Siasa

Saudia yapinga takwa la Uturuki la kufanya uchunguzi wa mauaji ya Khashoggi kuwa wa kimataifa

Saudia yapinga takwa la Uturuki la kufanya uchunguzi wa mauaji ya Khashoggi kuwa wa kimataifa

Kimataifa, Siasa
Kufuatia mashinikizo ya kieneo na kimataifa ya kutaka kufuatiliwa kimataifa faili la mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud, serikali ya Riyadh imekataa kuufanya wa kimataifa uchunguzi wa faili hilo. Jumatano ya jana Rais Recep Tayyip Erdoğan alitangaza kwamba Ankara itaendelea kufuatilia faili la mauaji ya mwandishi huyo na kwamba iwapo itahitajika basi faili hilo litawasilishwa katika mahkama ya kimataifa. Kufuatia hali hiyo, Bandar bin Mohammed Al-Aiban, Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Saudia na katika kujaribu kuzuia kuendelea kufichuliwa zaidi kashfa za viongozi wa nchi hiyo, amekataa pendekezo hilo la kuufanya uchunguzi huo kuwa wa kimataifa. Kabla ya hapo pia kanali ya televisheni ya Al Jazeera ilifichua kwamba
Ufaransa yaimarisha uhusiano wa kijeshi, uchumi na Afrika

Ufaransa yaimarisha uhusiano wa kijeshi, uchumi na Afrika

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Rais Kenyatta akimpokea mgeni wake Rais Macron Rais Emmauel Macron wa Ufaransa amewasili jijini Nairobi, Kenya, hii leo akiwa katika ziara ya siku nne ya nchi za Pembe na Mashariki ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuimrisha uhusiano wa kiuchumi na kijeshi. Kiongozi huyo anakutana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta leo na wanatarajiwa kuzungumza juu ya jukumu la Kenya katika kuleta utulivu nchini Somalia, vita vyake dhidi ya ugaidi na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kiutamaduni na kijeshi na Kenya. Macron apokelewa kwa heshima kubwa Rais Macron alipokelewa kwa heshima zote na Rais Uhuru Kenyatta alipowasili kwa ziara yake ya kwanza rasmi. Ziara hiyo ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Ufaransa tangu Kenya kujinyakulia uhuru wake 1963. Akiwa huko Nairobi kio...
India na Pakistan zaendelea kutunishiana misuli, zafanyia majaribio makombora yao mapya

India na Pakistan zaendelea kutunishiana misuli, zafanyia majaribio makombora yao mapya

Kimataifa, Siasa
India na Pakistan zimeyafanyia majaribio kwa mafanikio makombora yao mapya. Mujahid Anwar Khan, Kamanda wa vikosi vya anga nchini Pakistan ametangaza kwamba jeshi la nchi hiyo limelifanyia majaribio kombora lake jipya hii leo. Ameongeza kwamba majaribio hayo ya kombora la masafa ya mbali lililoundwa na wataalamu wa Pakistan, linaweza kuangamiza kikamilifu aina yoyote ya shabaha linaipiga. Wakati huo huo Idara ya Uchunguzi na Ustawi wa Anga nchini India (DRDO) imetangaza kwamba, jeshi la nchi hiyo limeyafanyia majaribio kwa mafanikio makombora yake aina ya Pinaka. Wasi wasi wa India na Pakistan kuingia vita kali Kwa mujibu wa taarifa hiyo, majaribio hayo yamefanyika katika jimbo la Rajasthan nchini India. Makombora ya Pinaka yanaongozwa kisasa kabisa na yana...
EU yaionya Marekani isithubutu kuivamia kijeshi Venezuela

EU yaionya Marekani isithubutu kuivamia kijeshi Venezuela

Kimataifa, Siasa
Umoja wa Ulaya umeionya Marekani kuhusu hatari ya chokochoko zake za kutaka kuivamia kijeshi Venezuela. Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini aliyasema hayo jana Jumanne mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuonya kuwa, Marekani isijaribu kuivamia kijeshi Venezuela kwani matokeo ya uvamizi huo yatakuwa ni maafa makubwa. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa EU ameongeza kuwa, Marekani inapaswa kuelewa kwamba kuna machaguo mengine bora zaidi kuliko hilo la kuivamia kijeshi Venezuela. Amesema mgogoro wa Venezuela unaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia za amani, kama kupitia mazungumzo, diplomasia na mchakato wa kisiasa.  Licha ya Juan Guaidó kuungwa mkono na Marekani na nchi za Magharibi baada ya kujitangaza kuwa r
Pompeo asema Utawala wa Trump utahakikisha Iran haiuzi nje mafuta yake

Pompeo asema Utawala wa Trump utahakikisha Iran haiuzi nje mafuta yake

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Uongozi wa rais Donald Trump utashusha mauzo ya nje ya mafuta ya Iran kufikia sifuri ndani ya muda mfupi iwezekanavyo.  Pompeo, amesema vikwazo vya Marekani vimeathiri kwa kiasi kikubwa biashara ya mafuta ya Irani duniani. Mauzo ya nje ya mafuta ya Irani imekuwa haiwezekani. Pompeo akizungumza katika wiki ya nishati ya CERA  alisema Iran imeongeza ushawishi wake mashariki ya kati hasa nchini Irak kwa kutumia sekta ya mafuta. Pompeo alisema wakati Marekani ikijaribu kujenga taifa la Irak lililokuwa huru, Iran kwa kutumia mafuta yake imekuwa ikijaribu kuitawala Irak. Pompeo aliongeza kwamba mwezi uliopita Marekani imefanya kazi ya kupunguza kiasi cha mafuta ya Iran yanayouzwa duniani lakini pia kuwashawi...
error: Content is protected !!