Nyumbani

SHILINGI milioni 391 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kifuta jasho kwa wasimamizi wa mashamba ya serikali ya mikarafuu.

SHILINGI milioni 391 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kifuta jasho kwa wasimamizi wa mashamba ya serikali ya mikarafuu.

Biashara & Uchumi, Nyumbani
SHILINGI milioni 391 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kifuta jasho kwa wasimamizi wa mashamba ya serikali ya mikarafuu. Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi, wa Pemba Sihaba Haji Vuai, aliyasema hayo wakati akizunguzma na mwandishi wa gazeti hili huko Wizara ya Kilimo, Maliasili na Uvuvi Maruhubi. Alisema fedha hizo zitatumika kwa wakulima 835 ambao walifanyiwa uhakiki juu ya usimamizi wa mashamba hayo. Aidha alisema awali walipanga kutumia shilingi 479,075,500 kwa kuwalipa wakulima 1,010, lakini kutokana na badhi ya wakulima kukosa sifa stahiki ya usimamizi wa mashamba hayo. Alisema malipo ya wakulima hao tayari yameanza kutolewa kwa kuanzia Septemba 11 mwaka huu ambapo wakulima hupokea fedha hizo kwa kiwango tofauti. Alisema hatua hiyo ni moja...
TAMWA watoa somo kwa walezi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu

TAMWA watoa somo kwa walezi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu

Jamii, Nyumbani
Wazazi na Walezi Mkoa wa kaskazini Unguja wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha na kutowapeleka skuli watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) jambo linalopelekea kuwa nyuma kimaendeleo na kuwasababishia watoto hao kuwa tegemezi. Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Wilaya ya Kaskazin “B” Unguja  Mshamara Chum Kombo katika mkutano maalum wa kujadili matatizo wanayokabiliana nayo wananchi katika mkoa wa kaskazini Unguja ikiwa ni muendelezo wa kutekeleza mradi wa Paza kushirikiana na wanaharakati na  Jumuiya za maendeleo katika vijiji husika katika Nyanja za Elimu , Afya, kilimo, mazingira  na maji, Alisema tatizo la kuwaficha na kutowapeleka skuli  kupata elimu  watoto wenye mahitaji maalum kwa mkoa wa kaskazini Unguja limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuwazorotesha watoto ha
CUF ya Lipumba yavitaka vyama vya siasa kuiunga mkono Serikali

CUF ya Lipumba yavitaka vyama vya siasa kuiunga mkono Serikali

Nyumbani
Mratibu wa uchaguzi wa chama cha wananchi Cuf Ali Makame Issa amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo nchini. Ali Makame Issa ambaye mratibu wa chama cha wananchi CUF kwa upande wa Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba visiwani Zanzibar, Alisema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikijitahidi kwa namna tofauti tofauti katika kuhakikisha inapiga hatua katika suala zima la maendeleo. “Suala zima la maendeleo halina chama cha siasa kwani wote lengo letu kujenga nyumba moja”alisema Ali Makame Issa. Aidha alisema viongozi  wa vyama vya siasa wanaojitambua huwa wapo mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo na Si kuibeza. “Ukiwa upo kati
MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani, katika kijiji cha Kikungwi wilaya ya kati Unguja.

MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani, katika kijiji cha Kikungwi wilaya ya kati Unguja.

Jamii, Nyumbani
MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani, katika kijiji cha Kikungwi wilaya ya kati Unguja. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan, alisema tukio hilo limetokea saa 11:30 na kumtaja marehemu kuwa ni Asha Mohamed Muombwa mkaazi wa Kikungwi. Alisema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Mnazimmoja na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi. Hivyo, alitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia uamuzi sambamba na kuwa na ushirikiano na familia zao ili kuweza kuepusha vifo vilivyokuwa sio vya lazima. Nae Mratibu wa wanawake na watoto shehia ya Kikungwi, Bahati Issa, alisema, marehemu huyo alichukua hatua hiyo kutokana na msongo wa mawazo, kwa...
Zaidi ya madawati 22,000 yanatarajiwa kuingia nchini mwishoni mwa mwezi huu yakitokea China.

Zaidi ya madawati 22,000 yanatarajiwa kuingia nchini mwishoni mwa mwezi huu yakitokea China.

Jamii, Nyumbani
ZAIDI ya madawati 22,000 yanatarajiwa kuingia nchini mwishoni mwa mwezi huu yakitokea China. Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya kampeni ya uchangishaji madawati, Haroun Ali Suleiman, aliyasema hayo wakati akizungumzan na gazeti hili ofisini kwake Mazizini Unguja. Alisema madawati hayo yatagaiwa kwa skuli mbalimbali visiwani Zanzibar, yakiwa na lengo la kuondosha uhaba wa madawati uliopo katika skuli mbalimbali. Alisema awamu ya pili ya madawati hayo yataingia nchini mwezi Disemba mwaka huu ikitokea nchini China. Alisema ujio wa madawati hayo ni kutokana na harambee maalum uliyofanywa na kamati yake ambayo imekusanya jumla ya shilingi bilioni 1.4 kutoka kwa taasisi za umma, binafsi na watu mbalimbali. Haroun ambae pia ni Waziri wa Nchi, Katiba, Sheria na Utumishi wa Umma ...
error: Content is protected !!