Kimataifa

Papa Francis, Viongozi Kanisa Katoliki Marekani kujadili kashfa ya ngono

Papa Francis, Viongozi Kanisa Katoliki Marekani kujadili kashfa ya ngono

Jamii, Kimataifa
Papa Francis anatarajiwa kukutana Alhamisi na viongozi wa Kanisa Katoliki la Marekani, kuzungumzia kashfa ya ngono iliyo likumba kanisa hilo nchini Marekani, na vitendo vya kuficha madai hayo yaliyotolewa kwa miaka mingi dhidi ya mamia ya mapadri. Mkutano huo na Papa Francis unafanyika wakati ambapo kumekuwa na wito wa balozi mstaafu wa Vatican nchini Marekani (Askofu Mkuu Carlo Maria Vigano) ukimtaka papa aachie madaraka. Anadai kuwa kuwa papa alikuwa anajua kwa miaka mingi iliyopita juu ya ukweli wa taarifa ya kuwa Askofu Mkuu Theodore McCarrick wa Washington alikuwa amemnyanyasa kijana ambaye ni mtumishi wa altare mwaka 1970 na wanafunzi wengine wanao somea upadri na mapadri vijana, lakini hakuthubutu kumkabili juu ya madai hayo. Pope Francis alimuondoa McCarrick ...
Junker: Ushirikiano mpya wa AU na EU kubuni nafasi milioni 10 za ajira

Junker: Ushirikiano mpya wa AU na EU kubuni nafasi milioni 10 za ajira

Biashara & Uchumi, Kimataifa
Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya amesema EU inapania kuzindua ushirikiano mpya kati yake na Umoja wa Afrika utakaosababisha kubuniwa mamilioni ya nafasi za ajira. Katika hotuba yake ya kila mwaka katika Bunge la Umoja wa Ulaya hii leo, Jean-Claude Juncker amesema umoja huo unaandaa fremu ya kuvutia uwekezaji mkubwa barani Afrika. Amesema, "Hii leo, tunapendekeza kuundwa muungano mpya, utakaohakikisha kuwa kuna mchakato endelevu wa kustawishwa uwekezaji na kubuniwa nafasi za ajira baina ya Afrika na Ulaya, mkakati ambao utapelekea kuundwa nafasi milioni 10 za ajira barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo pekee." Amebainisha kuwa, "Afrika haihitaji tena misaada, bali inahitaji ushirikiano wa kweli na uadilifu, na sisi Ulaya tunahitaji mshirika wa namna hii pia." Wa
Rais Rouhani: Hivi sasa Marekani iko katika hali mbaya sana duniani

Rais Rouhani: Hivi sasa Marekani iko katika hali mbaya sana duniani

Kimataifa
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba ukiachilia nchi na tawala chache zinazojulikana katika eneo la Mashariki ya Kati ambazo ziko pamoja na Washington, Marekani iko katika hali mbaya zaidi duniani. Rais Rouhani ameyasema hayo Jumatano ya leo katika kikao cha serikali na kuongeza kuwa, hii leo waitifaki wa Marekani hawako pamoja na nchi hiyo na kwamba hata marafiki wake wa zamani na wa jadi nao wamejitenga na kujifakharisha kuwa mbali na nchi hiyo ya kibeberu. Aidha Rais wa Iran amefafanua kuwa, hata asasi za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), haziko pamoja na siasa za Marekani. Rai
Sarraj: Uchaguzi hauwezi kufanyika Libya katika mazingira ya sasa

Sarraj: Uchaguzi hauwezi kufanyika Libya katika mazingira ya sasa

Kimataifa
Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amesema ni muhali kufanyika uchaguzi nchini humo katika mazingira ya hivi sasa. Fayez al Sarraj ameyasema hayo leo Jumatano katika mahojiano na gazeti la Italia la Corriere della Sera na kuongeza kuwa, "Hatuwezi kupiga kura wakati huu ambapo kuna ukosefu wa usalama wa uthabiti mitaani, ni sharti uchaguzi ufanyike katika mazingira ambayo matokeo yake yatakubaliwa na kila mtu." Ingawaje huko nyuma alitangaza kuunga mkono juhudi za kisiasa za kutatua mgogoro wa nchi yake kupitia uchaguzi wa rais na bunge, lakini kauli yake mpya inatilia shaka uwezekano wa kufanyika uchaguzi huo kabla ya kumalizika mwaka huu. Sarraj (kushoto), Macron na Khalifa Haftar Sarraj pamoja na hasimu wake Khalifa Haftar, Kamanda Mkuu wa Jeshi mashariki mwa
Basi labingiria bondeni na kuua watu 43 nchini India

Basi labingiria bondeni na kuua watu 43 nchini India

Kimataifa
Kwa akali watu 43 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kubingiria kwenye bonde, katika wilaya ya Jagtial kusini mwa India. Duru za habari zimeripoti kwamba, basi hilo lilikuwa limebeba abiria 55 waliokuwa wametoka hekaluni katika matambiko ya kidini, katika eneo la milima lililoko kwenye jimbo la Telangana kusini mwa nchi mapema leo, kabla ya kupoteza muelekeo na kubingira bondeni. Mashuhuda wanasema dereva wa basi hilo lililokuwa likitokea eneo la hekalu la Anjaneya Swamy katika wilaya ya Jagtial alipoteza muelekeo alipojaribu kukwepa kugongana ana kwa ana na basi jingine katika eneo hilo lenye shughuli nyingi. Baadhi ya majeruhi hata hivyo wanasema dereva huyo alikuwa akiliendesha basi hilo kwa mwendo wa kasi ndiposa akapoteza muelekeo. Ind
error: Content is protected !!