Siasa

Cameroon imefanya uchaguzi wa urais

Cameroon imefanya uchaguzi wa urais

Kimataifa, Siasa
Taifa la Cameroon lilishuhudia matukio kadhaa ya ghasia Jumapili wakati upigaji kura ulipoanza katika uchaguzi uliotarajiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza muda wa utawala wa Rais Paul Biya, mmoja wa viongozi wa Afrika aliye madarakani kwa muda mrefu. Shirika la habari la Reuters lilieleza kwamba zoezi la upigaji kura lilifanyika salama kwa sehemu kubwa ya taifa hilo la Afrika ya kati lililopo katika mgawanyiko wa lugha na kupelekea baadhi ya vituo vya kupiga kura kutofunguliwa katika maeneo ya Anglophone na kuzusha ghasia. Watu takribani watatu waliokuwa na silaha kwenye eneo linalojitenga walifyatuliwa risasi na kuuwawa na vikosi vya usalama huko kaskazini mashariki katika mji wa Bamenda unaozungumza lugha ya ki-Ingereza, chanzo kimoja cha usalama kilisema.
Trump na Kim watakutana tena haraka iwezekanavyo

Trump na Kim watakutana tena haraka iwezekanavyo

Kimataifa, Siasa
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong UN wamekubaliana kupanga mkutano wa awamu ya pili kati ya Marekani na Korea kaskazini haraka iwezekanavyo, ofisi ya Rais wa Korea kusini ilisema Jumapili. Tangazo hilo lilikuja muda mfupi baada ya Pompeo alipowasili Seoul kufuatia ziara yake ya siku nne kuelekea Korea kaskazini mahala ambapo alikutana na Kim. Pompeo alisema Marekani na Korea kaskazini walikubaliana kuendeleza mazungumzo na kuchagua tarehe maalumu pamoja na mahala ambako mkutano ujao utafanyika kulingana na taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Korea kusini, Moon Jae-In. Moon alimshukuru Pompeo kwa ziara yake na aliwatakia mafanikio mema kwenye mkutano ujao kati ya Kim na Rais Donald Trump wa Marekani. Viongozi hao wawili walikutana...
Ufaransa: Marekani haina haki ya kuchukua maamuzi kwa niaba ya Ulaya

Ufaransa: Marekani haina haki ya kuchukua maamuzi kwa niaba ya Ulaya

Kimataifa, Siasa
  Waziri wa Fedha wa Ufaransa amesema kuwa, Marekani haiwezi kuchukua maamuzi kuhusiana na ushirikiano wa kibiashara wa nchi za Ulaya na Iran na kuongeza kuwa, vikwazo vya serikali ya Washington dhidi ya Iran ni fursa kwa Ulaya kwa ajili ya kuanzisha taasisi zinazojitegemea za kifedha. Bruno Le Maire ameuambia mkutano unaofanyika huko Slovakia kwamba Umoja wa Ulaya umesasisha sheria ya kukabiliana na vikwazo vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran ili kuyawezesha makampuni ya nchi za bara hilo kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kibiashara. Wakati huo huo imepangwa kwamba katika wiki kadhaa zijazo Umoja wa Ulaya utaanza kutekeleza taratibu mpya zitakazodumisha miamala ya kifedha na Iran mkabala wa vikwazo vipya vya kifedha vya Marekani. Sera za kijuba na ...
Mwanamfalme wa Saudi Arabia amshambulia Donald Trump

Mwanamfalme wa Saudi Arabia amshambulia Donald Trump

Kimataifa, Siasa
Prince Salman ameishambulia Marekani kwa kusema kuwa taifa la Saudi Arabia limekuwepo kwa miaka mingi kabla hata taifa la Marekani halijatengenezwa hivyo Washington isiibabaishe Saudi Arabia yenye utajiri mkubwa wa mafuta. Mwanamfalme wa Saudi Arabia Salman amesema kuwa nchi yake haitokaa kuilipa Washington kwa ajili ya usalama wake. "Saudi Arabia imekuwepo kabla ya Marekani.Taifa la Saudi Arabia limekuwepo toka mwaka 1744 nikiamini ni miaka 30 kabla ya taifa la Marekani halijatengenezwa",alisema Salman. Wiki iliyopita rais Donald Trump alisema kuwa mfalme wa Saudi Arabia hawezi kusalia madarakani kwa zaidi ya wiki mbili bila msaada wa jeshi la Marekani. Salman nae ametoa jibu kwa tamko hilo na kusema kuwa mtu anapaswa kukubali kuwa kuna wakati rafiki anaweza kuzungumza vit...
Mpinzani wa Kagame, mama yake waachiwa huru Rwanda

Mpinzani wa Kagame, mama yake waachiwa huru Rwanda

Kimataifa, Siasa
Mahakama nchini Rwanda Ijumaa imeamuru kuachiwa huru mpinzani wa Rais Paul Kagame ambaye alizuiliwa kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi dhidi yake katika uchaguzi wa urais mwaka 2017. Jaji wa Mahakama Kuu amesema katika uamuzi wake kuwa Diane Rwigara na mama yake, ambao walikamatwa pamoja mwaka 2017, wataachiwa huru mara moja lakini kwa sharti ya kuwa hawaruhusiwi kuondoka mjini Kigali “bila ya kibali.” Wakati jaji akisoma hukumu hiyo katika chumba cha mahakama ambacho kilikuwa kimejaa wanadiplomasia, waandishi wa habari na ndugu wa wanawake hao waliokuwa wamevaa nguo za kifungoni rangi ya pinki, chumba cha mahakama ghafla kilijawa na furaha na watu kadhaa walipiga kelele “Mungu Asifiwe!”. Rwigara na mama yake walihukumiwa kifungo Octoba 2017 kwa mashtaka ya
error: Content is protected !!