Mikoani

Tanzania ina upungufu madaktari wa macho

Tanzania ina upungufu madaktari wa macho

Afya, Mikoani
TANZANIA ina madaktari bingwa wa macho 55 ambao wanatoa huduma kwa watu zaidi ya milioni 50. Hiyo ni sawa na wastani wa daktari mmoja kwa watu milioni moja, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na wastani wa dunia unaotaka daktari mmoja kuhudumia watu 400,000. Kaimu Rais wa Madaktari wa Macho nchini, Dk. Cyprian Gabriel alisema idadi ya madaktari hao pia ni wale walioko mijini lakini wanakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba wakati vijijini hawana kabisa huduma hizo. Alitoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya ugonjwa wa macho jana jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya macho duniani. “Mheshimiwa mgeni rasmi, tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria, madaktari ni wachache wakati tatizo ni kubwa zaidi vijijini,” alisema. Aidha alisema tatizo la watu wengi kujiita
TRA Yawakamata Watu Wawili Kwa Tuhuma za Kugushi Risiti za EFD Jijini Dar es Salaam.

TRA Yawakamata Watu Wawili Kwa Tuhuma za Kugushi Risiti za EFD Jijini Dar es Salaam.

Biashara & Uchumi, Mikoani
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewakamata watu wawili mwanamke na mwanaume kwa kosa la kugushi Risiti za Kielektroniki za EFD katika maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Richard Kayombo, amesema kuwa, watuhumiwa hao ni Doreen Urassa (40) mkazi wa Kunduchi na Raymond Alexander (31) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni jijini hapa. "Tarehe 4 Oktoba, 2018 majira ya saa 1 jioni, tulifanikiwa kuwakamata watu wawili maeneo ya Sinza Mori wakiwa wanagushi risiti za EFD. Watuhumiwa hawa tutawafikisha mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria", alisema Kayombo. Kayombo ametoa wito kwa watu wote wanaojishughulisha na makosa hayo kuacha mara moja kwa kuwa TRA itaendelea kufanya msako mkali na mt...
NECTA yafuta matokea ya mitihani darasa la saba

NECTA yafuta matokea ya mitihani darasa la saba

Mikoani
Leo Oktoba 2 2018, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini. Miongoni mwa shule zilizokumbana na kadhia hiyo ya kufutwa kwa matokeo hayo ni Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo wilaya ya Chemba, Shule ya Msingi Kisiwani, iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa iliyopoHalmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Alliance na New Alliance zilizopo halmashauri ya Mwanza jiji, Shule za Msingi za halmashauri ...
Ajali ya Moto : Wafanyabiashara wapoteza mali zao Mwanza

Ajali ya Moto : Wafanyabiashara wapoteza mali zao Mwanza

Biashara & Uchumi, Mikoani
SOKO la wafanyabiashara wa nguo na viatu mjini Mwanza, Tanzania, limefungwa Jumamosi kwa muda wa siku mbili baada ya kuteketea kwa moto majira ya saa 10:00 alfajiri . Moto uliounguza soko hilo, maarufu kama Soko la Mlango Mmoja, ambalo liko Kata ya Mbugani, Wilaya ya Nyamagana, unadaiwa kuwa huenda chanzo chake ni majiko yakiwa na moto yaliyo telekezwa katika eneo hilo. Vyanzo vya habari vimesema kuwa soko hilo lina zaidi ya wafanyabiashara 1,000 na linategemewa na wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza. Zaidi ya maduka 150 na vibanda 100 pamoja na mali zilizo kuwamo katika eneo hilo, vimeteketea kwa moto na kusababishia hasara kubwa. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alitembelea soko hilo na kuwaelekeza viongozi wa mitaa na wilaya ya Nyamagana washirikiane na vio...
error: Content is protected !!