Jamii

SMZ imesema bado ina fursa ya kukopesheka kwa vile ipo katika kiwango cha chini cha kupewa mkopo katika mabenki ya dunia.

SMZ imesema bado ina fursa ya kukopesheka kwa vile ipo katika kiwango cha chini cha kupewa mkopo katika mabenki ya dunia.

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Mohammed Salum SERIKALI imesema bado ina fursa ya kukopesheka kwa vile ipo katika kiwango cha chini cha kupewa mkopo katika mabenki ya dunia. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Mohammed Salum, aliyasema hayo jana wakati akitoa majumuisho ya ripoti ya kamati ya kudumu ya bajeti ya baraza la wawakilishi kwa mwaka wa fedha 2018/2019, katika ukumbi wa baraza hilo, Chukwani. Ripoti hiyo, iliyowasilishwa na Mwakilishi wa jimbo la Mpendae, Mohamed Saidi Dimwa, ilifahamisha kwamba deni la taifa hadi kufikia Febuari 2019, ni shilingi 444.480 bilioni linalojumuisha deni la ndani la shilingi 162.870 bilioni na deni la nje shilingi 281.601 bilioni. Mwakilishi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, alisema sababu za kuwepo kwa deni la ...
Lori lagongana na msafara wa harusi nchini India

Lori lagongana na msafara wa harusi nchini India

Jamii, Kimataifa
Lori limegongana na msafara wa harusi na kusababisha vifo vya watu 13 katika jimbo la Racastan magharibi mwa India. Afisa Mkuu wa Wilaya Shyam Singh Rajpurohi, amesema kuwa ajali hiyo imetokea katika barabara kuu ya mji wa Pratapgarh baada ya lori liyokuwa ikienda kwa kasi kubwa kugongana na msafara wa harusi na kusababisha vifo vya watu 9 papo hapo. Watu wengine wanne wamefariki baada ya kufikishwa hospitali. Watu wengine 19 wamejeruhiwa.
Dk. Shein aahidi kutandika miundombinu Uzi

Dk. Shein aahidi kutandika miundombinu Uzi

Jamii, Nyumbani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Uzi wilaya ya Kati baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa, akiwa katika ziara mkoa wa Kusini Unguja. Kulia waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma na waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheri.(PICHA NA IKULU). RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi, Dk.Ali Mohamed Shein, amesema  serikali itajenga daraja, barabara na skuli ya sekondari katika kijiji cha Uzi Ng’ambwa, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu  kwa wakaazi wa kijiji hicho na maeneo jirani. Aliyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi
Tiba dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi

Tiba dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi

Afya, Jamii, Kimataifa
Wanasayansi kutoka nchini Italia wamegundua chanjo dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI "AIDS" (Acquired Immune Deficiency Syndrome / Upungufu wa Kinga Mwilini). Kinga hio imefanikiwa kupunguza mwilini idadi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukımwi "HİV" kwa asilimia 90. Timu ya utafiti huu iliongozwa na Barbara Ensoli ambaye amefahamisha yafuatayo kuhusiana na matokeo ya utafiti huo: Utafiti wao mpaka ulipofikia imethibitika kwamba chanjo waliyoitengeneza imetoa majibu ambayo waliyakusudia, yaani kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi. Na cha zaidi imefanikiwa kupunguza kiwango cha virusi vya Ukimwi kwa asilimia 90. Chanjo hiyo ambayo bado ipo kwenye majaribio inailenga aina maalum ya "protein " ijulikanayo kama HIV-1 Tat. Pro
Jinsi hesabu zilivyoijenga China na kumwezesha Mfalme ‘kulala’ na wanawake 121 dani ya siku 15

Jinsi hesabu zilivyoijenga China na kumwezesha Mfalme ‘kulala’ na wanawake 121 dani ya siku 15

Jamii
Kuanzia kupiga hesabu ya nyakati mpaka kuvuka bahari, hesabu ndio utaalamu ambao falme na ustaarabu wa watu wa kale waliutegemea. Safari ya uvumbuzi wa hesabu ilianzia Misri, kisha Mesopotamia na Ugiriki, lakini baada ya dola hizo kuanguka, maendeleo ya hesabu nayo yakaanguka ka umande wa Magharibi. Lakini kwa upande wa Mashariki mambo yalikuwa tofauti na hatua kubwa zilikuwa zikipigwa. China ya kale, hesabu ndio kilikuwa kiungo tegemezi cha kusimamisha Ukuta Mkuu ambao mpaka leo ni moja ya maajabu ya dunia. Na namba zilikuwa muhimu hata katika kupangilia maisha katika nyumba ya ufalme. Mpangilio wa hesabu za mapenzi Kuwa mfalme kulihitaji mtu awe na nguvu za kutosha Kalenda na mwenendo wa sayari ndio vilichangia maamuzi yote ya mfalme...
error: Content is protected !!