Jamii

Mvua kubwa kunyesha Novemba 2018, Mikoa 11 yapewa tahadhari

Mvua kubwa kunyesha Novemba 2018, Mikoa 11 yapewa tahadhari

Jamii, Mikoani, Nyumbani, Updates
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi  vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019 katika kanda za magharibi, kati na nyanda za juu kusini. Maeneo yatakayoathirika na mvua hizo za juu ya wastani hadi wastani ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara. Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 18, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema  utabiri huo ni kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. “Katika kipindi cha mvua za msimu hali ya unyevunyevu wa udongo kwa ustawi wa mazao na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi,” amesema. “Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi kama vile mahindi,
Mpigapicha maarufu wa kimataifa wa Uturuki aaga dunia akiwa na umri wa miaka 90

Mpigapicha maarufu wa kimataifa wa Uturuki aaga dunia akiwa na umri wa miaka 90

Jamii, Kimataifa
Ara Güler , mpigapicha maarufu wa Uturuki ambae alikuwa  akifahamika kimataifa ame aga dunia akiwa na umri wa miaka 90. Mpigapicha wa kimataifa wa Uturuki Ara Güler amefariki    usiku wa Jumatano akiwa katika  hospitali ya Florence  Nightingale mjini Istanbul ambapo alikuwa akipatiwa matibu kwa muda. Güler alikuwa akifahamika kwa kazi zake za upigaji picha ulimwenguni kote. Taatifa kuhusu  kifo cha mpigapicha huyo imetolewa na daktari Zafer Gokay. Daktari huyo alifahamisha kuwa  vyombo vya matibabu alivyokuwa amefungwa Güler  havikuweza kuendelea kutoa matibabu na Güler kufariki. Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan amempigia simu mkurugenzi wa jumba la makumbusho la Ara Güler na kumpa pole Cağla Saraç. Viongozi na mawaziri wa Uturuki wametoa samal za rambi rambi kwa f
Mzee wa miaka 65 awadhalilisha kijinsia watoto anaowalea akiwemo mwanawe wa kambo Unguja

Mzee wa miaka 65 awadhalilisha kijinsia watoto anaowalea akiwemo mwanawe wa kambo Unguja

Jamii, Nyumbani
Babu anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 65 adaiwa kumlawiti mtoto wake wa kambo pamoja na kumkashifu sehemu za siri mtoto ambae anamlea na hatimae kukimbia pasipojulikana. Tukio hilo limetokea Shehia ya Gulioni Mjini Unguja,watoto hao ni wa kike majina yao yamehifadhiwa ikiwa mmoja anaumri wa miaka 8 na mwengine anaumriwa miaka 12. Mama wa watoto hao amesema kuwa mumewe alikuwa akiwafanyia vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo chooni huku akiwapa kipigo na vitisho pasi na mama huyo kujua kinachoendelea ndani kwake. Kwa upande wake Sheha wa shehia ya Guliaoni Hamimu Issa Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kwa mujibu wa taarifa hizo tayari ameweza kuzifikisha kituo cha Polisi.             CHANZO:...
Benki ya Dunia yatahadhaharisha kuhusu kuenea umasikini duniani

Benki ya Dunia yatahadhaharisha kuhusu kuenea umasikini duniani

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa
Benki ya Dunia imetahadharisha kuhusiana na kuenea umasikini katika maeneo mbalimbali duniani. Benki ya Dunia imesema katika ripoti yake ya pili ya mwaka hhuu kwamba, licha ya kufanyika juhudi kubwa za kupambana na umasikini, lakini nusu ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na umasikini ambapo wanaishi chini ya kiwango cha dola tano na senti tano kwa siku, Ripoti hiyo inaeleza kuwa, idadi ya watu masikini wanazidi kuongezeka kila siku. Benki ya Dunia imeeleza wasiwasi wake katika ripoti yake hiyo kwamba, katika baadhi ya nchi umasikini upo katika hali ya kushadidi na kwamba, juhudi za kupuunguza umasikini duniani muda si mrefuu zitakuwa na taathira ndogo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) liliyataka mataifa ya du
Giza nene limetanda mkasa wa kutekwa kwa bilionea Mo Dewji

Giza nene limetanda mkasa wa kutekwa kwa bilionea Mo Dewji

Jamii, Mikoani
Tukio la kutekwa bilionea Mohammed Dewji, 43, Alhamisi ya wiki iliyopita bado limesalia kuwa ni fumbo lisilokuwa na jibu. Mpaka kufikia leo, Jumatano jioni bado haijulikani ni akina nani waliomteka na wapi walipomficha na lipi hasa kusudio la kumteka mfanya biashara huyo maarufu kama Mo. Mo alikwapuliwa na watu wasiojulikana nje ya hoteli moja jijini Dar es Salaam alipokuwa akienda kufanya mazoezi. Toka hapo, giza nene limetanda juu ya tukio hilo, licha ya hatua kadhaa ambazo mamlaka za nchi na familia imezichukua. Toka siku ya kwanza ya tukio polisi kupitia Kamanda wa Dar es Salaam wamekuwa wakiuhakikishia umma kuwa ulinzi umeimarishwa na uchunguzi unafanyika kwa kasi na weledi. Maeneo yote ya kutoka na kuingia jiji la Dar es Salaam ikiwemo fukwe za bahari zinakaguliwa. Ha...
error: Content is protected !!