Mikoani

Mbunge wa Mtera ashauri serikali isifanye uchaguzi wa Rais 2020

Mbunge wa Mtera ashauri serikali isifanye uchaguzi wa Rais 2020

Mikoani, Siasa
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde ameshauri Serikali isifanye uchaguzi wa kipengele cha Urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 na badala yake iruhusu uchaguzi uhusishe Wabunge na Madiwani pekee. Akizungumza Bungeni amesema ni kutokana na kwamba Rais John Magufuli hana mpinzani kwa sasa na badala yake fedha ambazo zinatarajiwa kutumika katika uchaguzi huo zitumike katika kujenga nchi. “Kuna faida gani kwenda kupoteza fedha chungu mzima kwa ajili ya uchaguzi Rais ambaye hana mpinzani, tufanye uchaguzi wa Udiwani na Ubunge kwenye Urais tuache na hizo pesa za uchaguzi tumkabidhi Rais zisaidie kuboresha kujenga Nchi,” amesema Lusinde.
Tanzania kupiga marufuku mifuko ya plastiki kuanzia Julai mosi

Tanzania kupiga marufuku mifuko ya plastiki kuanzia Julai mosi

Afya, Jamii, Mikoani
Tanzania iko katika mchakato wa kupiga marufuku utengenezaji, uagizaji, biashara na matumizi ya mifuko ya plastiki, ambapo utekelezaji wake utaanza Julai, 2019, ikiwa ni hatua kabambe kukabiliana na uchafuzi wa mazingira. Tanzania, inaungana na nchi ambazo hivi karibuni zilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki isiyoweza kuoza inapoingia ardhini na ambayo imetajwa na umoja wa mataifa kuwa miongoni mwa changamoto kubwa za mazingira. Kulingana na Umoja wa Mataifa, Kati ya bilioni 9 ya plastiki zinazo tengenezwa kote duniani, asilimia 9 pekee ndio huweza kutumiwa tena na kutokuwa sehemu ya uchafuzi wa mazingira. Tanzania inaungana na nchi zaidi ya 60 ambazo tayari zimetangaza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Nchi nyingine ni China, Ufaransa, Kenya...
Hatimaye bunge la Tanzania lapitisha azimio la kutofanya kazi na CAG, wapinzani wakataa

Hatimaye bunge la Tanzania lapitisha azimio la kutofanya kazi na CAG, wapinzani wakataa

Mikoani, Siasa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Uamuzi huo umepitishwa Jumanne ya leo ikiwa ni baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki,  Maadili na Madaraka ya Bunge,  Emmanuel Mwakasaka kuwasilisha na kusoma bungeni taarifa ya kamati hiyo iliyomuhoji Profesa Mussa Assad,  kumtia hatiani, kwa kile ilichokisema kuwa imebaini kauli aliyoitoa kwamba bunge ni dhaifu,  alilidhalilisha Bunge la nchi hiyo. Katika kikao hicho cha bunge la Tanzania, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alitoa nafasi kwa wabunge kujadili jambo hilo, ambapo wabunge walionekana kutofautiana kimaoni juu ya uamuzi huo, huku wengine wakipinga. Miongoni mwa wabunge walioupinga vikali uamuzi huo ni
error: Content is protected !!