Kimataifa

Kura ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya Syria ya kumiliki eneo la Golan licha ya upinzani wa Marekani

Kura ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya Syria ya kumiliki eneo la Golan licha ya upinzani wa Marekani

Kimataifa, Siasa
Rasimu ya "Azimio la Golan" iliyopasishwa siku ya Ijumaa kwa kura nyingi katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika mjini New York imethibitisha tena kwamba eneo la Golani ni milki ya Syria. Nchi 151 zililipigia kura za ndio azimio hilo hilo. Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel pekee zilipiga kura ya kupinga rasimu hiyo ya "Azimio la Golan". Azimio hilo linathibitisha kuwa  eneo la Golan linalokaliwa kwa mabavu na Israel ni milki ya Syria na imezitaja hatua zote za utawala wa Kizayuni katika eneo hilo kuwa ni batili na kinyume cha sheria. Utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 1967 ulivamia na kulikaribia kwa mabavu eneo la ardhi ya Syria la karibu kilomita mraba 1200 pamoja na miinuko ya Golan na baada ya kupita muda utawala huo ukaliunganisha eneo hilo na ardhi
Nchi 100 kuwakilishwa katika Kongamano la 32 la Umoja wa Kiislamu nchini Iran

Nchi 100 kuwakilishwa katika Kongamano la 32 la Umoja wa Kiislamu nchini Iran

Kimataifa
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madehehbu za Kiislamu amesema, wageni kutoka nchi 100 wamealikwa kushiriki katika Kongamano la 32 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu ambalo limepangwa kufanyika tarehe 24 hadi 26 mwezi huu wa Novemba hapa mjini Tehran. Ayatullah Muhsin Araki aliyasema hayo jana Jumamosi katika mkutano na waandishi wa habari hapa Tehran na kuongeza kuwa: "Pamoja na kuwepo njama za madola ya kiistikbari za kujaribu kuvuruga umoja wa madhehebu za Kiislamu, lakini wawakilishi wa nchi 100 watashiriki katika mkutano wa 32 wa Umoja wa Kiislamu mjini Tehran." Ayatullah Muhsin Araki ameashiria hatua zilizochukuliwa kukurubisha madhehebu za Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema kwamba, kumekuwepo na njama za madola ya kibeberu na kiistikbari za kuvuru
Awer Mabil: Kuanzia kuishi nyumba ya udongo kambi ya wakimbizi hadi kufunga mabao Australia

Awer Mabil: Kuanzia kuishi nyumba ya udongo kambi ya wakimbizi hadi kufunga mabao Australia

Jamii, Kimataifa, Michezo
Safari ya Awer Mabil ilianzia kwenye nyumba ya matope akiwa mkimbizi na leo hii anatikisa nyavu akiwa mchezaji mpira wa kimataifa. Mcheza kandanda huyo mwenye miaka 23 alikulia kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya na mazingira duni yalikuwa ni matatizo ya kila siku kwa familia yake. Baada ya kuhamia nchini Australia kama sehemu ya programu ya kibinadamu, alikumbwa na ubaguzi wa rangi wakati akijaribu kucheza kandanda. Lakini ameyapitia mengi na hata kulifungia bao taifa lililompa hifadhi la Australia wakati ikiichakaza Kuwait kwa mabao 4-0 mwezi Oktoba. Mabil alizaliwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma baada ya wazazi wake kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan. Njaa na mazingira mabaya vilikuwa changamoto mbili za kila siku familia yake ilikumbana nazo. "...
Jamal Khashoggi asaliwa sala ya jeneza mjini Istanbul Uturuki

Jamal Khashoggi asaliwa sala ya jeneza mjini Istanbul Uturuki

Jamii, Kimataifa
Sala ya jeneza kwa ajili ya mwanahabari wa Saudia Jamal Khashoggi aliieuwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul. Baada ya sala ya Ijumaa, waumini  katika msikiti wa Fatih wamediriki sala ya jeneza kwa ajili ya mwanahabari huyo  ambae aliuawa kinyama Oktoba 2 mjini Istanbul. Wanaharakati  na wanasiasa wamediriki sala hiyo kwa  lengo la kutoa wito wa umoja na kukemea  mauaji. Baada ya sala hiyo kumetolewa wito wa kuheshimisha sharia pindi wahusika wa kifo cha Khashoggi watabainika. Ikumbukwe kuwa Saudia alikiri kuuawa kwa Jamal Khashoggi katika ofisi za ubalozi  wake mdogo Istanbul  baada ya Uturuki kutoa ushahidi na viashirio tangu kuonekana kwa mara ya mwisho Khashoggi akiwa hai  akiingia katika ubalozi huo.
Marekani kuendeleza vikwazo dhidi ya Burundi

Marekani kuendeleza vikwazo dhidi ya Burundi

Kimataifa, Siasa
Marekani imesema Ijumaa itaendelea kutekeleza vikwazo iliyopitisha Novemba 22, 2015 dhidi ya Burundi kutokana na kuendelea kwa hali ya taharuki, ikiwemo uvunjifu wa amani nchini humo. Imesema ili kukabiliana na tishio hilo vikwazo hivyo vilivyo kuwa vimewekwa lazima viendelezwe baada ya Novemba 22, 2018. Hali ya usalama nchini Burundi inaendelea kuwa siyo ya kawaida na ni tishio kwa usalama wa taifa na sera ya nje ya Marekani inayotokana na hali halisi nchini Burundi, imesema taarifa ya White House, yenye amri ya kiutendaji lilosainiwa na Rais Donald Trump. Agizo la Trump limesema kumekuwepo na uvunjaji wa amani dhidi ya raia, ghasia, uchochezi unaopelekea vurugu, na ukandamizaji mkubwa wa kisiasa, ambao unahatarisha amani, usalama, na utulivu wa Burundi na eneo lote...
error: Content is protected !!