Mikoani

Injinia Alphonse Augustino Cherehani: Asimulia vipi alivyopatikana hai siku 3 baada ya kuzama MV Nyerere

Injinia Alphonse Augustino Cherehani: Asimulia vipi alivyopatikana hai siku 3 baada ya kuzama MV Nyerere

Mikoani
Jina la Injinia Augustine Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara. Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika. Injinia ambaye ndiye fundi mkuu wa kivuko hicho kilichopinduka Mwezi wa tisa tarehe 20 mwaka wa 2018 na kuua watu zaidi ya 225, alimsimulia mwandishi wa BBC Eagan Salla mkasa mzima. 'Siku kama siku nyingine' Siku ya tukio Injinia anasema ilkuwa siku kama siku nyingine lakini kwao kwa misingi ya usafirishaji ilikuwa siku ya kazi kubwa kwani ilikuwa ni siku ya gulio eneo la Bugorora. Kawaida...
Anne Makinda: Viongozi bora huanzia skuli

Anne Makinda: Viongozi bora huanzia skuli

Jamii, Mikoani
SPIKA mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, amesema skuli zina jukumu la kuwaandaa vijana, kwani wanafunzi wanaoaminishwa kuwa wanaweza kuwa viongozi bora tangu wakiwa wadogo hujenga tabia ya wao kujilinda na kujichunga wenyewe. Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya skuli ya sekondari Imperial (ISS) yaliyofanyika Msolwa Chalinze mkoani Pwani, alisema skuli zina jukumu hilo ili kuandaa viongozi bora wa baadaye. Makinda ambaye alizindua kampeni maalumu ya skuli hiyo inayotambua mchango wa viongozi mbalimbali katika kuhamasisha uongozi bora, alisifia jitihada za skuli hiyo kwa kutambua wajibu na kuanzisha kampeni hiyo mapema wanafunzi wakiwa skuli. Pamoja na kusifia mandhari nzuri ya skuli hiyo, alisema anaamini viongozi wazuri watatoka skulini hapo na kuwasihi waz...
Tanzia: Mwigizaji mkongwe Tanzania amefariki dunia

Tanzia: Mwigizaji mkongwe Tanzania amefariki dunia

Jamii, Mikoani
Habari za hivi punde Mwigizaji wa siku nyingi Tanzaniani kupitia kundi la KAOLE SANAA GROUP, Ramadhan Mrisho Ditopile maarufu  Mashaka amefariki dunia katika hospitali ya Amana iliyopo Ilala ,Dar Es Salaam  asubuhi ya leo October 20,2018. Mpaka sasa bado haujatajwa ugonjwa uliosababisha kifo cha Ramadhan Mrisho ‘Mashaka’ ingawa inaelezwa kuwa Marehemu alionekana kuzidiwa jana usiku na hivyo kukumbizwa hospitali na ndipo umauti ulipomkuta katika hospitali ya Amana. Marehemu Mashaka aliwahi kuigiza na kuonekana kwenye maigizo mbalimbali ya Kaole yaliyotamba mwanzoni mwa miaka ya 2000..
Mo Dewji arejea nyumbani salama salimini

Mo Dewji arejea nyumbani salama salimini

Biashara & Uchumi, Mikoani
Mfanyabiashara maarufu wa nchini Tanzania aliyetoweka wiki iliyopita, Mohammed Dewji amepatikana na amerejea nyumbani salama salimini: Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dewji amemshukuru Mungu, Watanzania na wote duniani waliomuombea apatikane salama na pia amelishukuru jeshi la polisi la Tanzania kwa kufanya kazi kuhakikisha anapatikana. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam leo Jumamosi, Inspekta Mkuu wa Polisi ya Tanzania Simon Sirro amesema Dewji alitelekezwa na watu waliokuwa ndani ya gari ambalo polisi ililionyesha kwa vyombo vya habari jana Ijumaa. Silaha zapatikana IGP Simon Sirro, Inspekta Mkuu wa Polisi Tanzania (Picha ya Maktaba) Sirro amesema baada ya kutelekezwa ''Mohammed Mo alipata mlinzi mmoja akapiga simu kwa wazazi wake, baadaye ndipo s...
Mvua kubwa kunyesha Novemba 2018, Mikoa 11 yapewa tahadhari

Mvua kubwa kunyesha Novemba 2018, Mikoa 11 yapewa tahadhari

Jamii, Mikoani, Nyumbani, Updates
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi  vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019 katika kanda za magharibi, kati na nyanda za juu kusini. Maeneo yatakayoathirika na mvua hizo za juu ya wastani hadi wastani ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara. Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 18, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema  utabiri huo ni kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. “Katika kipindi cha mvua za msimu hali ya unyevunyevu wa udongo kwa ustawi wa mazao na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi,” amesema. “Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi kama vile mahindi,
error: Content is protected !!