Siasa

Wabunge wa Umoja wa Ulaya wataka kutambuliwa rasmi nchi ya Palestina

Wabunge wa Umoja wa Ulaya wataka kutambuliwa rasmi nchi ya Palestina

Kimataifa, Siasa
Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wamezitaka nchi wanachama wa umoja huo kuitambua rasmi na haraka iwezekanavyo nchi huru ya Palestina. Wabunge wa Kamati ya Uhusiano na Palestina ya Bunge la Ulaya jana walitoa taarifa rasmi na kutaka kuchukuliwa hatua za maana na umoja huo kwa ajili ya kuunga mkono haki ya wananchi wa Palestina kujiainishia mustakabali wao. Wajumbe wa Kamati ya Uhusiano na Palestina ya Bunge la Ulaya siku ya Jumatatu walielekea Palestina kwa ajili ya kukitembelea kijiji cha Khan al-Ahmar kilichoko mashariki mwa Quds inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu. Hayo yanajiri katika hali ambayo, uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kuataka kubomoa kijiji hicho cha Khan al Ahmar mashariki mwa mji mtakatifu wa Quds umeendelea kulaaniwa kila kona ya dunia. Wapale
Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi la raia wa Zanzibar waliowasilisha kesi kupinga uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kesi hiyo isikiliziwe Zanzibar.

Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi la raia wa Zanzibar waliowasilisha kesi kupinga uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kesi hiyo isikiliziwe Zanzibar.

Siasa
Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi la raia wa Zanzibar waliowasilisha kesi kupinga uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kesi hiyo isikiliziwe Zanzibar. Rashid Salum Adiy na wenzake 39,999 kutoka Zanzibar wamewasilisha kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania wakisema muungano huo ni haramu. Walalamishi walikuwa wamejitetea kwamba wengi wao ni wakazi wa Zanzibar na huenda ikawa vigumu kwao kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo iwapo itaendelea kusikiliziwa Arusha. Ombi hilo limetupiliwa mbali na majaji katika mahakama hiyo mjini Arusha, ingawa hawakutoa maelezo kuhusu sababu zilizowaongoza kutoa uamuzi huo. Katika uamuzi wake, majaji walisema hakuna haja na wala haifai kwa mahakama hiyo kuagiza kwamba vikao vya kesi hiyo viandaliwe Zanzibar. Kifu...
Upinzani Zimbabwe wakatisha hotuba ya Mnangagwa bungeni

Upinzani Zimbabwe wakatisha hotuba ya Mnangagwa bungeni

Siasa
Wabunge wa upinzani nchini Zimbabwe Jumanne walitoka nje ya bunge wakati wa hotuba ya kitaifa iliyokuwa inatolewa na Rais Emmerson Mnangagwa. Wachambuzi wanailesa hatua hiyo kama ishara ya hasira ya wabunge hao baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais na bunge wa mwezi Julai mwaka huu. Wanachama wa Movement for Democratic Change, MDC, wakiongozwa na kiongozi wao Nelson Chamisa, ambaye alishindwa na Mnangagwa kwenye uchaguzi huo, walianza kupiga kelele katika bunge, na baadaye kuondoka, muda mfupi baada ya Mnangagwa kuanza kusoma hotuba yake. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadaye wabunge hao walianza kuimba nyimbo za kukikashfu chama kinachotawala cha Zanu PF. Kiongozi wa upinzani wa cahama cha upinzni cha Zimbabwe, MDC, Nelson Chamisa.
Kutimuliwa Balozi wa Palestina nchini Markeani; hatua mpya ya Washington katika kuunga mkono Israel

Kutimuliwa Balozi wa Palestina nchini Markeani; hatua mpya ya Washington katika kuunga mkono Israel

Kimataifa, Siasa
Hatua za kiuadui za Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Palestina na kuunga mkono kwake utawala haramu wa Israel kwa namna isiyo na kifani sasa zimeingia katika duru mpya. Marekani kama mshirika wa kistratijia wa Israel daima imekuwa ikizingatia uungaji mkono wa utawala huo kama nukta ya kimsingi ya sera zake za kigeni. Katika uga huu, baada ya Marekani kukata misaada yake kwa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina la Umoja wa Mataifa (UNRWA),  mara hii imeamua kumtimua Balozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina aliyeko Washington. Husam Zomlot, Balozi wa Palestina nchini Marekani ametangaza kuwa, wakuu wa Marekani wamemtaka aondoke nchini humo mara moja pamoja na kuwa vitambulisho vyake vilimruhusu awe balozi hadi mwaka 2020. Wakuu wa Marekani wamebatilisha visa ya Zomlo
Chama tawala chazoa viti vingi katika uchaguzi wa Bunge Mauritania

Chama tawala chazoa viti vingi katika uchaguzi wa Bunge Mauritania

Kimataifa, Siasa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Mauritania imetangaza habari ya kuibuka mshindi chama tawala nchini humo katika duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge iliyofanyika Septemba 15. Ikitoa tangazo hilo jana Jumatatu, tume hiyo imesema chama hicho cha Union for the Republic kimejizolea viti 93 kati ya 157 vya Bunge la Kitaifa. Kadhalika chama hicho tawala chake Rais Mohamed Ould Abdul Aziz kimeshinda viti vyote katika uchaguzi wa majimbo huku kikizoa manispaa 169 kati ya 219 katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Septemba Pili. Uchaguzi wa rais nchini Mauritania unatazamiwa kufanyika katikati ya mwaka 2019, na kuibuka mshindi chama tawala katika uchaguzi wa Bunge, majimbo na serikali za mitaa, ni bishara njema kwa Rais Abdul Aziz. Rais Mohamed Ould Abdul Aziz wa Maurtiania Itakumb
error: Content is protected !!