Nyumbani

Ukweli kuhusu mgomo wa wafanyakazi kitengo cha huduma kwa wateja Zantel, Zanzibar

Ukweli kuhusu mgomo wa wafanyakazi kitengo cha huduma kwa wateja Zantel, Zanzibar

Biashara & Uchumi, Nyumbani
Wafanyakazi wa shirika la mawasiliano ya simu Zanzibar Telecom Limited (ZANTEL) kitengo cha huduma kwa wateja wamegoma kufanya kazi hiyo kwa madai kuwa mshahara wanaolipwa na shirika hilo ni mdogo na utaratibu wa kazi hauzingatii usalama wa afya ya mfanyakazi. Mgomo huo umefanyika mapema jana Septemba 28 majira ya asubuhi nje ya ofisi za ZANTEL Amani Mjini Unguja. Wafanyakazi hao ambao ni Wanafunzi waliomaliza Digree na Diploma za fani tofauti kutoka chuo cha Zanzibar University (ZU) na chuo cha Karume Institute of Science and Technology (KIST) wamelalamikia mazingira ya kazi kuwa si salama kwa afya zao na mshahara wanaopewa haukidhi mahitaji. Wamesema wanafanya kazi kwa saa 8 kila siku na kwa mtu mmoja hupokea zaidi ya simu 160 hadi 200 kwa siku jambo ambalo ni hatari kwa...
Wafanya biashara wahimizwa kutunza kumbukumbu zao

Wafanya biashara wahimizwa kutunza kumbukumbu zao

Biashara & Uchumi, Nyumbani
Wafanya biashara kisiwani Pemba wamehimizwa kutimiza wajibu wao kwa kulipa kodi kwa hiari   pamoja na kutunza kumbukumbu  zote  wanazolipia kodi ili kuepusha usumbufu wakati wa kuingiza na  kusafirisha  mizigo ya biashara zao. Maelezo hayo yametolewa na Afisa Mdhamini  Wizara ya Fedha na Mipango Pemba Ibrahim Saleh Juma  alipokuwa akifungua mkutano kati na wafanya biashara  wa  Mkoa wa Kusini Pemba na Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB uliofanyika huko katika ukumbi wa  baraza la mji chake chake ambapo mbali ya mambo mengine ulikuwa na dhamira ya kuwasilisha mabadiko ya sheria za kodi za Zaznibar. “kulipia kodi ni wajibu kwa kila mfanyabiashara hivyo kwa maendeleo ya nchi usisubiri mpaka ulazimishwe kufanya hivyo lipa kodi kwa hiari na ujiepushe na usumbufu”alisema afisa mdhamini huyo
Ujasiriamali kwa wanawake isiwe sababu ya kwenda kinyume na mafundisho ya dini

Ujasiriamali kwa wanawake isiwe sababu ya kwenda kinyume na mafundisho ya dini

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
WANAWAKE wa kiislamu nchini, ambao ni wajasiriamali, wameshauriwa kuyahifadhi maungo yao wakati wote, wanapokuwa kwenye shughuli zao, na sio kuyaacha wazi na wengine kufikiria kuwa, kufanya hivyo, ndio sahihi. Ushauri huo umetolewa na ustadhati Khadija Mohamed Hassan wa Mtambile, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya ruhusa kwa wanawake kuijiingiza kwenye ujasiriamali na uzingatiaji wa maadili. Alisema, hakuna aya wala hadithi ambayo inamkataza mwanamke kujiingiza kwenye biashara yoyote halali, bali kinachotakiwa kutanguliwa ni kuulinda kwa kuuhifadhi mwili wake wakati wote. Alisema kujiingiza kwenye biashara kama za kuuza nazi, samaki, duka, uchongaji na hata kuwa dereva wa taxi, isiwe sababu kwa wanawake hao, kuyaweka wazi maungo yao. Ustadhati huyo al...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amewateua Dk. Ali Makame Ussi na Dk. Haroun Ayoub Maalim, kuwa Naibu Makamu Wakuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amewateua Dk. Ali Makame Ussi na Dk. Haroun Ayoub Maalim, kuwa Naibu Makamu Wakuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Nyumbani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amewateua Dk. Ali Makame Ussi na Dk. Haroun Ayoub Maalim, kuwa Naibu Makamu Wakuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Kwa mujibu wa taarifa ya SUZA kwenda kwa wananchi na wadau wa chuo hicho, Dk. Ussi ameteuliwa kuwa Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho atakaeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri. Aidha Dk. Maalim ameteuliwa kuwa Naibu Makamu Mkuu atakaeshughulikia Fedha na Utawala. Dk. Shein ambae pia ni Mkuu wa Chuo hicho, amefanya uteuzi huo chini ya sheria namba 11 ya 2009 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kifungu cha 4(10) (1). Uteuzi huo umefanywa kufuatia waliokuwa wakishikilia nafasi hizo, Dk. Zakia Mohamed Abubakar (Naibu Makamu Mkuu-Fedha na Utawala) na Dk.Haji Mwevu...
error: Content is protected !!