Kimataifa

Imran Khan kupiga mnada leo magari ya kifahari ya ofisi ya waziri mkuu, Pakistan

Imran Khan kupiga mnada leo magari ya kifahari ya ofisi ya waziri mkuu, Pakistan

Kimataifa
Magari ya kifahari ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistan yanapigwa mnada hii leo kwa lengo la kutafuta fedha kwa maslahi ya umma. Ripoti zinaeleza kuwa miongoni mwa magari yanayopigwa mnada ni magari 102 kati ya magari 200 ya kifahari ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo.  Chama cha Tehreek-e-Insaf kinachoongozwa na waziri mkuu huyo kimetangaza kwamba, fedha zote zitakazopatikana katika mnada huo wa magari zitatumiwa katika maslahi makuu ya umma nchini. Imran Khan, Waziri Mkuu Mpya wa Pakistan ambaye ameamua kuishi maisha ya kawaida yasiyo ya kifahari Katika hatua nyingine, ni kwamba hivi karibuni Ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistan inatarajiwa kubadilishwa kuwa Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Intelejensia. Kuishi maisha ya kawaida ni moja ya nara muhimu za serikali ya Imran Khan. Inaelezwa
Kaka wa Mfalme Salman wa Saudia, atoroka nchi akilalamikia siasa za Mohammad Bin Salman

Kaka wa Mfalme Salman wa Saudia, atoroka nchi akilalamikia siasa za Mohammad Bin Salman

Kimataifa, Siasa
Kaka wa Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia na katika kulalamikia siasa za kigeni za mfalme huyo na Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo na uingiliaji wake katika vita vya Yemen, ameamua kuondoka Saudia sambamba na kuwaondoa watu wa familia yake kutoka ardhi ya nchi hiyo. Hivi karibuni Ahmed bin Abdulaziz Al Saud ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Njdani alionekana wazi akiandamana pamoja na watu kadhaa mjini Longon, Uingereza wakilaani siasa za kigeni zinazotekelezwa na Mfalme Salman bin Abdulaziz pamoja na mwanaye Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo na kadhalika nafasi yao katika kuishambulia kijeshi Yemen. Inaelezwa kuwa, matamshi ya ukosoaji wa mwanamfalme huyo wa Saudia yaliibua hasira kali ya Mfalme Sal
Mvua na upepo mkali vyasababisha vifo vya watu zaidi ya 40 nchini Ufilipino

Mvua na upepo mkali vyasababisha vifo vya watu zaidi ya 40 nchini Ufilipino

Kimataifa
Mvua na dhuruba kali ya upepo vyasababisha vifo vya watu 40 Jumapili  nchini Ufilipino. Miongoni wa jeshi la Polisi Oscar Albayalde  amesema kuwa watu wengi wamefariki  kutokana na maporomoko ya ardhi. Watu zaidi ya  laki moja wameondolewa katika maeneo hatari  na kuwekwa katika mahali salama. Upepo huo ulikuwa na mwendo wa kilomita 100 kwa saa. Upepo huo umejielekeza  Kusini mwa  China na Hong Kong.
Magaidi kadhaa wa Boko Haram wauliwa na jeshi la Nigeria, Borno

Magaidi kadhaa wa Boko Haram wauliwa na jeshi la Nigeria, Borno

Kimataifa
Wanachama kadhaa wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram wameuawa katika operesheni iliyofanywa jana Jumapili na wanajeshi wa Nigeria katika jimbo la Borno, la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Katika taarifa yake, jeshi la Nigeria bila ya kutaja idadi kamili limesema "Kikosi cha 222 cha jeshi letu kimepambana na wanachama wa Boko Haram mjini Maiduguri, karibu na eneo la Bama na magaidi kadhaa wameuawa na wengine wamefanikiwa kutoroka wakiwa na majeraha ya risasi." Picha zilizosambazwa na jeshi la Nigeria katika mtandao wa kijamii wa Twitter zinaonesha miili ya magaidi hao ikiwa imerundikana kandokando ya barabara. Operesheni ya Upinde Kadhalika silaha kadhaa za magaidi hao wakufurishaji zimepatikana katika operesheni hiyo iliyopewa jina la Upin...
Wakazi wa mji mkuu wa Libya, Tripoli walalamikia hali mbaya ya usalama

Wakazi wa mji mkuu wa Libya, Tripoli walalamikia hali mbaya ya usalama

Kimataifa
Wakazi wa mji mkuu wa Libya, Tripoli jana walifanya maandamano wakilalamikia hali mbaya ya usalama katika mji huo mkuu na kutaka kuboreshwa hali ya maisha nchini humo. Wafanya maandamano hao ambao walikuwa wakipiga nara dhidi ya serikali wamesisitiza kuwa wananchi wa Libya wanakabiliwa na maafa na masaibu mengi na kwamba serikali pia imeshindwa kupunguza mashinikizo yanayowakabili wananchi. Wakazi hao wa Tripoli wametaka kuvunjwa bunge, serikali ya umoja wa kitaifa na baraza la uongozi la nchi hiyo. Aidha wametaka kulindwa raia huko Tripoli na kufurushwa wanamgambo wenye silaha katika mji mkuu huo. Waandamanaji aidha wametaka kuundwa jeshi na polisi yenye nguvu huko Libya ili kuinusuru nchi na makundi yenye silaha. Libya ina serikali mbili kufuatia upinzani wa kisiasa ulioko nchin...
error: Content is protected !!