Jamii

WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya kupatikana na dawa za kulevya.

WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya kupatikana na dawa za kulevya.

Jamii, Nyumbani
WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya kupatikana na dawa za kulevya. Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Haji Abdalla Haji, aliwataja watuhumiwa kuwa nii Staling Makame Machano mkaazi wa Chaani Njaro, aliyepatikana na kete 293 zikiwa kwenye vifurushi. Mwengine ni Mohamed Chum Haji (39) mkaazi wa Mahonda aliyepatikana na kete 98 zinazosadikiwa kuwa nibangi. Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 9, mwaka huu saa 9:00 usiku. Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia operesheni ya kupambana na dawa za kulevya. Alisema jeshi hilo litaendelea kupambana na wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya kwa lengo la kukomeshabiashara hiyo. Hata hivyo, aliwanasihi vijana kuacha kutumia dawa za kulevya pamoja na kujihusisha na biashar...
UNCTAD: Wapalestina Ghaza wanakabiliwa na hali mbaya kutokana na mzingiro wa Israel

UNCTAD: Wapalestina Ghaza wanakabiliwa na hali mbaya kutokana na mzingiro wa Israel

Jamii, Kimataifa
Ukanda wa Ghaza umegeuka kuwa janga la kibinadamu lililogubikwa na madhila na utegemezi wa misaada kila uchao kutokana na mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ardhi hiyo ya Palestina. Hayo yamo katika ripoti mpya ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo na biashara UNCTAD ambayo imeongeza kuwa ukosefu wa ajira katika eneo hilo unaifanya Ghaza kuwa eneo linaloongoza kwa jambo hilo duniani kutokana na kuongezeka ukosefu wa ajira kwa zaidi ya asilimia 27, huku pato la kila mtu likishuka, uzalishaji wa kilimo ukipungua kwa asilimia 11 na hali ya kiuchumi na kijamii kwa mwaka 2017 ikizorota zaidi. Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba masharti yaliyowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo yanawaathiri vibaya wanawake na vijana, na kuonya kwamba kupungua kwa msaad
KIKOSI cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar (KZU), kimetoa tahadhari kwa wamiliki wa majengo ambao hawatokuwa tayari kutoa ushirikiano katika ukaguzi unaofanywa na kikosi hicho.

KIKOSI cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar (KZU), kimetoa tahadhari kwa wamiliki wa majengo ambao hawatokuwa tayari kutoa ushirikiano katika ukaguzi unaofanywa na kikosi hicho.

Jamii
KIKOSI cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar (KZU), kimetoa tahadhari kwa wamiliki wa majengo ambao hawatokuwa tayari kutoa ushirikiano katika ukaguzi unaofanywa na kikosi hicho. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa sheria wa Zimamoto, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Kilimani. Alisema, ukaguzi wanaofanya katika majengo mbalimbali ni kwa mujibu wa sheria namba 7 ya mwaka 1999 chini ya kifungu cha 7 (1) ambacho kinampa mamlaka Kamishna wa Zimamoto kufanya ukaguzi katika majengo. Alisema, ukaguzi huo ulianza Agosti 12 mwaka huu na wamefanikiwa kukagua hoteli 11, mikahawa mitatu, maduka 10, maghala ya kuhifadhia chakula matatu, hosteli moja, duka moja na ofisi ndogo moja kwa upande wa mkoa wa mjini magharibi. Aidha alisema, lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuh...
Larkin Crow, mtalii kutoka jimbo la Texas nchini Marekani amejinyonga kwa kamba na kujimalizia maisha nchini Uganda

Larkin Crow, mtalii kutoka jimbo la Texas nchini Marekani amejinyonga kwa kamba na kujimalizia maisha nchini Uganda

Jamii
Larkin Crow, mtalii kutoka jimbo la Texas nchini Marekani amejinyonga kwa kutumia mkanda na kujimalizia maisha katika umbali wa kilomita 40 na jiji la Kampala nchini Uganda Alkhamis. Tukio hilo limetokea Wakiso. Taarifa hiyo imetolewa na  naibu msemaji wa jeshi la Polisi  Patrick Onyango. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na  naibu huyo, Karkin Crow amekutwa amefariki kwa kujinyonga katika kituo cha mafunzo Entebbe. Uchunguzi umeanzishwa kufahamu ni kipi lichotokea kabla ya tukio hilo.
TAMWA watoa somo kwa walezi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu

TAMWA watoa somo kwa walezi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu

Jamii, Nyumbani
Wazazi na Walezi Mkoa wa kaskazini Unguja wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha na kutowapeleka skuli watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) jambo linalopelekea kuwa nyuma kimaendeleo na kuwasababishia watoto hao kuwa tegemezi. Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Wilaya ya Kaskazin “B” Unguja  Mshamara Chum Kombo katika mkutano maalum wa kujadili matatizo wanayokabiliana nayo wananchi katika mkoa wa kaskazini Unguja ikiwa ni muendelezo wa kutekeleza mradi wa Paza kushirikiana na wanaharakati na  Jumuiya za maendeleo katika vijiji husika katika Nyanja za Elimu , Afya, kilimo, mazingira  na maji, Alisema tatizo la kuwaficha na kutowapeleka skuli  kupata elimu  watoto wenye mahitaji maalum kwa mkoa wa kaskazini Unguja limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuwazorotesha watoto ha
error: Content is protected !!