Siasa

Serikali ya Tanzania: Hatutoruhusu wachunguzi kutoka nje kuja kuchunguza tukio la kutekwa nyara Mo Dewji

Serikali ya Tanzania: Hatutoruhusu wachunguzi kutoka nje kuja kuchunguza tukio la kutekwa nyara Mo Dewji

Biashara & Uchumi, Mikoani, Siasa
Naibu Waziri wa Mambo  ya Ndani nchini Tanzania,  Hamad Masauni amesema kuwa, serikali haiwezi kuruhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje ya nchi kuja kuchunguza tukio la kutekwa nyara mfanyabiashara mkubwa wa nchi hiyo na Afrika Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’. Masauni aliyasema hayo Jumanne ya jana katika mkutano na waandishi wa habari na kuongeza kuwa,  anayo imani kwamba ndani ya jeshi la polisi kuna wataalamu wanaoijua kazi yao, na wanaoifanya kwa kuzingatia maadili. “Kuna haja gani ya kuleta vyombo vya nje wakati tuna jeshi bora na lenye uelewa mkubwa licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale?” Alihoji Naibu Waziri Masauni. Kadhalika Naibu Waziri wa Mambo  ya Ndani nchini Tanzania Amesema  kuwa, polisi ya nchi hiyo hawajashindwa kuchunguza jambo hilo na lipo ndani ya uwezo
Godbless Lema ataka polisi wotoe picha za CCTV kutekwa kwa Mo

Godbless Lema ataka polisi wotoe picha za CCTV kutekwa kwa Mo

Mikoani, Siasa
Mwanasiasa machachari wa upinzani Tanzania na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Godbless Lema amelitaka jeshi la polisi kutoa picha za CCTV kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambazo zinaonyesha tukio la kutekwa kwa bilionea Mohamed Dewji. Mwanasiasa huyo amesema kama serikali ipo tayari kupokea msaada kutoka kwa wananchi ili kufahamu mahali alipo Mo Dewji basi iachie picha hizo ili wananchi waweze kuwatambua watekaji na magari yaliyotumika. "Baada ya kugundua kuwa waliomteka Mo ni wazungu wawili na wameonekana kwenye mkanda wa CCTV, na si polisi wanataka wananchi watoe ushirikiano? Chamuhimu una zitoa picha za video, hao wazungu tuwaone. Swali kwanini wanaficha hizo picha za CCTV? Kwanini hata kwa (Tundu) Lissu kamera ilichukuliwa?," amehoji Lema. Lema pia ameitaka serikal...
Seneta wa Marekani: Muhammad bin Salman lazima auzuliwe

Seneta wa Marekani: Muhammad bin Salman lazima auzuliwe

Kimataifa, Siasa
Seneta Lindsey Graham wa chama tawala cha Republican nchini Marekani ametoa maneno makali akisema Muhammad bin Salman ndiye mhusika wa mauaji ya Jamal Khashoggi na kutaka auzuliwe wadhifa wake wa urithi wa ufalme wa Saudi Arabia. Akizungumza katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Fox News, Graham ameashiria mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari mkosoaji wa utawala wa Saudia kwenye ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki na kusisitiza kuwa, hakuna tukio lolote linalojiri nchini Saudi Arabia bila Muhammad bin Salman kuwa na taarifa nalo. Seneta huyo wa chama cha Republican amemkosoa mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia na kusema: "Mimi sitakuwa na maelewano yoyote na Saudi Arabia maadamu Muhammad bin Salman ni mrithi wa ufalme". Seneta Lindsey Graham si
Trump asema huenda wahuni walio muua mwandishi wa Saudia

Trump asema huenda wahuni walio muua mwandishi wa Saudia

Kimataifa, Siasa
Rais wa Marekani Donald Trump anaamini mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi aliye toweka yapata wiki mbili zilizopita, huenda wahuni walio muua. Khashoggi alitoweka tangu Oktoba 02 baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki. Trump amesema Jumatatu amefanya mazungumzo ya simu kwa dakika 20 na Prince wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ambaye amemwambia kwamba haana taarifa yoyote kuhusu kilichomtokea Khashoggi. Rais alimtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje Mike Pompeo mjini Riyadh kufanya mazungumzo na mfalme Salman kuhusu kutoweka kwa Khashoggi. Khashoggi aliingia katika ubalozi mdogo Octoba 2 ili kuchukuwa makaratasi yake aliyokuwa anayahitaji ili kumwezesha kufunga ndoa na mchumba wake, Hatice Cengiz, raia wa Uturuki ambaye alisu...
Familia ya Mo Dewji imetangaza dau la BILIONI 1

Familia ya Mo Dewji imetangaza dau la BILIONI 1

Biashara & Uchumi, Jamii, Mikoani, Siasa
Familia ya Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’, aliyetekwa siku ya Alhamisi na watu wasiojulikana, imezungumza na wandishi wa habari leo mchana katika ofisi za kampuni ya MeTL Group zilizopo katika jengo la Golden Jubilee Towers ghorofa ya 20 mtaa wa Ohio, Posta jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo, familia hiyo imetangaza zawadi ya Tsh. Bilioni Moja (1,000,000,000) kwa mtu yeyote ambaye atatoa taarifa ambazo zitawezesha kupatikana kwa Mohammed Dewji. Mwenye taarifa anaweza kuwasiliana na mwanafamilia Murtaza Dewji kwa namba 0755 030014, 0717 208478 na 0784 783228.
error: Content is protected !!