Michezo

Mchezaji bora wa soka wa mwaka nchini Uingereza

Mchezaji bora wa soka wa mwaka nchini Uingereza

Kimataifa, Michezo
Shirikisho la wachezaji wa soka La kulipwa nchini Uingereza (PFA) limetangaza majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka nchini humo. Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo imetaja wachezaji hao kuwa ni Sergio Aguero, Raheem Sterling na Bernardo Silva kutoka Manchester City,  Virgil van Dijk na Sadio Mane kutokea Liverpool na mwingine ni Eden Hazard kutokea Chelsea. Mchezaji bora wa msimu uliopita Muhammed Salah Mmisri anayechezea Liverpool msimu huu sio miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo Mchezaji atakayeshinda atatunukiwa tuzo hiyo katika hafla itayofanyika jijini London mnamo April 28.
Wimbo wa Takataka wapigwa marufuku Kenya

Wimbo wa Takataka wapigwa marufuku Kenya

Kimataifa, Michezo
Ezekiel Mutua ( kulia) amesema Takataka umeimbwa kwa lugha katili na unawafanya wanawake kuonekana kama vifaa na kuhimiza wanaume wawaumize Mamlaka nchini Kenya zimepiga marufuku kuchezwa kwa wimbo Takataka, unaosemwa kuwa unawatusi wanawake. Bodi ya kudhibiti filamu nchini Kenya imezuwia mara moja wimbo Takataka- ulioimbwa na msanii Alvin almaarufu Alvindo uliozalishwa na kampuni ya FastCash Music Group. Mkurugenzi wa Bodi ya udhibiti wa viwango vya filamu nchini Ezekiel Mutua aliuelezea wimbo huo kama wenye wakishamba na wenye matusi na kuongeza kuwa " kama watu wanaowajibika hatuwezi kuukubali ." " Wimbo Takataka umeimbwa kwa lugha katili unaowafanya wanawake kuwa kama vifaa na kuhimiza wanaume waumizwe kuumizwa na wanaume ," al...
Evarton yaichapa Arsenal, Yafikisha alama 43 na kujikita nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi

Evarton yaichapa Arsenal, Yafikisha alama 43 na kujikita nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi

Michezo
Wiki ya 33 ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza, Premier league, imeendelea kwa michezo kati ya Evarton na Arsenal. Mchezo uliopigwa katika dimba la Goodison Park. Evarton wakicheza uwanja wa nyumbani walifanikiwa kupata ushindi wa golli 1-0. Goli ambalo lilipatikana dk ya 10 kupitia kwa  Phil Jagielka. Evarton ambayo inasinda mechi yake ya 3 mfufulizo imefikisha alama 46 na kujikita nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi. Arsenal kwa upande wake ina alama 63 ikiwa nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi.
Udhamini unahitajika kwa maendeleo ya soka Zanzibar

Udhamini unahitajika kwa maendeleo ya soka Zanzibar

Michezo
HUKU Ligi Kuu ya Zanzibar ikiendelea kuchanja mbuga kuelekea ukingoni, klabu zimeendelea kupaza kilio chao cha kukosekana kwa udhamini kwenye ligi hiyo kubwa nchini. Huko nyuma, tuliwahi kuchapisha habari juu ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), namna kinavyohitajika kutafuta wadhamini ili kukuza ushindani na kuzipunguzia mzigo wa gharama klabu zinazoshiriki ligi hiyo. Zanzibar Leo kama wadau wa michezo tunaungana na klabu hizo na ZFA kwa ujumla katika kuona udhamini unapatikana kwa ajili ya kuhakisha ligi inakuwa ya ushindani ili kutoa wawakilishi bora wa kimataifa. Ni ukweli usiopingika kuwa ZFA inapita kwenye kipindi kigumu cha kusimamia ligi hiyo kutokana na kutokuwepo kwa mdhamini rasmi na hivyo kuzifanya klabu kubeba mzigo mzito wa ushiriki wao. Kama inavyoelewe...
Magoli bora katika historia ya Barcelona FC

Magoli bora katika historia ya Barcelona FC

Kimataifa, Michezo
Barcelona timu ya mpira wa miguu ya ligi kuu ya Uhispania (La Liga) imeendesha kura ya kuchagua  magoli bora yaliyowahi kufungwa na timu hiyo. Kura hiyo iliyoendeshwa kupitia mtandao wa Twitter ilihusisha wapiga  wapenzi wa mpira kura laki 5 kutoka mataifa 160. Magoli yaliofungwa na Lionel Messi yalishika nafasi za juu. Magoli 63 yalishindanishwa katika kura hizo. Nafasi 3 za kwanza katika matokeo ya kura hio zilichukuliwa na nyota wa Arjentina, Lionel Messi. Goli alilofunga Messi katika mchezo baina ya Barcelona na Getafe, Nusu fainali ya kombe la mfalme, msimu wa 2006-07  ndilo limeshika nafasi ya kwanza kwa kupata kura asilimia 45. Goli hilo Messi alilifunga baada ya kutoka na mpira toka katikati ya uwanja na kuwalamba chenga wachezaji kadhaa wa timu...
error: Content is protected !!