Biashara & Uchumi

Kwa kutumia sheria ya ujasusi Marekani imemfungulia mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange mashtaka mapya 17

Kwa kutumia sheria ya ujasusi Marekani imemfungulia mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange mashtaka mapya 17

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Kwa kutumia “sheria ya ujasusi”Marekani yamfungulia mashtaka mapya 17 Julian Assange, mwanzilishi wa ukurasa wa mtandaoni wa WikiLeaks. Taarifa iliyotolewa na wizara ya sheria ya Marekani inasema, Asange amefunguliwa mashtaka mapya 17 kutokana na kujipatia taarifa za ulinzi wa taifa hilo kwa njia zisizo sahihi. Taarifa hiyo inasema Assange pamoja na Chelsea Manning aliyekuwa akifanya kazi kama mchambuzi wa usalama walijipatia maelfu ya nyaraka za siri. Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba kwa kusambaza taarifa hizo za siri ambazo pia zilikuwa zikitaja majina ya watu waliokuwa wakifanya kazi za serikali kisiri kwa njia ya WikiLeaks kungewatia watu hao na Marekani yenyewe hatarini.
Sateliti ya China yaanguka

Sateliti ya China yaanguka

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Teknolojia
Zoezi la kurusha sateliti ya China iitwayo "Yaogan-33" lafanyika bila mafanikio. Kwa mujibu wa habari zilizoripotiwa na shirika la habari la Shinhua. Zoezi la kuirusha Sateliti ya Yaogan-33 lilifanyika katika kituo cha anga cha Taiyuen kilichopo jimbo la  CangChi .Sateliti hiyo ilirushwa kwa kutumia roketi ya Long March-4C. Imefahamishwa kwamba, baada ya kurushwa hatua ya kwanza na ya pili zilipita bila mushkeli, ama katika hatua ya tatu ndipo matatizo yalipotokea. Urushaji huo uliomalizika bila mafanikio uliishia kwa sateliti na mabaki ya roketi kuanguka na kujibamiza ardhini. Huku uchunguzi ukiwa umeanza kufanywa kuhusu zoezi hilo, habari za kuhusu wapi hasa mabaki ya sateliti hiyo yameangukia hazijatolewa. Ifikapo mwaka 2045 China inataka kuwa kiongozi ...
Huawei yaendelea kukabiliwa na changamoto baada ya vikwazo vya Marekani

Huawei yaendelea kukabiliwa na changamoto baada ya vikwazo vya Marekani

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Mtaalam wa Uingereza, anayeunda vifaa maalum vinavyonasa mawasiliano, amesitisha uhusiano wake na kampuni ya mawasiliano ya Huawei, ili kuzingatia hatua ya Marekani kuifungia kampuni hiyo. Hatua hii inaweza kumaliza uwezo wa kampuni ya Huawei kutengeneza vifaa maalum vya kunasa mawasiliano kwa simu zake za kisasa, itakazotengeneza baadaye. Kampuni ya Huawei, sawa na Apple na watengenezaji wengine wa vifaa vya kunasa mawasiliano katika simu kama Qualcomm, zinatumia mfumo wa ARM kutengeneza vifaa vya usindikizaji ambavyo huwasha simu zake. Kampuni ya Huawei imesema inathamini sana uhusiano wake wa karibu na washirika wake, lakini inatambua hali ngumu ambayo baadhi ya washirika wake wanapitia kutokana na maamuzi yanayochochewa kisiasa. Marekani iliipiga marufuku kampu...
Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019

Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019. Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki - idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa. Zaidi ya ujumbe milioni saba za"chuki" pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami. Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina. Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg aliwakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ivunjiliwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuk...
Mtandao wa kimataifa wa wizi wa pesa wavunjwa

Mtandao wa kimataifa wa wizi wa pesa wavunjwa

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa, Teknolojia
Genge la uhalifu wa kimataifa linalotumia mtandao kuiba dola milioni 100 kutoka kwa watu zaidi ya 40,000 limevunjwa. Hii imefuatia operesheni kali ya polisi iliyofanyika katika mataifa ya Marekani , Bulgaria, Ujerumani , Georgia, Moldova na Ukraine. Genge hilo liliweza kuiba kwa watumiaji wa kompyuta zenye programu ya software unaofahamika kama - GozNym malware- iliyotengenezwa kwa lengo la kuvuruga, kuhatribu au kuweza kuingia kwenye mfumo wa kompyuta bila idhini ya mtumiaji ambao ulinasa taarifa za huduma za benki za mtandao na hivyo kuweza kuingia kwenye akaunti za benki. Genge hilo liliwajumuisha wahalifu ambao walitangaza ujuzi wao wa kuiba kupitia mitandao mbali mbali. Taarifa juu ya harakati za kuvunja mtanao wa genge hilo zimetolewa katika makao mak...
error: Content is protected !!