Mikoani

TANESCO Yawasha Kituo Kipya Cha Kupoza na Kusambaza Umeme Madaba Mkoani Ruvuma.

TANESCO Yawasha Kituo Kipya Cha Kupoza na Kusambaza Umeme Madaba Mkoani Ruvuma.

Biashara & Uchumi, Mikoani
Kituo kipya na cha kisasa cha Madaba Mkoani Ruvuma kikiwa kimewashwa rasmi usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Ujenzi wa kituo hicho ambao ulianza mwaka 2017, ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea wa msongo wa 220/33kV na sasa Songea imeunganishwa na Gridi ya Taifa na tayari mitambo ya kufua umeme wa jenereta iliyoko Songea mjini imezimwa rasmi, amethibitisha  Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO Bi. Leila Muhaji. HISTORIA imeandikwa upya kwa wakazi wa mji wa Songea na viunga vyake, baada ya serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwasha kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 220/33kv cha madaba usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Kituo hicho ni sehemu ya vituo vipya vitano vilivyojengwa chini ya mradi wa umeme Makambaka- Songea. K
Rais Magufuli amuagiza Dkt. Jingu kusimamia usajili na uratibu wa NGO nchini

Rais Magufuli amuagiza Dkt. Jingu kusimamia usajili na uratibu wa NGO nchini

Mikoani
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. John Jingu, kusimamia kwa karibu usajili na uratibu wa NGO nchini kwa kuwa kumekuwa na vitendo vya ovyo vinavyofanywa na asasi hizo. Dk. Magufuli alisisitiza kuwa NGO zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ambazo pamoja na mambo mengine zinatakiwa kuendesha shughuli zao kwa uwazi hususani katika masuala ya mapato na matumizi ya fedha za ufadhili wa shughuli zake. “Nataka ukasimamie usajili na uratibu wa NGO, najua zipo chini ya maendeleo ya jamii, kasimamie kuwe na uwazi wa utendaji kazi wa NGO,” alisisitiza Rais Magufuli. Rais Magufuli aliyasema hayo jana katika Ikulu ndogo ya Chamwino, wakati wa hafla ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, J
KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H

KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa, Mikoani, Nyumbani, Teknolojia, Updates
REF: MM/OD/E/2018/TO/SE11-077                                                                         11-09-2018 Taarifa kwa Umma, As Salaam A’laykum, KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Allah (S.W) kwa kutujaalia sote tukiwa wazima wa Afya na wale wote waliowagonjwa basi Allah awajaalie siha njema, pia kumtakia rehma mtume wetu Muhammad (S.A.W) pamoja na maswahaba wake, wake zake, jamaa zake na waislamu wote kwa ujumla dunia. Pia tunawaombea ndugu zetu katika imani ambao wametangulia mbele ya haki, Kampuni ya Moyo Media tunayo furaha kusherehekea mwaka mpya wa kiislamu 1440 H, Kwa niaba ya Uongozi wa kampuni, tunawatakia wafanyakazi wetu wote na waislamu duniani kote kheri na Baraka za mwaka 1440 H, Tunakuomba Mungu wet
Wafanyabiashara Watakiwa Kutumia Mawakala Waliothibitishwa na TRA Kupata Karatasi za Risiti.

Wafanyabiashara Watakiwa Kutumia Mawakala Waliothibitishwa na TRA Kupata Karatasi za Risiti.

Biashara & Uchumi, Mikoani
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb). Na.Peter Haule. Serikali imetatua tatizo la kuwepo kwa karatasi za risiti  zinazofutika maandishi zinazotolewa na Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti (EFDs)  kwa kuwataka wafanyabiashara wote kununua karatasi hizo kwa mawakala waliothibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Mussa Bakari Mbarouk, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu risiti zinazotolewa na Mashine za EFDs kufutika maandishi kwa muda mfupi na muda ambao utatolewa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kurekebisha hali hiyo. Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serika
“Mtu anaogopa kuongea Kiswahili, haya ni maajabu kweli”- JPM

“Mtu anaogopa kuongea Kiswahili, haya ni maajabu kweli”- JPM

Mikoani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa amesikitishwa na Watanzania wanaoona aibu kuongea Kiswahili na kujilazimisha kuongea Kiingereza. Ameyasema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani Meatu mkoani Simiyu na kutolea mfano Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), Jacqueline Mahon ambaye amekuwa akitumia lugha ya Kiswahili. “Uzalendo wetu ni kulinda cha kwetu unaweza ukaona hapa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon, anatoka Ulaya na amekipiga Kiswahili vizuri tu lakini unakuta Mswahili wa Tanzania ambaye anatakiwa kuitangaza lugha yetu anaogopa anataka azungumze Kiingereza,”amesema rais Dkt. Magufuli Aidha, katika mkutano huo, Jacqueline amesema kuwa mikakati ya
error: Content is protected !!