Biashara & Uchumi

India yajibu mapigo, yatangaza ushuru wa juu kwa bidhaa za Marekani

India yajibu mapigo, yatangaza ushuru wa juu kwa bidhaa za Marekani

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Serikali ya India imetangaza ushuru wa juu wa forodha kwa bidhaa 28 za Marekani, ikiwa ni radimali ya nchi hiyo ya Asia kwa vikwazo vya kibiashara vya Washington dhidi yake. Miongoni mwa bidhaa hizo za Marekani ambazo zimeongezewa ushuru mkubwa wa forodha ni bidhaa za chuma, matunda ya tufaha na lozi (almonds) pamoja na jozi (walnuts). Mchumi mmoja ameliambia gazeti la Times of India kuwa, kwa kuongezwa ushuru huo kwa bidhaa hizo za Marekani, serikali ya New Delhi itaweza kupokea ushuru wa ziada wa dola milioni 217. Vita hivi vya kibiashara kati ya New Delhi na Washington viliibuka Machi mwaka jana, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuongeza kwa asilimia 25 ushuru wa forodha wa bidhaa za chuma zinazoagizwa na Marekani kutoka India, na a
Dunia yashindwa kuachana na makaa ya mawe

Dunia yashindwa kuachana na makaa ya mawe

Biashara & Uchumi, Teknolojia
Pamoja na juhudi zinazofanywa kupunguza utoaji wa ukaa duniani, takwimu zinaonyesha kwamba mwaka uliopita umeme zaidi (10100 terawatt “tW”) ulizalishwa kwa kutumia makaa ya mawe. Mwaka 2018 kiasi cha umeme uliozalishwa duniani kilikuwa 26614 tW.  Kati ya kiasi hicho kilichozalishwa kiasi kikubwa zaidi 10100 tW zilizalishwa kutokana na makaa ya mawe. Kiasi kikubwa kilichofuatiwa 6182 tW kilizalishwa kutokana na gesi asilia, 4193 tW zilizalishwa kutokana na umeme wa maji, Nishati ya nyuklia ilizalisha umeme kiasi cha 2701 tW. Nishati safi inayoweza kutumika upya ilitoa kiasi cha 2480 tW cha umeme. Katika nchi zilizoongoza kwa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe, China ilishika namba 1 ikifuatiwa na Marekani kisha India.Kwa upande wa umeme wa nguvu za maji Saudia iliong
Russia yaishukuru Iran kwa juhudi zake za kuwaokoa mabaharia wa meli zilizoshambuliwa

Russia yaishukuru Iran kwa juhudi zake za kuwaokoa mabaharia wa meli zilizoshambuliwa

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa shukurani zake za dhati kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na juhudi zake za kuwaokoa mabaharia wa Kirusi waliokuwa kwenye meli mbili za mafuta zilizoshambuliwa siku ya Alkhamisi katika maji ya Bahari ya Oman. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia sambamba na kuishukuru Iran kwa hatua hiyo, pia imelaani vikali shambulizi dhidi ya meli hizo. Kadhalika wizara hiyo imetaka kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kuzuia hali ya mambo kuwa mbaya zaidi katika eneo la Asia Magharibi na kuongeza kuwa, utolewaji tuhuma dhidi ya upande fulani kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufanyika uchunguzi wa kimataifa usiopendelea upande wowote ni jambo lisilokubalika. Alkhamisi iliyopita vyombo vya habari viliripoti kujiri shambulizi...
Mahakama yasimamisha disko hoteli ya Ngalawa

Mahakama yasimamisha disko hoteli ya Ngalawa

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
MAHAKAMA Kuu ya Zanzibar imepiga marufuku shughuli zote za muziki katika hoteli ya Ngalawa iliyopo eneo la Kihinani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja. Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu katika kesi ya madai namba 72 ya mwaka 2016, katika uamuzi wake imetoa amri ya kusitisha upigaji muziki katika hoteli hiyo hadi hapo ombi hilo litakaposikilizwa pande zote mbili. Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na mahakama hiyo na kusainiwa na Mrajis wa Mahakama Kuu, Mohamed Ali Mohamed kwenda kwa hoteli hiyo ya Juni 13 mwaka huu, uongozi wa hoteli hiyo umetakiwa kutekeleza amri hiyo. Nakala ya uamuzi huo imepokelewa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Bububu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi na Sheha wa Shehia ya Chuini kwa ajili ya utekelezaji wa amri ya mahakama. Kesi hiyo ya m...
Real Madrid yamtambulisha mchezaji wake ghali zaidi kupata kumnunua

Real Madrid yamtambulisha mchezaji wake ghali zaidi kupata kumnunua

Biashara & Uchumi, Michezo
Timu ya soka ya Real Madrid imemtambulisha kwa mashabiki na waandishi wa habari nyota wa soka wa Ubelgiji aliyehamia katika timu hiyo Eden Hazard. Hazard katika utambulisho huo alisema tangu alivyokuwa mtoto ndoto yake ilikuwa ni kucheza soka katika timu ya Real Madrid. Hazard amehamia Real Madrid akitokea Chelsea kwa malipo ya Euro milioni 100, kwa kiasi hicho Hazard amevunja rekodi ya uhamisho kwa timu ya Real Madrid, mara ya mwisho Madrid kulipa pesa nyingi za uhamisho ilikuwa ni kwa nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo ambaye alihamia klabu hio akitokea Manchester United mwaka 2009 kwa uhamisho wa dola milioni 96. Mashabiki elfu 50 walijitokeza kushuhudia utambulisho wa Hazard, huku utambulisho wa Ronaldo bado unashikilia rekodi kwa kuhudhuriwa na mashabiki elfu 70.
error: Content is protected !!