Nyumbani

Lady Jay Dee anogesha tamasha la utalii Zanzibar

Lady Jay Dee anogesha tamasha la utalii Zanzibar

Nyumbani
MALKIA wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee ‘Bint Machozi’, amesema wasanii wana nafasi kubwa ya kuutangaza utalii wa Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia sanaa wanazofanya. Alisema kupitia muziki, ngoma za asili na aina nyenginezo za utamaduni, sanaa hizo zimekuwa nyenzo muhimu katika kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi na kuitembelea Zanzibar ambayo imebarikiwa kuwa na vivutio kadhaa. Jay Dee aliyasema hayo katika hafla maalum iliyoandaliwa na Mkahawa wa 6 degrees South, ulikopo Shangani Zanzibar, unaomilikiwa na Mwekezaji Mzalendo Saleh Said, ikiwa ni shamrashamra za kufanikisha Tamasha la Utalii Zanzibar, lililozinduliwa hivi karibuni. Katika hafla hiyo iliyohusisha viongozi mbali mbali wa serikali, wawekezaji , wadau wa Utalii pamoja na wageni mbalimbali, msanii hu
Wanafunzi 3,000 kupewa mikopo – Zanzibar

Wanafunzi 3,000 kupewa mikopo – Zanzibar

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mmanga Mjengo Mjawiri, ameitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar, kuwashirikisha wadau wote wa elimu katika suala la ulipaji wa mikopo ili kurahisisha urejeshaji wa fedha za wananchi. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa bodi hiyo katika muendelezo wa ziara zake katika idara zilizopo chini ya wizara yake hiyo. Alisema, hatua hiyo itasaidia kuondosha tatizo la mrundikano wa madeni yaliyotokana na wanafunzi kutoresha mikopo yao kwa wakati. Alifahamisha kuwa baadhi ya wanufaika wanashindwa kurejesha mikopo baada ya kumaliza masomo yao jambo ambalo linasababisha wenzao kushindwa kukopeshwa. Aliwasisitiza watendaji wa bodi hiyo kuwasimamia wote waliokopeshwa ili kuhakikisha fedha zilizotolewa zirudi n...
Maimamu Zanzibar wataja chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika

Maimamu Zanzibar wataja chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika

Jamii, Nyumbani
Kuanzishwa kwa chuo cha maadili ya ndoa  zanzibar kutaweza kusaidia kupunguza wimbi kubwa la talaka pamoja na  kuondoa migogoro kwenye familia. Akizungumza katika Mafunzo Maalumu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maimam zanzibar huko Mkwajuni TC   kwa ajili ya Mashekh na Makadhi wenye jukumu la kufungisha ndoa za waislamu nchini Mwezeshaji wa jumuiya hiyo Shekhe Iddi Said amesema chuo kilichoa anzishwa kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa wanandoa na jamii kwa ujumla kwani utafiti unaonesha chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika ni kukosekana kwa elimu ya maadili ya ndoa kwa jamii hivyo chuo kimelenga kutoka mafunzo maalumu yatakayo wajenga wanandoa  kuwa na mapenzi na huruma pamoja na maadili katika ndoa zao. Amewataka Mashekh na Makadhi kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa elimu katika maeneo
Malindi, Mwenge zaanza na mkosi ligi kuu

Malindi, Mwenge zaanza na mkosi ligi kuu

Michezo, Nyumbani
LIGI Kuu ya soka Zanzibar jana iliendelea kupigwa katika viwanja vinne tofauti Unguja na Pemba, huku timu zikiendelea kuvuna pointi tatu muhimu. Katika michezo iliyopigwa dimba la Amaan, ambapo majira ya saa 8:00 mchana timu ya Mafunzo imefanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wakongwe wa soka Zanzibar Malindi. Mchezo huo ambao ulikuwa mzuri na kupendeza kwa muda wote, Mafunzo ilijipatia bao la mapema dakika ya tano lililofungwa na Mohamed Abdulrahim Mbambi, kwa njia ya penalti. Hata hivyo baada ya bao hilo mchezo ulizidi kuwa wa kasi huku Malindi ikisaka bao la kusawazisha kila pembe, wakati Mafunzo wao wakisaka bao la pili lakini hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Mafunzo iliongoza kwa bao moja. Kipindi cha pili Malindi ilianza kwa kulisakama lang...
error: Content is protected !!