Jamii

ICC yaanza kuchunguza jinai za Myanmar dhidi ya Waislamu Warohingya

ICC yaanza kuchunguza jinai za Myanmar dhidi ya Waislamu Warohingya

Jamii, Kimataifa
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeanza kuchunguza jinai dhidi ya binaadamu zinazofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya. Taarifa iliyotolewa na Fatou Bensouda, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC imesema korti hiyo yenye makao yake mjini The Hague nchini Uholanzi imeanzisha uchunguzi wa awali wa kubaini iwapo kuna ushahidi wenye mashiko ambao utatoa waranti wa kuanzisha uchunguzi kamili kuhusu jinai za jeshi la Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya, yakiwemo mauaji, ubakaji na kufukuzwa makwao watu wa jamii hiyo ya wachache katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia. Tangazo hilo la ICC limetolewa katika hali ambayo, Umoja wa Mataifa hapo jana Jumanne pia ulisisitizia haja ya kufunguliwa mashitaka makamanda waandamizi wa jeshi la Mynamar kutokana na m
Sababu ya Afrika Kusini kuhalalisha utumizi wa bangi

Sababu ya Afrika Kusini kuhalalisha utumizi wa bangi

Jamii
Watu wakivuta bangi nje ya mahakama ya katiba nchini Afrika Kusini baada ya ukuzaji na uvutaji wa bangi kuhalalishwa Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha. Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi. Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa ban gi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Hata hiyyo itakuwa haramua kutumia bangi katika maeneo ya umma au kuiuza. Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini limeunga mkono uamuzi wa mahahakama dhidi ya matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho. Uamuzi huu un...
Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili

Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili

Jamii, Kimataifa
Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini amesema shule za nchi hiyo zitaanza kufunza lugha ya Kiswahili kuanzia mwaka 2020. Angie Motshekga aliyasema hayo jana Jumatatu na kufafanua kuwa, uamuzi huo wa kuanza kufunzwa lugha ya Kiswahili latika shule za umma, binafsi na huru za nchi hiyo umeidhinishwa na Baraza la Mawaziri la nchi hiyo. Waziri huyo amebainisha kuwa, "Tunaamini kwamba, kufundishwa lugha ya Kiswalihi katika shule za Afrika Kusini kutasaidia kuimarisha utangamano wa kijamii na Waafrika wenzetu." Amesema Kiswahili kina uwezo wa kupanuka na kuenea katika nchi za Afrika ambazo hazizungumzi lugha hiyo, na kina uwezo wa kuwakurubisha tena pamoja wananchi wa Afrika. Kinara wa chama cha upinzani cha EFF nchini Afrika Kusini, Julius Malema Kiswahili ni lugha ya kwanza y...
Baba wa kambo adaiwa kumbaka mtoto wa mkewe huko Ndijani Kusini Unguja

Baba wa kambo adaiwa kumbaka mtoto wa mkewe huko Ndijani Kusini Unguja

Jamii, Nyumbani
Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Unguja limempandisha katika kizimba cha mahakama ya mkoa Mwera mtuhumiwa Bakari Makame Khatib miaka 30 mkaazi wa Binguni wilaya ya kati kwa kosa la kumuingilia maharimu wake. Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka Shumbana Mbwana mbele ya hakimu Harub Shehe Pandu kwamba mnamo tarehe 19, 3, 2018 majira ya saa 1 usiku huko Ndijani mkoa wa Kusini Unguja bila ya halali na kwamakusudi mtuhumiwa alimuingilia kimwili binti wa miaka 18 ambaye ni mtoto wa mkewe jina linahifadhiwa huku akijua kuwa jambo hilo ni kosa kisheria. Baada ya kusomewa kosa lake mahakamani hapo Mtuhumiwa alikataa kosa na kuiomba mahakama impe dhamana ambapo mahakama imeamuru aende rumande hadi tarehe 24, 9, 2018 ndipo itakaposikilizwa dhamana yake.
Coca-Cola ilivyopata jina lake

Coca-Cola ilivyopata jina lake

Afya, Jamii
Coca-Cola ni moja ya kampuni maarufu duniani, ambayo hutengenezwa soda maarufu ya Coke na vinywaji vingine vya soda. Lakini, ilikuwaje hadi ikawa na jina hilo? Labda umewahi kusikia kwamba Coca-Cola wakati mmoja ilikuwa na kiungo cha kusisimua ambacho kiliwafanya wateja kulipenda sana. Hii ni moja ya vilivyochangia jina lake. "Coca", kwa Kiswahili koka, ni jina la jani la mmea wa koka, moja ya viungo ambavyo mvumbuzi wa kinywaji hicho, mwanakemia wa Atlanta John Stith Pemberton, alichanganya na shira kutengeneza kinywaji chake. Majani ya koka hutumiwa kutengeneza kokeini. Wakati huo, mwishoni mwa karne ya 19, ilikuwa kawaida kwa majani ya koka kuchanganywa na divai na kuwa kinywaji cha kuchangamsha mwili. Kinywaji kipya alichotengeneza Pemberton kilikuwa njia nzuri ya kukwep...
error: Content is protected !!