Kimataifa

Wakurdi wa Iraq wateremka vituoni kulichagua bunge jipya

Wakurdi wa Iraq wateremka vituoni kulichagua bunge jipya

Kimataifa, Siasa
Wakurd wa Iraq, wanateremka vituoni katika jimbo lenye utawala wa ndani la kaskazini kulichagua bunge jipya, mwaka mmoja baada ya kura ya maoni ya kutaka kuwa huru iliyoikasirisha serikali kuu ya Iraq mjini Baghdad. Matokeo yanatarajiwa kutangazwa masaa 72 baadae. Wadadisi wanasema matokeo hayo yatashawishi zoezi la kuchaguliwa rais wa shirikisho na bunge la nchi hiyo kesho jumatatu mjini Baghdad, wadhifa ambao kijadi hudhibitiwa na Mkurd. Hadi saa 12 jioni, wapiga kura milioni tatu na laki moja watawachagua wabunge 111 kati ya wagombea 673 wanaowakilisha vyama 29 vya kisiasa- viti 11 vinatengwa kwaajili ya jamii za wachache na za kidini za Waturkmenia, Wakristo na Waarmenia. Jimbo la kaskazini mwa Iraq wanakoishi jamii kubwa ya Wakurd lina mikoa mitatu na limejipatia utawala ...
Waziri mkuu wa jimbo India atangaza mpango wa kuwa na wizara ya ng’ombe

Waziri mkuu wa jimbo India atangaza mpango wa kuwa na wizara ya ng’ombe

Jamii, Kimataifa
Serikali ya jimbo moja katikati mwa India imetangaza mpango wa kuanzisha wizara ya masuala ya ng'ombe. Waziri mkuu wa jimbo la Madhya Pradesh Shivraj Singh Chouhan amesema hatua hiyo itachangia kuongezwa kwa fedha za kusaidia uhifadhi wa ng'ombe. Taarifa zinasema Bw Chouhan, ambaye ni wa chama cha BJP, amechukua hatua hiyo kama moja ya njia za kujaribu kumzidi mgombea wa chama cha upinzani cha Congress kila mmoja akijaribu kuwavutia wapiga kura wanaowathamini sana ng'ombe. Alitoa tangazo hilo siku chache baada ya kiongozi wa chama cha Congress katika jimbo hilo Kamal Nath kuahidi kuanzisha makao ya kutoa hifadhi kwa ng'ombe iwapo chama chake kitashinda uchaguzi. Amesema amesikitishwa sana na vifo vya ng'ombe ambao mara kwa mara hugongwa na magari wakivuka barabara katika jimbo ...
Ahukumiwa kifungo cha miezi mitatu kwa kukashifu Uislamu katika mitandao ya kijamii Uswidi

Ahukumiwa kifungo cha miezi mitatu kwa kukashifu Uislamu katika mitandao ya kijamii Uswidi

Jamii, Kimataifa
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 ahukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu gerezani kwa kosa la kukashifu uislamu katika mitandao ya kijamii. Tukio hilo limetokea  Jönköping nchini Uswidi. Taarifa zilizotolewa na kituo cha runinga cha SVT nchini Uswidi zimefahamisha kuwa mwanamke huyo amehukumiwa adhabu hiyo kwa kosa la kukashifu uislamu katika  ukurasa wake wa Facebook. Mwanamke huyo ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa fikra za  waislamu ni fikra za kale.  
Watu 384 wapoteza maisha kufuatia tetemeko, tsunami Indonesia

Watu 384 wapoteza maisha kufuatia tetemeko, tsunami Indonesia

Kimataifa
  Maafisa wa Indonesia wamesema kuwa watu wasio pungua 384 wamepoteza maisha na wengine 540 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 7.5 liliotokea Ijumaa na kufuatiwa na kishindo cha wimbi kubwa la tsunami katika miji miwili – Palu na Donggala – eneo la kati la jimbo la Sulawesi. Vyombo vya usalama vimesema Jumamosi mamia ya watu walikuwa kwenye ufukwe wa Palu wakiwa katika tafrija wakati tetemeko hilo lilipozuka na wimbi kubwa la tsunami kulikumba eneo hilo, likiwazoa watu wengi na kupoteza maisha. Msemaji wa kitengo cha maafa cha taifa Sutopo Purwo Nugroho amesema kuwa tsunami hiyo ilikuwa ina safari kilomita 800 kwa saa, na limeharibu majengo na miundo mbinu. Amesema maelfu ya nyumba, hospitali na sehemu za maduka makubwa na hoteli zi
UN: Wakimbizi 30 elfu wanahitajia misaada ya haraka, mashariki mwa Syria

UN: Wakimbizi 30 elfu wanahitajia misaada ya haraka, mashariki mwa Syria

Jamii, Kimataifa
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kuna wakimbizi 30 elfu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Syria kutokana na mashambulizi ya miezi mitatu iliyopita dhidi ya maeneo ya magaidi wa Daesh (ISIS) mkoani Deir ez-Zor. Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini New York Marekani kuwa, kwa mujibu wa ripoti za maafisa wa Umoja wa Mataifa na taasisi za misaada ya kibinadamu, mshambulizi ya kijeshi dhidi ya genge la kigaidi la Daesh katika mkoa wa Deir ez-Zor yaliyoanza mwezi Juni 2018 yamepelekea watu 30 elfu kuyakimbia makazi yao. Amesema hali ya wakimbizi hao ni mambo sana na hawana suhula zozote za lazima zikiwemo za afya huku baadhi yao wakiwa wanahitajia huduma za haraka za tiba.   Tangu mwaka 2014, Marekani na kundi
error: Content is protected !!