Jamii

KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H

KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa, Mikoani, Nyumbani, Teknolojia, Updates
REF: MM/OD/E/2018/TO/SE11-077                                                                         11-09-2018 Taarifa kwa Umma, As Salaam A’laykum, KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Allah (S.W) kwa kutujaalia sote tukiwa wazima wa Afya na wale wote waliowagonjwa basi Allah awajaalie siha njema, pia kumtakia rehma mtume wetu Muhammad (S.A.W) pamoja na maswahaba wake, wake zake, jamaa zake na waislamu wote kwa ujumla dunia. Pia tunawaombea ndugu zetu katika imani ambao wametangulia mbele ya haki, Kampuni ya Moyo Media tunayo furaha kusherehekea mwaka mpya wa kiislamu 1440 H, Kwa niaba ya Uongozi wa kampuni, tunawatakia wafanyakazi wetu wote na waislamu duniani kote kheri na Baraka za mwaka 1440 H, Tunakuomba Mungu wet
Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare

Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare

Jamii, Kimataifa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amesema watu wasiopungua 16 wamefariki dunia wiki iliyopita kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Clemens Dori ameashiria kuenea maambukizi ya kipindupindu kusini magharibi mwa Zimbabwe na kueleza kwamba watu 106 wamelazwa hopsitali ya maradhi ya maambukizi mjini Harare. Mkurugenzi Mkuu huyo wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji wa Harare ameongeza kuwa maafisa husika wameweka usimamizi maalumu katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo na kutuma kwenye maeneo hayo timu za maafisa wa Wizara ya Afya za uchukuaji hatua za haraka. Katika kipindi cha kati ya mwezi Agosti mwaka 2008 hadi Juni 2009 watu 98,596 walipatwa na ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe ambapo 4,369 miongoni
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu CCM Mhe. Simai Mohammed Said Amewaasa Watoto Kusoma Quran Ili Iwajenge Kimaadili

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu CCM Mhe. Simai Mohammed Said Amewaasa Watoto Kusoma Quran Ili Iwajenge Kimaadili

Jamii
Na Salum Vuai JAMII katika Wilaya ya Kati, imehimizwa kuwasimamia vyema watoto na kuhakikisha wanasoma vizuri elimu zote, dini na dunia. Akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Kuran kwa madrasa za kanda ya Bungi katika jimbo la Tunguu, Mwakilishi wa jimbo hilo Simai Mohammed Said, amesema elimu ya dini ndio dira ya kuwaongoa watoto wa Kizanzibari. Amesema vitendo vya udhalilishaji vilivyokithiri nchini, vinaweza kudhibitiwa iwapo kila mzazi atabeba kikamilifu dhima ya uchunga wa familia kwa ushirikiano na wanajamii wote. Simai alieleza kufurahishwa na utaratibu wa kuandaa mashindano hayo ya kuhifadhi kitabu kitatakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisema hicho cha kwanza kwani kimebeba mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu. “Usomi wowote unaendana na kusoma vitabu vya aina
Tatizo la ndoa za watoto

Tatizo la ndoa za watoto

Jamii
Kuwaozesha watoto wadogo huwa na madahara kadhaa ya kimwili kama vile kutokuwa tayari kushika mimba katika umri mdogo na vile vile matatizo ya kisaikolojia kutokana na kulazimishwa kufunga ndoa n.k. Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Tume Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, kila siku duniani mabanati 39 huozwa bila kuridhia wala pasina haki ya kuchagua mume. Iwapo hali kama hii itaendelea, inatabiriwa kuwa ifikapo mwaka 2020, kutakuwa na wasichana milioni 142 walioozeshwa kabla ya kufika umri wa miaka 18. Elina ni binti kutoka nchi ya Malawi ambaye alilazimishwa kufunga ndoa akiwa na umri wa miaka 15. Anasema hivi kuhusu suala hilo: "Nilipata matatizo mengi baada ya kuolewa. Nilikuwa mtoto mdogo na sikujua ni vipi niwe mke. Kipindi kibaya zaidi kilikuwa wakati nilipo...
error: Content is protected !!