Nyumbani

Zoezi la kuchanja mbwa kufanyika kesho Ndijani

Zoezi la kuchanja mbwa kufanyika kesho Ndijani

Nyumbani
IDARA ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar, kesho inatarajia kufanya zoezi la kuwanja mbwa katika kijiji cha Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na kichaa cha mbwa.  Hafla hiyo itakuwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa, ambapo kimataifa iliadhimishwa Septemba 28.  Mkuu wa huduma za maabara ya mifugo, Dk. Khadija Noor Omar, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili kwa njia ya simu.  Alisema pamoja na zoezi hilo, pia watatoa elimu kwa wafugaji kwa ujumla pamoja na watoto katika kijiji hicho.  Alisema tangu kuanza kwa utaratibu wa kuchanja mbwa hadi sasa, wamefanikiwa kwa asilimia 63 ya mbwa waliochanjwa ambapo malengo yao ya baadae ni kufikia asilimia 70.  Alisema lengo la kimataifa ni kutokomeza mara
Dk. Shein atuma rambi rambi Indonesia

Dk. Shein atuma rambi rambi Indonesia

Nyumbani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Indonesia, Joko Widodo, kufuatia tetemeko la ardhi lililoambatana na tsunami lililotokea katika kisiwa cha Sulawesi Ijumaa ya Septemba 28, 2018 na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa. Katika salamu zake, alisema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar pamoja na wananchi wake, anatuma salamu hizo kwaserikali, familia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa Indonesiakufuatia tukio hilo kubwa lakusikitisha lililosababisha vifo vya watuwapatao 832 na majeruhi kadhaa. Kufuatia tukio hilo, Dk. Shein alimtumia salamu hizo Rais Widodo na kumuomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Aidha, alimuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira ndugu, jamaa, m...
Vitambulisho vya Mkazi vyamuibua Mbunge wa Jimbo la Malindi Unguja

Vitambulisho vya Mkazi vyamuibua Mbunge wa Jimbo la Malindi Unguja

Nyumbani, Siasa
Mbunge wa Jimbo la Malindi (CUF) Mh. Ali Saleh amelaani vikali kitendo cha badhi ya wananchi kuzuiliwa kuandikisha vitambulisho vya Mzanzibari  mkaazi katika jimbo lake. Mbunge Ali Saleh ametoa kauli hiyo Leo Oktoba 1 2018,  majira ya saa 7 mchana wakati akizungumza na Wandishi wa Habari Skuli ya Darajani Mjini Unguja. Amesema zoezi la vitambulisho katika jimbo la Malindi limekubwa na baadhi ya changamoto zikiwemo usumbufu kwa waliopoteza vitambulisho, waliohama pamoja na vijana ambao ndio kwanza wanafikisha miaka 18. “Sheria haisemi kuwa kama vijana wapya wanasiku yao yakujiandikisha wakati mzanzibari aliefikia miaka 18 anayo haki ya kujiandikisha sasa hawa wakija kujiandikisha pana usumbufu mkubwa unaotokezea” Akizungumza na waandishi wahabari miongoni mwa kijana aliefikw
CUF yaendeleza mgomo Zanzibar, yasusia chaguzi Jimbo la Jang’ombe

CUF yaendeleza mgomo Zanzibar, yasusia chaguzi Jimbo la Jang’ombe

Nyumbani, Siasa
Chama Cha Wananchi  (CUF) Zanzibar kimesema hakita shiriki Uchaguzi wa ubunge au wawakilishi wa majimbo ya Zanzibar hadi utakapofika uchaguzi mkuu mwaka 2020 kwa kile walichokidai kushiriki chaguzi hizo ni kuhalalisha matokeo ya Uchaguzi wa marudio ya Urais yaliofanyika machi 20 mwaka 2016 na kumpitisha Dkt Shein kuwa Rais. Akizungumza Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF Mbarara Maharagande amesema chama hicho hakija msimamisha mgombea yeyote kwenye marudio ya Uchaguzi wa kupata mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe licha ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza kumsimamisha. “Kama chama msimamo wetu ni kwamba hatutashiriki uchaguzi wa Jang’ombe, sababu uchaguzi huo umetokana na uchaguzi haramu wa machi 20 2016, kwa hiyo hatutashiriki uchaguzi wowote, utak
error: Content is protected !!