Michezo

Msanii Bongo Fleva akutwa ugangani live bila ya chenga

Msanii Bongo Fleva akutwa ugangani live bila ya chenga

Michezo
Mkali wa muziki wa singeli Dullah Makabila ameonekana akiwa katika mazingira ya ugangani huku picha na videos zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akifanyiwa vitendo vinavyoashiria kuwa ni vya kishirikina. Miezi kadhaa nyuma mkali huyo wa wa singeli aliwahi kuzungumza na kusema kuwa anaamini imani za kishirikina katika kazi za muziki wake ili kufanikiwa na aliongezea kwa kusema kuwa asilimia kubwa ya wasanii nchini wanatumia ushirikina ili wafanikiwe katika muziki. Kutokana na picha hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wamezidi kubaki na viulizo huku wengi wakiamini kuwa huenda akawa anafanya kiki kwaajili ya video ya ngoma yake mpya na wengine wakihisi kuwa ni kweli.     CHANZO: ZANZIBAR 24
Ukosefu wa fedha watajwa kufanya vibaya timu za Pemba

Ukosefu wa fedha watajwa kufanya vibaya timu za Pemba

Michezo
BAADHI ya klabu zilizoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora kutoka Pemba na wadau wa wamesema, moja ya sababu kubwa iliyopelekea timu hizo kufanya vibaya msimu huu ni kutokana na ukosefu wa fedha unaoukabili klabu hizo. Zimesema hivi sasa ligi imekuwa na gharama kubwa, kuanzia maandalizi ya usajili na kuwaweka kambini wachezaji. Waliitaja sababu nyengine ni ukosefu wa udhamini katika ligi hiyo ambao pia ulichangia kwa kiasi kikubwa kwa timu za Pemba kufanya vibaya katika ligi hiyo. Mmoja wa viongozi wa Opec ya Pandani, Ali Omar ‘MECCO’, alisema, timu yao ilishindwa kuhimili mikimikiki ya ligi hiyo, kwa kutokuwa na fedha za kuwaweka wachezaji pamoja kambini. Ukitizama tokea unaanza usajili, fedha nyingi zinahitajika, hujacheza unahitaji fedha, sisi tulikuwa tunatok
Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar Wamtembelea Mwenyekiti wa ZFA Mstaaf Ali Ferej Tamim Nyumbani Kwake Shangani Zanzibar.

Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar Wamtembelea Mwenyekiti wa ZFA Mstaaf Ali Ferej Tamim Nyumbani Kwake Shangani Zanzibar.

Michezo
Katibu wa kamati ya mpito inayosimamia  masuala ya soka visiwani Zanzibar kwa sasa Khamis Abdallah Said akizungumza na aliyekuwa rais wa chama cha mpira wa miguu visiwanibZanzibar Ali Fereji wakati alipotembelea nyumbani kwake pamoja na waandishi mbali mbali wa michezo . Mwenyekiti wa Zamani wa Chama Cha Mpira Zanzibar ZFA Ali Ferej Tamim akizungumza na mwandishi wa habari za Michezo Zanzibar Ndg. Salu Vuai walipofika nyumbani kwake shangani kumtembelea na kumjulia hali yake. Waandishi wa habari za michezo Zanzibar wakimtembelea na kumjulia hali Mwenyekiti Mstaaf wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar ZFA Ali Ferej Tamim walipofika nyumbani kwake shangani Zanzibar.  
Romelu Lukaku: Mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho ‘hawezi kuficha hisia zake’

Romelu Lukaku: Mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho ‘hawezi kuficha hisia zake’

Michezo
Romelu Lukaku alijiunga na United kutoka Everton kwa dau la £75m mwaka 2017 Jose Mourinho hadanganyi na hawezi kuficha hisia zake kama wakufunzi wenzake katika ligi ya Uingereza , kulingana na mshambulijia wa United Romelu Lukaku. Mkufunzi wa United Mourinho alitaka kupewa heshima na vyombo vya habari baada ya kukasirika katika mkutano na wanahabari baada ya timu yake kupoteza 3-0 nyumbani dhidi ya Tottenham mwezi Agosti. Lakini Lukaku anasema kuwa raia huyo wa Ureno ni mtu wa familia , ''huwafanya wachezaji kucheka na anawapigania'' , hivyobasi anahitaji heshima. ''Watu wanajua kwamba ana upande unaomfanya kuwa mshindi'', alisema Lukaku. 'Lakini kile ninachompendea hawezi kuficha hisia zake. Wakati anapokasirika utajua amekasirika, anapofurahi utajua anafurahi''. ''Sijui kw
Rashid Taha ,  mwanamuziki  mwenye asili ya Ageria amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59 mjini Paris nchini Ufaransa

Rashid Taha , mwanamuziki mwenye asili ya Ageria amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59 mjini Paris nchini Ufaransa

Michezo
Rashid Taha ,  mwanamuziki  mwenye asili ya Ageria amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59 mjini Paris nchini Ufaransa Rashid Taha amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59 mjini Paris kwa matatizo ya moyo. Jarida la Le Parisien limetangaza kifo cha mwanamuziki huyo  baada  ya kupata taarifa kutoka kwa familia ya Rashid Taha. Moja miongoni mwa vibao vyake  vilivyompa umashuhuri ni "Ya Rayah", "Abdel Kader" na "Ida". Rashid Taha alikuwa akifahamika katika muziki wa miondoko ya Rai kama Khaled na Faudel Afrika Magharibi. Muziki wa Rai ulichangia  katika harakati za kupigania uhuru  Algeria na ukoloni wa  Ufaransa.
error: Content is protected !!