Nyumbani

Wanaume Pemba watilia shaka ripoti ya Milele Foundation

Wanaume Pemba watilia shaka ripoti ya Milele Foundation

Nyumbani
WANAUME kisiwani Pemba, wameijia juu ripoti ya hivi karibuni iliosilishwa na Taasisi ya Milele Foundation Zanzibar mbele ya viongozi wa serikali, iliopewa jina la utafiti na kutaja kuwa wanawake 1, 316 wanaziongoza familia wakiwemo walioachika au kufiwa na waume. Aidha uwasilishwaji wa ripoti hiyo, ilisema asilimia 70 akinamama wajawazito, wa Mkoa wa kaskazini Pemba na asilimia 68 kwa Mkoa wa kusini Pemba, wanaupungufu wa damu, jambo ambalo wanaume hao walisikitishwa nalo. Wakizungumza na mwandishi wa habari kwa nyakati tofauti, walisema utafiti huo, unaonesha hakufanywa kiuhalisia, jambo ambalo limetoa takwimu zenye mashaka. Mmoja kati ya wanaume hao Abdillah Omar Himid wa mjini Chakechake, alisema utafiti huo haukuonesha kundi lipi la wanawake ambao ndio linajiongoza wenyewe...
Vijana 50 Wete kupata ajira za muda kuusafisha mji

Vijana 50 Wete kupata ajira za muda kuusafisha mji

Nyumbani
ZAIDI ya vijana 50 katika mji wa Wete wanatarajia kunufaika na ajira za muda za kufanya usafi wa mazingira ili kuunga mkono juhudi za Baraza la Mji huo za kuuweka mji katika mandhari ya kuridhisha. Vijana hao ambao watatoka kwenye vikundi , watakuwa na jukumu la kushirikiana na watendaji wa Baraza la Mji kusafisha mazingira baada ya uongozi wa baraza kukabiliwa na uhaba wa wafanyakazi. Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Hamad Mbwana Shehe , amesema uwamuzi huo umechukuliwa na Baraza baada ya kubaini kwamba uhaba wa wafanyakazi unasababisha baadhi ya maeneo kutofikiwa kufanyiwa usafi. Hamad ameyasema hayo kufuatilia malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wananchi juu ya kutofanyika usafi wa maeneo ya Mji huo hususani kwa siku ya Jumamosi na Jumapili hali ambayo inasababisha kuwepo ...
Adhabu kali zaendelea kutolewa dhidi ya wanaomkashifu rais Tanzania

Adhabu kali zaendelea kutolewa dhidi ya wanaomkashifu rais Tanzania

Nyumbani
Wanaotoa lugha za dhihaki dhidi ya Rais wa Tanzania ,John Magufuli waendelewa kushitakiwa Raia mwingine nchini Tanzania amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi sita au kulipa faini ya sh.200,000 kwa kosa la kutumia lugha ya kumdhihaki rais Magufuli. Yuston Emmanuel mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mkaAzi wa Ngara mkoani Kagera,Tanzania amehukumiwa kwa kosa a ambalo mwendesha mashtaka alidai kwamba alikuwa amekwenda kinyume na kifungu cha 89(1) (a) cha kanunu ya adhabu iliyorekebishwa na kuna umuhimu wa adhabu kali kutolewa ili iwe fundisho kwa wengine. Raia huyo ni miongoni mwa watu wasiopungua kumi wa nchi hiyo, idadi ambayo inajumuisha viongozi wa upinzani na raia wa kawaida walioshitakiwa kwa kosa la kumdhihaki au kumtusi rais Magufuli tangu aingie madarakani. Mwezi Juni...
Mjasiriamali Chakechake aonyesha ubunifu akitumia zana za kizamani

Mjasiriamali Chakechake aonyesha ubunifu akitumia zana za kizamani

Biashara & Uchumi, Nyumbani, Teknolojia
MJASIARIAMALI Nathoo Abdullkarim Nathoo akiwaonesha Viongozi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, wakiongozwa na Afisa Mdhamini Wizara hiyo Fatma Hamad Rajab na Afisa Mipango Omar Juma Ali, jinsi gani anavyofanya kazi zake kwa kutumia dhana za kizamani, wakati akichapisha fulana kwa kutumia kibao alichotengeneza mwenyewe.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) AFISA Mdhamini  Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab akiangalia utendaji wa kazi wa utengenezaji wa nembo na kudizaini vitu mbali mbali, kwa kutumia Komputa kutoka kwa mjasiriamali Nathoo Abdullkarim Nathoo wa Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
Baba wa kambo adaiwa kumbaka mtoto wa mkewe huko Ndijani Kusini Unguja

Baba wa kambo adaiwa kumbaka mtoto wa mkewe huko Ndijani Kusini Unguja

Jamii, Nyumbani
Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Unguja limempandisha katika kizimba cha mahakama ya mkoa Mwera mtuhumiwa Bakari Makame Khatib miaka 30 mkaazi wa Binguni wilaya ya kati kwa kosa la kumuingilia maharimu wake. Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka Shumbana Mbwana mbele ya hakimu Harub Shehe Pandu kwamba mnamo tarehe 19, 3, 2018 majira ya saa 1 usiku huko Ndijani mkoa wa Kusini Unguja bila ya halali na kwamakusudi mtuhumiwa alimuingilia kimwili binti wa miaka 18 ambaye ni mtoto wa mkewe jina linahifadhiwa huku akijua kuwa jambo hilo ni kosa kisheria. Baada ya kusomewa kosa lake mahakamani hapo Mtuhumiwa alikataa kosa na kuiomba mahakama impe dhamana ambapo mahakama imeamuru aende rumande hadi tarehe 24, 9, 2018 ndipo itakaposikilizwa dhamana yake.
error: Content is protected !!