Michezo

Ndege yenye Nembo ya Azam FC yazua gumzo, Meneja afunguka ukweli ulivyo

Ndege yenye Nembo ya Azam FC yazua gumzo, Meneja afunguka ukweli ulivyo

Biashara & Uchumi, Michezo, Mikoani
Kitendo cha wachezaji wa Azam FC kuonekana wakiwa wameteremka katika ndege yenye nembo ya Azam kimezua gumzo takribani wiki nzima huku watu wengi wakisema Azam FC sasa imepiga hatua hadi ya kumiliki ndege. Meneja wa Azam FC, Philipo Alando, hatimaye amefunguka juu ya suala hilo kwa kusema kuwa ndege hiyo siyo mali ya timu bali ni mali ya Makampuni ya SSB. Azam juzi ilikwenda kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kuvaana na Kagera Sugar ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Alando amesema kuwa watu wamezungumza mengi sana juu ya ndege hiyo lakini ukweli ni kwamba hiyo ndege siyo mali ya timu bali ni mali ya kampuni ya SSB ambayo ndiyo kampuni mama. “Hiyo ndege haina uwezo wa kubeba timu nzima hivyo inabeba abiria 13 tu, kwa sababu ni mali ya kampuni kwa ajili ya
Mafunzo ya Karati kufanyika leo

Mafunzo ya Karati kufanyika leo

Michezo, Nyumbani
CHAMA cha mchezo wa karati ‘Shotkani’ kinatarajia kutoa mafunzo ya siku mbili kwa wachezaji wa mchezo huo yatakayoanza leo. Akizungumza na gazeti hili mwenyekiti wa chama hicho Abdalla Hussein Rashid alisema kuwa mafunzo hayo yataenda sambamba na utoaji wa vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo hivi karibuni yataendeshwa na mkufunzi kutoka Switzerland Sesnse Andreas. Alisema kuwa mafunzo hayo yatashirikisha jinsia tofauti ambao watajifunza mbinu mbali mbali za mchezo wao wa karate ikiwemo mianguko, kujiamini na kujikinga kupitia mchezo huo. “Tupo katika jitihada mbali mbali za kuuendeleza mchezo huu, na leo tutapokea mgeni huyo ambae anakuja kwa nia na madhumuni ya kuendeleza ushirikiano wao katika masuala haya ya karate hapa Zanzibar”, alisema. Alisema kwamba kufanyika kw
Kikosi cha Zanzibar Heroes U-20 Chatangazwa

Kikosi cha Zanzibar Heroes U-20 Chatangazwa

Michezo
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Salum Ali Haji, ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 38, kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Cecafa ya Vijana yanayotarajiwa kufanyika Uganda Disemba 15-25, 2018 . Kocha Salum ametangaza kikosi hicho kwenye Ukumbi wa uwanja wa Amaan , katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mchana wa leo. Walioitwa kuunda kikosi hicho upande wa Makipa yupo, Peter Dotto Mashauri (Black Sailors), Abdulattif Said Masoud (Jamhuri), Mwinyi Ali Mwinyi (Mapembeani) na Yakoub Suleiman (Muembeladu). Mabeki: Khalid Khamis (Simba FC ya Zanzibar), Abdul hamid Ramadhan (Villa Fc), Abdulhakim Khamis Faki (Sporting FC), Abubakar Suleiman (ZFDC), Mudathir Nassor (New Afrika), Salum Suleiman (Kimbunga Fc) Ahmada Kham...
Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya walemavu ya Uturuki yatinga Fainali za kombe la dunia

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya walemavu ya Uturuki yatinga Fainali za kombe la dunia

Jamii, Kimataifa, Michezo
Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya walemavu ya Uturuki ambao pia ni mabingwa wa Ulaya wameandika historia baada ya Kutinga fainali za kombe la dunia za walemavu zinazofanyika nchini Mexiko. Katika mchezo wa nusu fainali ilikipiga na timu ya Mexiko ambao ni wenyeji wa mashindano hayo na pia walimaliza nafasi ya kwanza mzunguko wa makundi. Robo fainali walicheza na Urusi ambao ndio mabingwa watetezi na kufanikiwa kuwachabanga magoli 5-1. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan aliwapigia simu wachezaji hao kabla ya mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Mexiko na kuwapongeza kwa hatua waliyofikia na pia kuwatakia mafanikio. Katika mchezo huo wa nusu fainali timu hiyo ya taifa ilifanikwa kuwafurusha nje ya mashindano wenyeji hao wa mashindano Mexiko kwa magoli 4-0, na hivyo wao kutinga
error: Content is protected !!