
TAMWA watoa somo kwa walezi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu
Wazazi na Walezi Mkoa wa kaskazini Unguja wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha na kutowapeleka skuli watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) jambo linalopelekea kuwa nyuma kimaendeleo na kuwasababishia watoto hao kuwa tegemezi.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Wilaya ya Kaskazin “B” Unguja Mshamara Chum Kombo katika mkutano maalum wa kujadili matatizo wanayokabiliana nayo wananchi katika mkoa wa kaskazini Unguja ikiwa ni muendelezo wa kutekeleza mradi wa Paza kushirikiana na wanaharakati na Jumuiya za maendeleo katika vijiji husika katika Nyanja za Elimu , Afya, kilimo, mazingira na maji,
Alisema tatizo la kuwaficha na kutowapeleka skuli kupata elimu watoto wenye mahitaji maalum kwa mkoa wa kaskazini Unguja limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuwazorotesha watoto ha