Nyumbani

Balozi Karume awataka vijana waongeze ubunifu

Balozi Karume awataka vijana waongeze ubunifu

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
WAZIRI wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Ali Abeid Karume, amewataka vijana kuwa wabunifu wa kijasiriamali na kuondokana na mawazo ya kuajiriwa ili kujiongezea kipato na kutoa mchango zaidi kwa maendeleo ya taifa. Hayo ameyaeleza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa vijana waliopatiwa mafunzo ya namna ya kujiajiri huko Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), Mbweni mjini Unguja jana, Mafunzo hayo yaliendeshwa na Shirika la VSO kupitia ufadhili wa Shell Exploration and Production Tanzania na yaliwashirikisha vijana 40. Balozi Karume, alisema, ubunifu wa miradi ya ujasiriamali ni njia muhimu ya kuleta maendeleo endelevu kwa vijana na taifa badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini. “Ukiajiriwa ni utumwa, ukijiajiri unajituma”, alisema, Balo
Wakulima Upenja wapatiwa mbegu

Wakulima Upenja wapatiwa mbegu

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, imewakabidhi wakulima wa mpunga wa bonde la Upenja mkoa wa Kaskazini ‘B’ Unguja, kilo 200 za mbegu aina ya ahmada ambayo inazaa katika kipindi kifupi. Hivi karibuni gazeti hili liliripoti hasara waliyopata wakulima wa bonde hilo baada ya mpunga wao kushambuliwa na wadudu waharibifu aina ya kunguni mgunda. Akikabidhi mbegu hiyo kwa niaba ya Waziri wa kilimo, Mkurugenzi idara ya kilimo, Mohammed Rashid, aliwaomba wakulima kuitumia mbegu hiyo haraka iwezekanavyo kwa sababu msimu wa kilimo umepita ila kwa sababu mvua zinaendelea kunyesha mbegu hiyo inaweza kustawi vizuri. Alisema wizara baada ya kuwatembelea wakulima hao na kuona athari iliyojitokeza walichukua hatua za haraka kwa kuwatafutia mbegu. Alisema mbegu hiyo ina u
Balozi Ramia ataka masoko mapya ya utalii

Balozi Ramia ataka masoko mapya ya utalii

Biashara & Uchumi, Nyumbani
WADAU wametakiwa kuhakikisha wanautangaza vyema utalii wa Zanzibar ili waweze kufikia masoko mapya yaliyopo barani Asia na Mashariki ya Kati. Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohammed Ramia, alieleza hayo jana wakati akifungua mkutano wa kujadili mkakati na changamoto zilizopo katika sekta ya utalii uliofanyika katika hoteli ya Madinat al Bahar iliyopo Chukwani. Alisema ni vyema kwa wadau hao, kutoa taarifa sahihi kwa wageni zinazohusiana na masuala ya utalii sambamba na kutumia vyema maeneo ya kihistoria yaliopo nchini, kwani itasaidia kutumia fursa ya masoko hayo. Pia aliwataka wadau hao, kuhakikisha wanalipa kodi na kufuata sheria za nchi ili ukusanyaji wa mapato eneo hilo uwe endelevu sambamba na kuwa eneo muhimu linaloendelea kuchangia vizuri pato la taifa. ...
error: Content is protected !!