Michezo

Guaridiola achaguliwa kuwa meneja bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza “EPL” msimu 2018-19

Guaridiola achaguliwa kuwa meneja bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza “EPL” msimu 2018-19

Michezo
Meneja wa Manchester City muhispanyola, Pep Guardiola, atwaa tuzo ya meneja bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza “EPL”. Guardiola anakiongoza kikosi cha City, ambayo imefanikiwa kumaliza ligi ikiwa na alama 98 na kuipiga kikumbao Liverpool kwa kutwaa kombe la ligi hiyomsimu wa 2018-19. Tuzo hiyo ya meneja bora imetolewa na Umoja wa mameneja wa ligi.
Manchester City yakosolewa kwa kuwakejeli mashabiki wa Liverpool

Manchester City yakosolewa kwa kuwakejeli mashabiki wa Liverpool

Michezo
Wimbo wa manchester City unaonyesha mashabiki wa Liverpool ''wakichapwa katika mitaa" na "kulia " Manchester City wamekosolewa juu ya video ya wimbo wao iliyoonyesha wachezaji na wahudumu wa timu hiyo wakiungana katika kuimba wimbo wa kejeli wa kusherehekea mashabiki wa Liverpool "wakichapwa mtaani ". Video hiyo inadhaniwa kuwa ilichukuliwa kutoka kwenye ndege wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka kwenye sherehe za ushindi wa Primia Ligi wa 4-1 katika Brighton. Ushindi huo uliiwezesha the Blues kuichapo Liverpool kwa ushindi mwembaba wa pointi moja. Manchester City bado haijatoa kauli yoyote juu ya video hiyo. Haijabainika wazi ni wachezaji wala wahudumu gani wa klabu hiyo walishiriki katika wimbo huo, ambao unakumbusha kushindw...
Wachezaji wawili wa Ajax ambao ni waislamu raia wa Moroko wafungulia funga zao za Ramadhan wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham

Wachezaji wawili wa Ajax ambao ni waislamu raia wa Moroko wafungulia funga zao za Ramadhan wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham

Jamii, Michezo
Wachezaji wa soka wa timu ya Ajax, Mazraoui na Ziyech, ambao ni waislamu wafungulia funga zao za Ramadhan wakati wa mchezo wa ligi ya mbingwa dhidi ya Tottenham. Ajax ambayo ilifika nusu fainali za ligi ha klabu bingwa Ulaya kwa kuzitoa Real Madrid na Juventus wameshinwa kutamba mbele ya Tottenham. Mchezo huo ulichezwa katika dimba la Amsterdam Arena, Katika mchezo huo wachezaji wa Ajax ambao ni waislamu Noussair Mazraoui na Hakim Ziyech, walifungulia funga zao wakti mchezo ukiendelea. Wachezaji hao wawili raia wa Moroko  walioingia na kikosi cha kwanza, ilipofika dk ya 21 ya mchezo walikwenda katika kona ya uwanja na kufungulia huku kamera za warusha matangazo zikiwamulika. Kwa upande mwingine goli la 2 la Ajax liliwekwa kimiani na Hakim Ziyech mnamo dk 35.
David Beckham apigwa marufuku kuendesha gari

David Beckham apigwa marufuku kuendesha gari

Kimataifa, Michezo
David Beckham amepigwa marufuku kuendesha gari kwa miezi sita baada ya kupatikana akitumia simu wakati akiendesha gari. Kapteni huyo wa zamani wa England amekiri makosa. Mahakama imearifiwa amepigwa picha na raia akiwa ameshikilia simu wakati akiendesha gari lake aina ya Bentley 'taratibu' katika foleni. Beckham, mwenye umri 44, ametozwa faini ya £750, ameagizwa alipe £100 gharama ya kesi na malipo ya ziada ya £75 katika siku saba zijazo. Jaji katika mahakama hiyo amemuambia hata kama kasi ya gari ilikuwa taratibu kwenye foleni 'hakuna kisingizio' chini ya sheria. Mwendesha mashtaka amesema: "Badala ya kutazama mbele na kuangalia barabara alionekana akitazama mapajani mwake.' Wakili wa Beckham Gerrard Tyrrell amesema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester Unite
Tottenham waifuata Liverpool fainali za Klabu bingwa Ulaya

Tottenham waifuata Liverpool fainali za Klabu bingwa Ulaya

Michezo
Historia nyingine imeandikwa katika ligi ya mabingwa barani Ulaya. Baada ya Liverpool, Tottenham ambayo ilikuwa nyuma kwa goli 2-0 katika mchezo wake dhidi ya Ajax, yatoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-2 na kutinga fainali za klabu bingwa barani Ulaya. Mchezo huo wa marudio ulichezwa katika dimba la Johan Cruyff Arena jijini Amsterdam Mchezo huo ulioanza kwa kasi, Ajax iliyokuwa ikicheza uwanja wa nyumbani mnamo dk 5 tu ya mchezo kupitia kwa  Matthijs iliandika bao la kwanza na dk ya 35 iliandika goli la 2 kupitia kwa Hakim Ziyech.  Kipindi cha kwanza kilimalizika matokeo yakiwa 2-0. Kipindi cha pili kilitawaliwa na Tottenham, ambayo ilikuwa ikicheza ugenini. Lucas Moura ndiye aliyeitoa kimasomaso spurs kwa kufunga magoli yote matatu dk 55, 59...
error: Content is protected !!