Kimataifa

Bobi Wine kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu Uganda

Bobi Wine kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu Uganda

Kimataifa, Siasa
Bobi Wine kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Uganda mwaka 2021. Kyagulanyi Ssentamu  mwanamuziki nyota nchini Uganda na Afrika Mashariki ambae amejipatia umashuhuri wake katika dimba la siasa, katika mahojiano aliofanya na kituo cha habari cha “The Associated Press” amesema kuwa anataraji  kumenyana na rais Museveni katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Uganda mwaka 2021. Bobi wine amesema kuwa "I will challenge President Museveni on behalf of the people," katika mahojiano na  The Associated Press  Jumatatu.

Ni kwanini viongozi wa makampuni ya kamari kenya wamefurushwa?

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa, Teknolojia
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i ametia saini agizo la kuwarejesha makwao wakurugenzi 17 wa kigeni wa makampuni ya michezo ya kamari. Agizo hilo limetekelezwa moja kwa moja, kwa mujibu wa ofisi ya rais. Baadhi ya wakurugenzi hao walianza kuondoka jana kurejea makwao baada ya kushikiliwa kwa muda wa saa kadhaa kufuatia kusainiwa kwa agizo la Waziri wa mambo ya nje, yameripoti magazeti nchini humo. Uamuzi wa kuwaondosha nchini ulifikiwa baada ya Kamati ya ushauri wa masula la kiusalama nchini Kenya (NSAC), ulioafikiwa na rais Uhuru Kenyatta, kuamua kuanzisha vita dhidi ya makampuni ya kamari. Wengi miongoni mwa wakurugenzi wa makampuni waliofurushwa ni raia kutoka mataifa ya Ulaya yakiwemo Bulgaria, Italia, Urusi na Poland. Hata hivyo Wi...
Maelfu waandamana Uturuki kuilaani Marekani, Israel

Maelfu waandamana Uturuki kuilaani Marekani, Israel

Jamii, Kimataifa, Siasa
Maelfu wa wananchi wa mji wa Adana wa kusini mwa Uturuki wamefanya maandamano ya kuilaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, waandamanaji hayo walikuwa wanapiga mayowe ya kuilaani Marekani na utawala wa Kizayuni na kusema kuwa tawala hizo ndio wahusika wakuu wa jaribio la mapinduzi ya kijeshi la tarehe 15 Julai 2016 nchini Uturuki. Waandamanaji hao wameitaka serikali ya Ankara kufunga kambi za kijeshi za NATO nchini mwao hasa kambi ya jeshi la anga ya Incirlik ambayo ilisaidia jaribio hilo lililofeli la mapinduzi. Serikali ya Uturuki inaamini kuwa, Fethullah Gülen na wafuasi wake waliopandikizwa katika taasisi za mahakama, jeshini, taasisi za kielimu na kwenye asasi nyingine za se
Trump amekana shutuma dhidi yake kuwa yeye ni mbaguzi

Trump amekana shutuma dhidi yake kuwa yeye ni mbaguzi

Jamii, Kimataifa, Siasa
Raisi wa Marekani, Donald Trump amesisitiza kuwa yeye si mbaguzi baada ya mashambulizi yake kupitia Twitter dhidi ya wabunge wanne wanawake kukemewa vikali. Katika ukurasa wa Twitter aliwataka wanawake hao wasio na asili ya Marekani, ''kuondoka'' kuelekea kwenye nchi zao walipotoka. Kitendo hicho kiliamsha ghadhabu, alikataa shutuma kuwa yeye ni mbaguzi: ''sina asili ya ubaguzi mwilini mwangu!''. Bunge la wawakilishi linajiandaa kupigia kura makubaliano ya pamoja ya kukemea kauli zake, huku hatua hiyo ikitegemewa kupita kutokana na kuwepo wawakilishi wengi wa Democrats. Awali, wabunge Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley na Rashida Tlaib walitangaza kupuuza matamshi ya Trump wakidai yanalenga kuwaondoa kwenye mstari. Wabunge hao waliwataka watu n...
Iran yaisaidia meli ya mafuta ya kigeni baada ya kuombwa msaada Ghuba ya Uajemi

Iran yaisaidia meli ya mafuta ya kigeni baada ya kuombwa msaada Ghuba ya Uajemi

Kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jana usiku meli moja ya kigeni ya mafuta iliomba msaada wa Iran baada ya kukumbwa na matatizo ya kiufundi katika eneo la Ghuba ya Uajemi, na askari wa Iran waliitikia haraka ombi hilo. Sayyid Abbas Mousavi ametoa tamko hilo baada ya kuenea habari za kutatanisha kuhusu kushikiliwa meli ya mafuta ya Imarati katika maji ya Iran kwenye eneo la Ghuba ya Uajemi. Sayyid Mousavi amesema, meli moja ya mafuta ya kigeni jana usiku ilikumbwa na matatizo ya kiufundi na iliomba msaada wa Iran. Iran nayo ikatekeleze jukumu lake kwa mujibu wa sheria za kimataifa kwa kutuma chombo cha kuiburuta meli hiyo hadi kwenye maji ya Iran kwa ajili ya matengenezo. Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran am...
error: Content is protected !!