Kimataifa

Maziko ya Kofi Annan yahudhuriwa na viongozi wa kimataifa Ghana

Maziko ya Kofi Annan yahudhuriwa na viongozi wa kimataifa Ghana

Kimataifa
Wanajeshi wanaobeba jeneza kwa kulipa heshima stahiki wakiwa pembeni ya jeneza la Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan aliyeaga dunia huko Uswitz, kabla ya maziko ya kitaifa, ukiwa eneo la Uwanja wa ndege wa Jubilee Accra, Ghana. Raia wa Ghana wameendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan, wakati maandalizi ya kumzika Alhamisi yakiwa yamekwisha kamilika. Mwili wake Annan umewekwa kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Accra ambapo ibada ya kumuaga inafanyika kabla ya kuzikwa Alhamisi. Wageni waheshimiwa kutoka kote duniani wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo. Kati yao akiwemo Katibu Mkuu wa UN wa sasa Antonio Gutterrez na Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast. Vyombo vya habari nchini G...
Kimbunga Florence chatolewa tahadhari Marekani

Kimbunga Florence chatolewa tahadhari Marekani

Kimataifa
Wafanyakazi wakiweka vifaa vyenye nguvu kwenye madirisha ya duka huko Wilmington, Carolina Kusini kabla ya kuwasili kwa kimbunga Florence.REUTERS NEWYORK, MAREKANI RAIS wa Marekani  Donald Trump ametangaza hali ya hatari katika maeneo ya Kaskazini na kusini mwa jimbo la Carolina ambapo pia eneo kubwa la Washington DC limechukua pia tahadhari kufuatia kimbunga Florence. Takribani watu milioni 1.7 wanayahama maeneo yao kwa hiari na wengine kwa amri maalumu ili kuepuka madhara ya kimbunga hicho. Kimbunga hicho kinasafiri kwa kilomita 195 kwa saa,huku mawimbi yake yakienda juu kimo cha mita 25. Kimbunga Florence kinachotajwa kibaya kuwahi kutokea siku ya ijumaa 9leo) kinatarajiwa kuyapiga maeneo ya pwani ya mashariki. Kwa mujibu wa chanzo cha usalama nchini Marekani kwa sasa ku
Watu 6 wameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga mjini Mogadishu

Watu 6 wameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga mjini Mogadishu

Kimataifa
Watu 6 wameripotiwa kufariki na wengine 16 kujeruhiwa katika  shambulizi  la kujitoa muhanga lililoteka mjini Mogadishu nchini Somalia. Shambulizi hilo la kujitoa muhanga limetekelezwa na mtu mmoja aliekuwa katika  gari lililokuwa limeshhehni vilipuzi. Shambulizi hilo limelenga  ofisi za ktangoji cha Hodan. Mlipuko uliotokea  katika tukio hilo umeathiri kwa kiasi kikubwa  majengo karibu na eneo la tukio. Wanamgambo wa kundi la al Shabaab wanashukiwa kuhusika na shambulizi hilo.
UN yaorodhesha mataifa 38 yanayo “aibisha” duniani

UN yaorodhesha mataifa 38 yanayo “aibisha” duniani

Kimataifa
Umoja wa Mataifa Jumatano umetaja mataifa 38 "yanayo aibisha" yakiwemo China na Russia kwa kile walichodai kuwa ni ulipizaji kisasi au vitisho dhidi ya wale wanaoshirikiana na umoja huo kwa ajili ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu. Miongoni mwa unyanyasaji ulotajwa ni pamoja na mauaji, mateso na kukamatwa kiholela kwa watu hao. Ripoti ya kila mwaka iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres imetaja pia kuwepo na kampeni kuwafuatilia, kuwatendea maovu, na kuwaaibisha hadharani watetezi wa haki za binadam na waathiriwa. Mataifa hayo 38 yanajumuisha 29 yenye kesi mpya na mengine 19 yakikabiliwa na kesi zinazoendelea. Ripoti inaeleza kwamba mataifa mengi yanadaiwa kuwafungulia mashtaka wanaharakati wa haki za binadamu kwa ugaidi au kushirikiana na matai...
Viongozi wa Asia wakosoa sera za Trump

Viongozi wa Asia wakosoa sera za Trump

Biashara & Uchumi, Kimataifa
Rais wa Russia Vladimir Putin (kulia) na Rais wa China Xi Jinping (kushoto) wakipika wakati wa ziara yao ya mkutano wa kiuchumi wa nchi za Asia Mashariki EEF) katika maonyesho yanayoendelea pembeni huko mjini Vladivostok, Russia Septemba11, 2018. Viongozi wa nchi za Asia Mashariki wanao hudhuria mkutano wao wa Kiuchumi, EEF, mjini Vladivostok , Rashia, Jumatano, wamekosoa vikali mtindo wa sera ya Rais Trump wa Marekani ya kufunga masoko yao na kueleza ni hatari kubwa kwa uchumi wa Dunia. Viongozi hao pia wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao. Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mkutano huo wa tatu unaohudhuriwa pia na Rais wa China Xi Jingping na Waziri Mkuu wa Japan Shinto Abe, Rais wa Rashia Vladimir Putin amesema kuendelea kw...
error: Content is protected !!