Jamii

Wafungwa 52 wafariki kabla ya kufikishwa mahakamani Madagascar

Wafungwa 52 wafariki kabla ya kufikishwa mahakamani Madagascar

Jamii, Kimataifa
Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limesema watu 52 walikufa wakiwa kizuizini Madagascar mwaka uliopita kabla kesi zao hazijasikilizwa wakati nchi hiyo inakabiliwa na mfumo mbovu wa mahakama. Hayo yameelezwa katika ripoti ya Amnesty International iliyotolewa leo ambayo imeonya kuwa asilimia 55 ya watu 11,000 waliofungwa magerezani nchini Madagascar walikuwa wakisubiri kesi zao zisikilizwe kwa mwaka uliopita wa 2017, licha ya wengi wao kukabiliwa na uhalifu wa makosa madogo, ambapo kwa mujibu wa sheria za kimataifa, bado hawana hatia. Tamara Leger, mshauri na mtetezi wa haki za binaadamu wa Amnesty International nchini Madagascar, anasema kuwa utafiti wao unaonesha hali mbaya katika magereza ambako ni wazi watu wanakumbana na ukatili, vitendo visivyo vya kibin...
Wimbi la wahamiaji kutoka Amerika Kusini kuelekea nchini Marekani

Wimbi la wahamiaji kutoka Amerika Kusini kuelekea nchini Marekani

Jamii, Kimataifa
Wahamiaji kutoka Honduras waingia nchini Guatemala  wakiwa na lengo la kuingia Marekani  kupitia nchini Mexico. Jeshi la Polisi  nchini Mexico limejaribu kuwazuia wahamiaji hao katika moja ya madaraja bila ya kufaanikiwa kuhusu wahamiaji wengine wakichukuwa maamuzi ya kuvuka mto kwa kuogelea. Rais wa Marekani Doanld Trump asema kuwa atatuma jeshi katika mipaka wa nchi yake na Mexico huku akitishia kufuta mikataba iliosainiwa kati ya Marekani na mataifa hayo.
Makumi ya Wayemeni waaga dunia kwa ugonjwa wa dondakoo (Diptheria)

Makumi ya Wayemeni waaga dunia kwa ugonjwa wa dondakoo (Diptheria)

Afya, Jamii, Kimataifa
Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza kuwa tangu mwaka mmoja uliopita hadi sasa watu 141 wameaga dunia kwa ugonjwa wa dondakoo; wengi wakiwa ni watoto wadogo. Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza kuwa zaidi ya watu 2570 wameambukizwa ugonjwa wa dondakoo nchini humo hadi kufikia sasa. Taarfa ya wizara hiyo imeongeza kuwa vita ni chanzo kikuu cha kuenea maradhi ya kipindupindu na dondakoo huko Yemen; vita vilivyoanzishwa dhidi ya raia wa Yemen na muungano vamizi unaoongozwa na Saudia. Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kabla ya kutolewa taarifa ya Wizara ya Afya ya Yemen kwamba  karibu raia wa nchi hiyo milioni 16 wanahitaji misaada na huduma za kiafya. Wakati huo huo WHO imeripoti kuwa mamia ya watu wengine pia wamebainika kuambukizwa ugonjwa wa dondakoo katika mikoa 15 kati ya 22 y
Anne Makinda: Viongozi bora huanzia skuli

Anne Makinda: Viongozi bora huanzia skuli

Jamii, Mikoani
SPIKA mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, amesema skuli zina jukumu la kuwaandaa vijana, kwani wanafunzi wanaoaminishwa kuwa wanaweza kuwa viongozi bora tangu wakiwa wadogo hujenga tabia ya wao kujilinda na kujichunga wenyewe. Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya skuli ya sekondari Imperial (ISS) yaliyofanyika Msolwa Chalinze mkoani Pwani, alisema skuli zina jukumu hilo ili kuandaa viongozi bora wa baadaye. Makinda ambaye alizindua kampeni maalumu ya skuli hiyo inayotambua mchango wa viongozi mbalimbali katika kuhamasisha uongozi bora, alisifia jitihada za skuli hiyo kwa kutambua wajibu na kuanzisha kampeni hiyo mapema wanafunzi wakiwa skuli. Pamoja na kusifia mandhari nzuri ya skuli hiyo, alisema anaamini viongozi wazuri watatoka skulini hapo na kuwasihi waz...
Wanafunzi 3,000 kupewa mikopo – Zanzibar

Wanafunzi 3,000 kupewa mikopo – Zanzibar

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mmanga Mjengo Mjawiri, ameitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar, kuwashirikisha wadau wote wa elimu katika suala la ulipaji wa mikopo ili kurahisisha urejeshaji wa fedha za wananchi. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa bodi hiyo katika muendelezo wa ziara zake katika idara zilizopo chini ya wizara yake hiyo. Alisema, hatua hiyo itasaidia kuondosha tatizo la mrundikano wa madeni yaliyotokana na wanafunzi kutoresha mikopo yao kwa wakati. Alifahamisha kuwa baadhi ya wanufaika wanashindwa kurejesha mikopo baada ya kumaliza masomo yao jambo ambalo linasababisha wenzao kushindwa kukopeshwa. Aliwasisitiza watendaji wa bodi hiyo kuwasimamia wote waliokopeshwa ili kuhakikisha fedha zilizotolewa zirudi n...
error: Content is protected !!