Biashara & Uchumi

Rais Tayyip Erdoğan: Marekani inajaribu kuua kigaidi uchumi wa Uturuki

Rais Tayyip Erdoğan: Marekani inajaribu kuua kigaidi uchumi wa Uturuki

Biashara & Uchumi, Siasa
Kwa mara nyingine Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesisitiza kwamba, Marekani iko nyuma ya vita vya kiuchumi vilivyoanzishwa dhidi ya nchi yake. Rais Erdoğan ameyasema hayo akiwahutubia wafuasi wa chama chake ambapo ametaka kuimarishwa nafasi ya fedha ya kitaifa ya Lira ya nchi hiyo katika mabadilishano na nchi nyingine. "Tunakabiliwa na shambulizi la uchumi wa nchi yetu, na kuporomoka thamani ya sarafu ya Lira ni njama za adui kwa ajili ya kuua kigaidi uchumi wa Uturuki." Amesema Rais Erdoğan. Serikali ya Ankara inafanya juhudi kwa ajili ya kurejesha uthabiti wa sarafu yake ya Lira ambapo tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa fedha hiyo imepoteza karibu asilimia 40 ya thamani yake mkabala wa Dola ya Kimarekani. Sarafu ya Lira iliyopoteza thamani kutokana na njama za Marek
Mzanzibari anayetengeneza Furniture kwa kutumia Pipa

Mzanzibari anayetengeneza Furniture kwa kutumia Pipa

Biashara & Uchumi
Tumezoea kuona bidhaa nyingi zikibuniwa na watu kutoka mataifa ya nje nasisi kuishia kununua tu, lakini wapo vijana wabunifu wenye uwezo wa kutengeneza vitu vyenye thamani kubwa katika kisiwa chetu cha Zanzibar. Silima Borafya Silima mkazi wa Kisonge Mjini Unguja ni Mjasiriamali anayetengeneza Sofa za kisasa, Meza na viti vyake pamoja na Dressing table kwa kutumia Pipa za mafuta.
Watafiti wamepata mabaki ya pombe ya zamani zaidi duniani mjini Haifa, Israel

Watafiti wamepata mabaki ya pombe ya zamani zaidi duniani mjini Haifa, Israel

Biashara & Uchumi
Wataalamu wa vitu vya jadi wakitafuta ushahidi wa vyakula vya mimea baada ya kugundua mabaki ya pombe Watafiti wamefichua kiwanda cha pombe kilicho na mabaki ya pombe yaliodumu takriban miaka 13,000 iliopita katika pango la zamani karibu na mji wa Haifa nchini Israel. Walifikia ugunduzi huo wakati walipokuwa wanafanya uchunguzi kuhusu eneo la makaburi ya jamii ya wafugaji wa kuhama hama ambao walikuwa wawindaji. Utengenezaji wa pombe unadhaniwa kuwepo tangu miaka 5,000 iliopita lakini ugunduzi huu huenda ukabadili historia ya utengenezaji wa kinywaji hicho. Ugunduzi huo pia huenda usiashirie kuwa kileo hicho kilitumika kuoka mikate kama ilivyodhaniwa. Wanasayansi wanasema hawana uhakika ni kitu gani kilivumbuliwa kwanza kati ya pombe na mkate. Vitalu vya vifuniko vilipatikana ...
Tanzania Kukaribisha Wawekezaji wa Nje Kutumia Fursa Ziliopo.

Tanzania Kukaribisha Wawekezaji wa Nje Kutumia Fursa Ziliopo.

Biashara & Uchumi
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sif Ali Iddi akiingia kwenye Ukumbi wa Mikutano ndani ya Viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya 15 ya Biashara Mjini Nanning Guanxi Nchini China kuzungumza na Wawekezaji na Wafanyabishara wa Taifa hilo. Balozi Seif akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Wawekezaji na Wafanyabiashara ulioandaliwa na Tanzania kwa ajili ya kutangaza  fursa za vivutio ilivyonavyo ndani ya  Sekta ya Uwekezaji katika Maonyesho ya Biashara ya 15 ya Biashara yanayoendelea kwenye Mji wa Nanning Jimboni Guangxi Nchini China. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanda Tanzania { Tan Trade } Ndugu Edwin Rutageuka Akitoa Taarifa ya hali za Biashara Nchini Tanzania kwenye Mkutano wa Wawekezaji na Wafanyabiashara. Meneja huduma na mawasiliano wa Mamlaka ya Uwekezaji Vite
Marekani: Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vitaendelea kuwepo

Marekani: Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vitaendelea kuwepo

Biashara & Uchumi
Serikali ya Marekani haitaondoa vikwazo ilivyoiwekea Zimbabwe hadi pale serikali mpya ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo itakapodhihirisha kuwa inabadili mielekeo yake. Hayo yameelezwa na afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya uchumi wa Marekani. Naibu Waziri wa Uchumi na Masuala ya Biashara wa Marekani, Manisha Singh amesema kuwa watu na taasisi 141 za Zimbabwe akiwemo Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe wako chini ya vikwazo vya Marekani.  Amesema mashinikizo ya Marekani kwa Zimbabwe bado yako palepale. Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe Amedai kuwa Washington inajaribu kutumia njia ya mashinikizo ili kushawishi mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na kuheshimiwa haki za binadamu. Naibu Waziri wa Uchumi na Masuala ya Biashara wa Marekani ameon
error: Content is protected !!