Michezo

Rais wa Liberia George Weah acheza mechi ya kirafiki akiwa miaka 51

Rais wa Liberia George Weah acheza mechi ya kirafiki akiwa miaka 51

Michezo
George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan - akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City Rais wa Liberia George Weah alicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwa nchi yake siku ya Jumanne akiwa na miaka 51. Weah ambaye ni mchezaji wa kwanza wa soka kutoka Afrika kushinda tuzo la mchezaji bora wa Fifa, alicheza dakika 79 kwenye mechi ambapo walishindwa na Nigeria kwa mabao 2-1 nyumbani Monrovia. Liberia ilipanga mechi hiyo ya kirafiki kupumzisha shati namba 14 ambalo lilitumiwa na Weah wakati wa kilele cha taaluma yake. George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan - akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City Mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan, ambaye aliapishwa kuwa Rais mwezi Januari, alishangiliwa wakati akitolewa uwanjani wakati wa mabadiliko. ...
Hassan Mwakinyo: Bondia Mtanzania asema maisha magumu yamechangia ushindi wake

Hassan Mwakinyo: Bondia Mtanzania asema maisha magumu yamechangia ushindi wake

Michezo
Bondia Hassan Mwakinyo aliwashangaza wengi katika ndondi, baada ya kumchapa mpinzani wake Sam Eggington wa Uingereza katika pambano lililochezewa Birmingham. Mwakinyo, anayetokea Tanga, alicheza pambano la mwisho la utangulizi lililokutanisha bondia maarufu wa Uingereza Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas. Siri yake ya kufanikiwa ilikuwa nini? Nassor Rashid, meneja wa bondia huyo, anasema alikuwa na matumaini asilimia 95 kwamba angefanikiwa. Promota huyo anasema video ya ukalimani wake ambayo imesambaa sana mitandao ya kijamii imesaidia sana kumvumisha na kwamba ndoto ya kupambana na kelly Brook na Amir Khan bado ipo, na baadaye Floyd Mayweather.   CHANZO: BBC
Icardi, Dybala kuongeza nguvu dhidi ya Colombia

Icardi, Dybala kuongeza nguvu dhidi ya Colombia

Michezo
Washambuliaji Mauro Icardi na Paulo Dybala wanatarajiwa kuchezesha pamoja katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Colombia utakaochezwa siku ya Jumatano jijini New York, Marekani. Mpango wa wawili hao kuchezeshwa kwa pamoja, umekuja baada ya Mauro Icardi kujiunga na wenzake katika mazoezi ya pamoja kufuatia kupona majeraha ya misuli ya paja, huku Paulo Dybala akimaliza matatizo yake binafsi (matatizo ya kifamilia) na kurejea kambini rasmi. Kocha wa muda wa kikosi cha Argentina Lionel Scaloni anatarajiwa kufanya mabadiliko ya wachezaji wanane, tofauti na alivyokipanga kikosi chake wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Guatemala waliokubali kibano cha mabao matatu kwa sifuri, juma lililopita. Katika mchezo huo, mshambuliaji wa klabu ya Fiorentina Giovanni Simeone alifung...
Malindi yafanya uchaguzi wa viongozi wapya

Malindi yafanya uchaguzi wa viongozi wapya

Michezo
KLABU ya Malindi imefanya uchaguzi mkuu wa kuwachagua viongozi mbali mbali watakaongoza timu hiyo kwa miaka minne ijayo. Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Empire Darajani Mjini Unguja, Mohamed Abdallah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti, Mohammed Masoud Rashid yeye ameshinda kuwa Katibu Mkuu ambapo Amir Saleh amechaguliwa kuwa Mhasibu. Mshika Fedha Mkuu alichaguliwa kuwa Ali Majid na msaidizi Mshika Fedha ameshinda Rajab Said. Wengine walioshinda katika uchaguzi huo ni Jaffar Hussein Babu (Jeff) kuwa Makamu Mwenyekiti ambapo Naibu Katibu ameshinda Sefu Mussa wakati Abdallah Thabit (Dulla Sunday) kuwa Katibu Mwenezi. Waliochaguliwa nafasi ya ujumbe wa Kamati Tendaji ya timu hiyo ni Nassir Seif, Mustafa Ramadhan na Mahmoud Hamza. Akitangaza matokeo hayo msimamizi
error: Content is protected !!