Nyumbani

Utoaji Leseni ya utangazaji kupitia mitandaoni ‘Online’ Zanzibar

Utoaji Leseni ya utangazaji kupitia mitandaoni ‘Online’ Zanzibar

Nyumbani
Katika kutambua mchango wa mitandao ya kijamii katika kusambaza habari mbalimbali kwa jamii, Rasmi Leo Septemba 25, 2018 Serikali ya mapinduzi kupitia Tume ya utangazaji Zanzibar imekabidhi vyeti vya usajili kwa vyombo vya habari 10 vinavyorusha habari kwa njia ya mitandaoni (online TV na Blogs) kutoka Zanzibar. Miongoni mwa vyombo vilivyopatiwa leseni hizo ni Mubashara Media Network inayomiliki mtandao pendwa wa Zanzibar24, Mtandao wa ZBC, Habari maelezo Zanzibar, Pemba Tv online, Ktv online, Zanzinews, Jazeera Pemba, Mambo tv, n.k. Tukio la kukabidhiana vyeti hivyo (leseni) limefanyika majira ya saa 10 jioni katika ukumbi wa mikutano wizara ya habari Kikwajuni Mjini Zanzibar Akikabidhi leseni hizo kwa wahusika Waziri wa habari Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Th...
Dk. Karume atuma rambi rambi ajali MV.Nyerere

Dk. Karume atuma rambi rambi ajali MV.Nyerere

Nyumbani
RAIS mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, amemtumia salamu za rambi rambi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, kufuatia msiba wa ajali ya kivuko cha MV. Nyerere, kilichozama katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza. Katika salamu hizo, alisema msiba huo ni mkubwa kwa Watanzania wote, hivyo ni vyema kwa waliopatwa na janga hilo kuwa wastahamilivu na kushirikiana na serikali katika kipindi hiki cha maombolezi. Alisema ameguswa na msibahuo, ambao umepoteza maisha ya Watanzania hasa wanawake kwa kuwa idadi kubwa ya waliopoteza maisha walikuwa wanawake. Aliwaombea majeruhi wa ajali hiyo, kupona haraka na kuwashukuru wananchi wote wa Ukara waliojitokeza kusaidia kazi ya uokoaji tangu ajali hiyo ilipotokea. Pia aliwashukuru wote...
Kilomita 14 zimeshatiwa lami barabara Ole-Kengeja, Katibu Mkuu Fedha atoa neno

Kilomita 14 zimeshatiwa lami barabara Ole-Kengeja, Katibu Mkuu Fedha atoa neno

Nyumbani
KATIBU Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Khamis Mussa Omar, amesema kazi ya ujenzi wa barabra ya Ole Kengeja unaendelea vyema, licha ya mradi huo kukubwa na changamoto mbali mbali katika ujenzi wake. Alisema kwa sasa tayarai kilomita 11 zimeshawekewa lami, kutoka Ole hadi skuli ya Fidel Castro, jambo ambalo ni la kupongeza na kuridhisha huku kazi ikiendelea sehemu nyengine. Katibu Mkuu huyo,m aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo,eneo la Pujini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. “Licha ya ujenzi wa barabara hii kuchelewa kutokana na changamoto mbali mbali, lakini tunamshukuru Mungu kazi inafanyika vizuri na kila mtu anaiyona,”alisema. Alisema wananchi wanaotumia barabara ya Ole hadi kijiji c
Aliyedhaniwa kuwa Mchawi azusha Tafrani Kwarara Zanzibar

Aliyedhaniwa kuwa Mchawi azusha Tafrani Kwarara Zanzibar

Jamii, Nyumbani
Mzee mmoja anaekadiriwa kuwa na miaka 60 amezusha tafrani kubwa huko Kwarara maduka sita Wilaya ya Magharibi B Unguja baada ya kuomba choo na kuhisiwa anafanya mambo ya ushirikina katika choo hicho. Tukio hilo limetokea jana Septemba 23 majira ya saa 10 jioni. Akizungumza na Zanzibar24 mama mwenye nyumba hiyo amesema kuwa, Bibi  huyo alikwenda kuomba choo nyumbani hapo majira ya saa 10 jioni na kuruhusiwa kwenda kufanya haja yake, lakini alikawia kutoka chooni hapo na hatimae mama mwenye nyumba kumchunguza kwa kumchungulia na kumbaini anafanya shughuli zisizo za kawaida chooni hapo. “Nilikua nachoma mikate baada ya kumaliza kuchoma mikate nilikaa muda wa nusu saa sisikii maji chooni kitendo hicho kilinishangaza na kunitia hofu nilikwenda nikafungua pazia kwakumtizama nika muona k
error: Content is protected !!