Siasa

India yajibu mapigo, yatangaza ushuru wa juu kwa bidhaa za Marekani

India yajibu mapigo, yatangaza ushuru wa juu kwa bidhaa za Marekani

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Serikali ya India imetangaza ushuru wa juu wa forodha kwa bidhaa 28 za Marekani, ikiwa ni radimali ya nchi hiyo ya Asia kwa vikwazo vya kibiashara vya Washington dhidi yake. Miongoni mwa bidhaa hizo za Marekani ambazo zimeongezewa ushuru mkubwa wa forodha ni bidhaa za chuma, matunda ya tufaha na lozi (almonds) pamoja na jozi (walnuts). Mchumi mmoja ameliambia gazeti la Times of India kuwa, kwa kuongezwa ushuru huo kwa bidhaa hizo za Marekani, serikali ya New Delhi itaweza kupokea ushuru wa ziada wa dola milioni 217. Vita hivi vya kibiashara kati ya New Delhi na Washington viliibuka Machi mwaka jana, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuongeza kwa asilimia 25 ushuru wa forodha wa bidhaa za chuma zinazoagizwa na Marekani kutoka India, na a
Watunisia waandamana dhidi ya Israel, waiunga mkono Palestina

Watunisia waandamana dhidi ya Israel, waiunga mkono Palestina

Jamii, Kimataifa, Siasa
Makumi ya wanaharakati wa kisiasa na kijamii wa nchini Tunisia kwa mara nyingine wamefanya maandamano katika barabara za mji mkuu Tunis, kulaani mpango wowote wa kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, sambamba na kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina. Katika maandamano hayo ya jana Jumamosi, waandamanaji wamesikika wakipiga nara za kuulaani utawala haramu wa Israel na sera zake dhidi ya Wapalestina. Waandamanaji hao walikuwa wamebeba bendera za Palestina na mabango yenye maandishi ya kuilaani vikali Israel na kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina. Wananchi wa Tunisia katika maandamano hayo wamewataja viongozi wa nchi za Kiarabu kuwa 'wasaliti' huku wakitaja jitihada za kufanya wa kawaida uhusiano wa n...
Mwanamuziki maarufu wa Uganda Jose Chameleon kugombea Umeya

Mwanamuziki maarufu wa Uganda Jose Chameleon kugombea Umeya

Kimataifa, Michezo, Siasa
Joseph Mayanja, almaarufu kama Jose Chameleone, mwanamuziki maarufu kutokea Uganda ametangaza nia ya kushindana na Erias Lukwago kugombea kiti cha meya wa jiji la Kampala nchini . Hivi karibuni  Chameleone  alijiunga na Harakati ya nguvu za watu “People Power Movement”,  kundi la harakati linaloongozwa na mwanamuziki mwenzie aliyeibukia katika siasa, Bobi Wine.
Mapigano yaendelea nchini Libya

Mapigano yaendelea nchini Libya

Jamii, Kimataifa, Siasa
Vita kali inaendelea kuzunguka eneo la uwanja wa ndege wa Tripoli ikihusisha majeshi ya serikali ya makubaliano ya kitaifa Libya na majeshi ya Jenerali Haftar. Ndege za kivita za majeshi ya Haftar zilipiga maeneo mbalimbali ya majeshi ya serikali yaliyopo Tripoli na Tacure. Meya wa mji wa Tacure aliwaambia wanahabari kwamba kutokana na mashambulizi hayo yaliyofanywa na vikosi vya Jenerali Haftar, baadhi ya raia walijeruhiwa. Kiongozi wa kijeshi anayeongoza mashariki ya Libya, jenerali Khalifa Haftar alitoa amri ya kushambulia ili kuikamata Tripoli mnamo April 4, Kutokana na amri hiyo walianzisha oparesheni dhidi ya majeshi ya serikali yaliyopo katika mji wa Tripoli.
Russia yaishukuru Iran kwa juhudi zake za kuwaokoa mabaharia wa meli zilizoshambuliwa

Russia yaishukuru Iran kwa juhudi zake za kuwaokoa mabaharia wa meli zilizoshambuliwa

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa shukurani zake za dhati kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na juhudi zake za kuwaokoa mabaharia wa Kirusi waliokuwa kwenye meli mbili za mafuta zilizoshambuliwa siku ya Alkhamisi katika maji ya Bahari ya Oman. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia sambamba na kuishukuru Iran kwa hatua hiyo, pia imelaani vikali shambulizi dhidi ya meli hizo. Kadhalika wizara hiyo imetaka kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kuzuia hali ya mambo kuwa mbaya zaidi katika eneo la Asia Magharibi na kuongeza kuwa, utolewaji tuhuma dhidi ya upande fulani kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufanyika uchunguzi wa kimataifa usiopendelea upande wowote ni jambo lisilokubalika. Alkhamisi iliyopita vyombo vya habari viliripoti kujiri shambulizi...
error: Content is protected !!