Jamii

Faith Fennidy: Nywele za binti huyo zenye asili ya kiafrika zimezua mjadala katika mitandao ya kijamii Louisiana, Marekani

Faith Fennidy: Nywele za binti huyo zenye asili ya kiafrika zimezua mjadala katika mitandao ya kijamii Louisiana, Marekani

Jamii
Faith Fennidy, akifuta machozi baada ya kushambuliwa kwa maneno kuhusu nywele zake Video moja iliyotandaa mitandaoni inamuonesha msichana akiondoka shuleni kwasababu ya kuvunja sheria za shule imezua mjadala katika mitandao ya kijamii juu ya ubaguzi na ukosefu wa ufahamu kuhusu nywele za watu weusi. Msichana huyo ana umri wa miaka kumi na mmoja anaitwa Faith Fennidy, anaonekana kwenye video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao pendwa wa facebook, anaonekana akifuta machozi huku akikusanya vitu vyake katika shule ya Christ the King Parish iliyoko Terrytown, Louisiana. Mama wa binti huyo Montrelle amemtaka mwalimu aeleze kwanini rasta za mwanawe zilizofungwa nyuma ya kisogo chake, ni kwa namna gani zimekiuka sera za shule. Shule hiyo ya binafsi imetoa msimamo wake kwa kueleza kuwa wasicha...
Wanasheria wa Algeria: Ufaransa inapasa kuwalipa fidia wahanga wa ukoloni nchini Algeria

Wanasheria wa Algeria: Ufaransa inapasa kuwalipa fidia wahanga wa ukoloni nchini Algeria

Jamii
Mwanasheria mmoja wa haki za binadamu nchini Algeria ametaka Paris ilipe gharama na fidia kufuatia kukiri serikali ya Ufaransa kuwatesa na kuwaua wale wote waliokuwa wakiunga mkono mapinduzi ya Algeria. Muhammad Sami Abdulhamid mwanasheria wa nchini Algeria amesema kuwa Paris inapasa kuzilipa fidia familia za wahanga wa kipindi cha kukoloniwa Algeria na hiyo ni kufuatia Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kukiri na kumuomba radhi mke wa mmoja wa wafuasi wa mapinduzi ya Algeria ambaye aliaga dunia baada ya kuteswa na Wafaransa. Maurice Audin alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kifaransa ambaye alikuwa akiishi Algiers mji mkuu wa Algeria miaka kadhaa kabla ya kupata uhuru nchi hiyo; na alikuwa akiunga mkono mapinduzi dhidi ya wakoloni wa Kifaransa. Wanajeshi wa Ufaransa walimtia mbaroni
Waislam Uganda wafanya maombi maalum dhidi ya dhulma, mauaji na utekaji nyara

Waislam Uganda wafanya maombi maalum dhidi ya dhulma, mauaji na utekaji nyara

Jamii
Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam wa Uganda Maelfu ya waumini wa dini ya Kiislamu nchini Uganda wameshiriki maombi ya kitaifa kote nchini kutokana na ongezeko la mauaji, utekaji nyara na dhuluma za vyombo vya usalama na kutoweka kwa watu katika mazingira tatanishi. Ibada kuu imefanyika katika msikiti mkuu wa Old Kampala, ikiongozwa na Mufti Shaban Ramadhan Mubaje. Maombi kama hayo pia yamefanyika katika kila msikiti kote Uganda. “Tunawaombea wale wote waliouwawa, wanaozuiliwa gerezani kisiasa, hasa wanaozuiliwa kwa makosa ambayo hawakufanya, wanaopata vitisho dhidi ya maisha yao na taifa lote kwa ujumla,” amesema Kiongozi wa dini ya Kiislamu Uganda, Mufti Mubaje akiongezea kwamba maombi ya Ijumaa ni ya kidini na hayahusiani kwa namna yoyote na siasa za nchi hiyo.
Waislamu katika zaidi ya nchi 41 duniani wamkumbuka Ali Asghar, shahidi wa miezi 6 wa Karbala

Waislamu katika zaidi ya nchi 41 duniani wamkumbuka Ali Asghar, shahidi wa miezi 6 wa Karbala

Jamii
Shughuli ya kimataifa ya kukumbuka mtoto mchanga wa Imam Hussein bin Ali (as) aliyeuwa shahidi katika medani ya Karbala imefanyika leo nchini Iran na katika nchi nyingine zaidi ya 40 ikiwashirikisha wapenzi na wafuasi wa Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw). Mjini Tehran, shughuli hiyo ya kidini ilianza mapema leo katika msikiti mkubwa wa Imam Khomeini ikiwashirikisha kinamama waliokuwa wamebeba watoto wachanga wanaonyonya. Shughuli hiyo imeandamana na qasida, mashairi na tungo zinazowakumbuka mashahidi wa Karbala hususan Ali al Asghar, shahidi mchanga zaidi kati ya mashahidi waliouliwa wakiwa pamoja na mjukuu wa Mtume (saw), Imam Hussein (as) katika siku ya Ashuraa. Wairan wamkumbuka Ali al Asghar (as).  Shughuli kama hiyo imefanyika pia katika nchi 41 duniani ambako kinamama waliokuw
Hamas yaionya Israel isiendelee kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Hamas yaionya Israel isiendelee kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Jamii
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel juu ya hatari ya kuendelea kuuvinjia heshima Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu na kusisitiza kuwa utawala huo dhalimu ndio utakaobeba dhima ya lolote litakalotokea. Katika tamko lake la jana Alkhamisi, harakati ya HAMAS ilisema kuwa, kitendo cha walowezi wa Kizayuni cha kuzidi kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa katika siku za hivi karibuni kinaonesha kuwa Israel ina nia ya kuudhibiti msikiti huo na kutekeleza ngano za Kizayuni kuhusu eneo hilo takatifu. Walowezi wa Kizayuni wakiingia katika maeneo matakatifu ya Waislamu kwa ulinzi kamili wa wanajeshi wa Israel   Vile vile harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu imesema kuwa, hatua ya walowezi wa Kizayuni ya ku...
error: Content is protected !!