Jamii

Sierra Leone yaanzisha shule ya ‘kuwafunda’ wanaume baada ya kuongezeka ukatili dhidi ya wanawake

Sierra Leone yaanzisha shule ya ‘kuwafunda’ wanaume baada ya kuongezeka ukatili dhidi ya wanawake

Jamii, Kimataifa
Mwanamme mmoja ameamua kufungua shule ya "kuwafunda" wanaume jinsi ya kuishi vizuri na wake zao nchini Sierra Leone baada ya ukatili dhidi ya wanawake kuongezeka kupindukia katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Mwanamme huyo anayejulikana kwa jila la Pidia Joseph Allieu amesabilia maisha yake katika jitihada za kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nchini Sierra Leone. Takwimu ambazo ni muhali kuzithibitisha zinaonesha kuwa wanawake laki mbili walikuwa wahanga wa kijinsia katika vita vya muda mrefu vilivyoikumba nchi hiyo kuanzia mwaka 1991 hadi 2002. Mwezi ulioisha wa Februari 2019, Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone alitangaza vitendo vya ubakaji kuwa ni janga la taifa. Pidia amejitolea kutoa mafunzo kwa wanaume katika juhudi za kuleta mabadilik...
Bodi ya chakula na dawa Zanzibar yaangamzia Tani 520 za sukari isyokuwa na Kiwango

Bodi ya chakula na dawa Zanzibar yaangamzia Tani 520 za sukari isyokuwa na Kiwango

Afya, Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula na Dawa wakimwaga sukari katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe Wilaya ya Kaskazini B wakiwa katika zoezi la kuiangamiza sukari iliyokosa kiwango kwa matumizi ya wananchi. Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Hassan  Khamis Hafidh amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachukuwa hatuwa kali kwa Mfanyabiashara yoyote atakaeingiza bidhaa isiyokuwa na kiwango kwa ajili ya matumizi ya wananchi.  Aliyasema hayo Bandari ya Malindi Zanzibar alipofika kuangalia zoezi la kuhamisha tani 520 za sukari kwenda kuangamizwa kwenye mashimo ya mchango katika kijiji cha Zingwezingwe baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya binaadamu. Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar Dk. Khamis Ali akizungumza na waandishi ...
Talaka baina ya wanandoa zashamiri nchini Uturuki

Talaka baina ya wanandoa zashamiri nchini Uturuki

Jamii, Kimataifa
Shirika la takwimu nchini Uturuki (TÜİK) limetoa takwimu kuhusiana na ndoa zilizofungwa na zilizovunjika kwa mwaka 2018. Kwa mujibu wa takwimu hizo kiwango cha waliofunga ndoa kilipungua kwa asilimia 2.9 kutoka ndoa 569,459 mwaka 2017 hadi ndoa 553,202 mwaka 2018. Kwa wastani wa kiujumla katika kila watu 1000 zilifungwa ndoa 6.8. Kwa upande wa talaka, kuna ongezeko la asilimia 10.9 kutoka talaka 128,411 zilizotolewa mwaka 2017 hadi talaka 142,411 zilizotolewa mwaka 2018. Kwa wastani wa kiujumla kulikuwa na talaka 1.75 katika kila watu 1000.
Ukosefu wa Madaktari Tumbatu wasababisha kina mama kujifungua nyumbani

Ukosefu wa Madaktari Tumbatu wasababisha kina mama kujifungua nyumbani

Afya, Jamii, Nyumbani
Wanawake wa Kijiji cha Tumbatu kilichopo katika wilaya ya Kaskazini A Unguja wanakabiliwa na tatizo la kukosekana kwa huduma za Afya kijijini hapo kutokana na ukosefu wa madaktari katika kituo cha afya katika kijiji hicho. Hayo yameelezwa na Daktari msaidizi wa kituo cha afya Tumbatu Mcha Haji Makame wakati akizungumza na Waandishi wa Habari. Amesema licha ya jitihada za serikali za kuimarisha huduma za kijamii lakini suala la afya za mama na mtoto bado limeshindwa kutafutiwa ufumbuzi na kuwapa wakati mgumu wanawake wa kijiji hicho. Amesema wakina mama wa Tumbatu bado wanakabiliwa na matatizo  kwa kukosa kituo  cha kujifungulia kutokana na wodi ya wazazi kituo cha afya Tumbatu kushindwa  kutoa huduma kutokana na kukosekana na madaktari wa  kutoa huduma hizo z...
Rais wa Algeria mahututi hospitalini Uswisi, huku maandamano yakishadidi nchini mwake

Rais wa Algeria mahututi hospitalini Uswisi, huku maandamano yakishadidi nchini mwake

Afya, Jamii, Kimataifa
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, hali ya afya ya Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ni mbaya na kwamba kwa sasa yuko mahututi. Aidha ripoti nyingine zinasema kuwa, Rais huyo wa Algeria amezirai huko hospitalini mjini Geneva Uswisi alikopelekwa ajili ya matibabu huku madaktari wakisema kuwa, wanashindwa kumfanyia upasuaji kutokana na kudhoofika mno kiafya. Taarifa zaidi zinasema kuwa, Rais Abdelaziz Bouteflika,  aliyetimiza miaka 82 hapo jana na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1999 kwa sasa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ghorofa ya tisa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Geneva. Wakati huo huo, ndege maalumu ya Rais huyo imerejea nchini Algeria bila ya kiongozi huyo. Bouteflika anayetembelea kiti cha magurudumu na ambaye amekuwa ...
error: Content is protected !!