jinai (FBI) kufanya uchunguzi. Hili linajiri siku moja baada ya mahojiano yaliyo mhusisha jaji wa mahakama ya rufani na Christine Blasey Ford anaye mtuhumu jaji huyo kwa kumdhalilisha kingono. Nafasi ya Kavanaugh kuthibitishwa iliongezeka wakati Seneta Jeff Flake wa Republikan, mwenye kura peke iliyo kuwa inaweza kubadilisha uamuzi wa kamati hiyo, aliposema Ijumaa kuwa atapiga kura kumpitisha Kavanaugh, baada ya siku moja kabla kusema alikuwa hajafikia uamuzi. Haiko wazi iwapo Warepublikan watapa...
Wazambia waandamana kupinga ubadhirifu wa mali ya umma

Wazambia waandamana kupinga ubadhirifu wa mali ya umma

Kimataifa, Siasa
Wananchi wa Zambia wamefanya maandamano makubwa mbele ya Bunge la nchi hiyo mjini Lusaka wakipinga ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Waandamanaji hao waliokuwa na vitambaa vyenye maandishi yanayolaani wizi na ubadhirifu mkubwa unaofanyika ndani ya serikali ya nchi hiyo wametaka kutisishwa ufisadi haraka iwezekanavyo. Baadhi ya maandishi hayo yamehoji ni kwa nini Wazambia wanaishi katika umaskini ilhali nchi yao ina utajiri wa maliasili? Waandamanaji hao walikuwa wakipiga nara zinazosema: "Msikumbatie ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, komesheni wizi wa fedha za wananchi". Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia alijiuzulu wadhifa wake kulalamikia kashfa za ufisadi zinazoizunguka serikali ya Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo. Harry Kalaba a
Baraza Kuu la UN; uwanja wa kukejeliwa Trump, jukwaa la mazingaombwe ya Netanyahu

Baraza Kuu la UN; uwanja wa kukejeliwa Trump, jukwaa la mazingaombwe ya Netanyahu

Siasa
Kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimefanyika, huku walimwengu wakijionea igizo jengine la usanii wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel; utawala ambao una mamia ya vichwa vya nyuklia, silaha ambazo ni tishio na hatari kwa usalama wa dunia. Hata hivyo kutokana na kuungwa mkono na Marekani, utawala huo khabithi hauwajibiki kwa taasisi yoyote ile duniani. Jana Alkhamisi, tarehe 27 Septemba, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu, aliutumia muda wa hotuba yake katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuujadili tena mpango wa nyuklia wa Iran; na kwa mara nyingine akawaonyesha hadhirina picha alizodai kuwa ni ushahidi unaothibitisha kwamba Iran ingali inaendesha kwa siri shughuli zake za nyuklia katika eneo moja la kusini mw
Boris Johnson awasilisha mpango wa Brexit

Boris Johnson awasilisha mpango wa Brexit

Kimataifa, Siasa
LONDON, UINGEREZA WAZIRI wa zamani wa mambo ya nje wa Uingereza, Boris Johnson amewasilisha mpango mbadala wa nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit na amemtaka Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May kuachana na mapendekezo yake ya Brexit. Johnson aliandika katika gazeti la Telegraph toleo la jana kwamba,  huu ni wakati wa kubadilisha mfumo wa mazungumzo na kuleta haki kwa ajili ya matarajio mazuri ya Brexit. Mpango huo ambao ameutoa siku mbili kabla ya kufanyika mkutano wa chama cha Conservative, utaongeza shinikizo kwa May ambaye anapambana kukiunganisha na kukishawishi chama chake kikubaliane na mpango wake, wakati siku ya mwisho ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya ikiwa inakaribia. May amerudia kusema kwamba mapendekezo yake kuhusu Brexit
error: Content is protected !!