Kimataifa

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 katıka vıpımo vya ritcher limeıpıga Ecuador

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 katıka vıpımo vya ritcher limeıpıga Ecuador

Jamii, Kimataifa
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 lımerıpotıwa nchini Ecuador. Taasisi ya utafiti wa kijiolojia ya Marekani USGS, imesema kwamba kitovu cha tetemeko hilo ni kilomita 115 kusini mashariki mwa kijiji cha Palora kilichopo eneo la Morona Santiago. Tetemeko hilo limerıpotıwa kutoka kina cha kilomita 132.4. Hakuna hatari ya Tsunami ıliyotangazwa baada ya tetemeko hilo. Mpaka sasa haijatolewa habari yoyote kama kuna vıfo na uharibifu wa mali kutokana na tetemeko hilo.
Sudan : Bashir atangaza hali ya dharura, aitisha mjadala wa kitaifa

Sudan : Bashir atangaza hali ya dharura, aitisha mjadala wa kitaifa

Kimataifa, Siasa
Rais Omar al-Bashir Rais Omar el-Bashir wa Sudan Ijumaa amewataka waasi, wanaharakati na vyama vya upinzani kukutana na kufanya mjadala wa kitaifa. Rais pia amezivunja serikali za mitaa na taifa na ataunda serikali mpya baada ya mjadala wa taifa kufanyika. Pia ametangaza hali ya dharura ya taifa kwa kipindi cha mwaka mmoja. Nchini Sudan kumekuwa na maandamano yalidumu tangu Disemba 19, wakati serikali ilipandisha bei ya mkate. Tangu wakati huo, maandamano yameongezeka na kuambatana na vurugu kati ya polisi wa kukabiliana na ghasia na waandamanaji. Maandamano sasa yamegeuka na kuwa ya kutaka rais Omar Al-Bashir kuondoka madarakani. Serikali ya Sudan inasema watu 31 wamekufa kufuatia maandamano hayo, lakini wachunguzi wa kimataifa wa haki za kibinadamu wanasema watu ...
Watetezi wa haki za binadamu waandamana kupinga hukumu za vifo Misri

Watetezi wa haki za binadamu waandamana kupinga hukumu za vifo Misri

Kimataifa
Watetezi wa haki za binadamu wamefanya maandamano katika nchi kadhaa duniani kupinga utekelezaji wa hukumu ya kifo dhidi ya wapinzani wa serikali ya Misri. Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu katika miji ya Tunis na Berlin walikusanyika katika miji hiyo wakilaani hukumu ya kifo iliyotekelezwa nchini Misri dhidi ya wapinzani wa mapinduzi ya serikali halali ya nchi hiyo katika kadhia inayojulikana katika vyombo vya habari kuwa ni ya mauaji ya aliyekuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo, Hisham Barakat. Waandamanaji hao wanasema hukumu za vifo dhidi ya wapinzani hao hazikutegemea misingi sahihi na ya kiadili ya mahakama. Waandamanaji hao ambao walikusanyika mbele ya ubalozi wa Misri mjini Tunis, Tunisia wametoa nara dhidi ya utawala wa kijeshi wa Misri na ...
Sisitizo la Umoja wa Mataifa la kusaidiwa kifedha Waislamu wa jamii ya Rohingya

Sisitizo la Umoja wa Mataifa la kusaidiwa kifedha Waislamu wa jamii ya Rohingya

Jamii, Kimataifa
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutolewa misaada ya kifedha kwa ajili ya Waislamu wa jamii ya Rohingya walioko nchini Bangladesh. Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kwamba, unahitajia msaada wa kiasi cha dola bilioni moja kwa ajili ya kuwapatia misaada ya kibinadamu zaidi ya Waislamu 900,000 wa jamii ya Rohingya walioko katika kambi za wakimbizi katika mpaka wa Myanmar na Bangladesh. Umoja wa Mataifa umewahi kusema katika moja ya ripoti zake kwamba, muamala wa serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu Warohingya kuwa ni jinaii dhidi ya binadamu na kutaka kupandishwa kizimbani makamanda wa jeshi wa nchi hiyo wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kizazi dhidi ya Waislamu Warohingya. Waislamu wa Rohingya wakiwa katika maisha ya ukimbizini Hata hivyo ser...
error: Content is protected !!